FT: Tanzania 0-1 Uganda | AFCON Qualifier | Benjamin Mkapa Stadium | 28.03.2023

FT: Tanzania 0-1 Uganda | AFCON Qualifier | Benjamin Mkapa Stadium | 28.03.2023

Screenshot_2023-03-28-19-32-58-974_com.allfootball.news.png
 
Mechi haitakuwa rahisi kwa Taifa Stars ila tunawaombea angalau sare
 
Kila la heri Taifa Stars...

Mechi ya leo ni ngumu sana kwa Stars, kuna kitu kinaniambia tunapoteza hii mechi...

Eenh Mungu epushilia mbali...
 
Majira ya Saa 2:00 Usiku kwa Masaa ya Afrika ya Mashariki, Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) itashuka dimbani Benjamin Mkapa kuwaalika Uganda (The Cranes) katika mchezo wa nne wa kundi F kuelekea kufuzu Afcon mwaka 2023..

Taifa Stars yenye point 4 iliyopo nafasi ya pili nyuma ya vinara Algeria ambao washafuzu itashuka dimbani ikiwa na kumbukumbu yakuibuka na ushindi wa 1-0 siku chache zilizopita.

Taifa Stars ikishinda itafikisha alama 7 na kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu kwa mashindano hayo makubwa na adhimu kwa bara la Afrika kwa mara ya 3 katika historia ya mashindano hayo.

Tujitokeze kwa wingi tushangilie timu yetu ya Taifa, hatuna timu nyingine jamani.

Mechi itakuwa mubashara AzamtV, Dstv kupitia chaneli 225 ya kifurushi cha POA.

Kila la heri Taifa Stars!
Kila la heri Tanzania!!!
Game haitakuwa Nyepesi hata kidogo...
Hawana budi kukaza sana
 
Uniform za benchi la ufundi zimekaa kama za Yanga bana. Ni kama khanga imevaliwa juu ya blauzi. Mambo ya Sheria Ngowi haya nini 🤣😂🤣
 
Back
Top Bottom