Makelele kIbao timu bovu tukiwaambia utopolo kimataifa bado katika ligi ya bongo jamaa wamenunua sana mechi nyie mkafikiri ni uwezo wao matokeo yake wakienda kimataifa wanagongwa kwa jinsi walivyocheza Leo wanatoka mapema tu mdomo mwingi timu hakuna kima nyie
We jamaa uko na akili sawa sawa kweli?? Yaan Yanga walinunua mechi zipi hizo pamoja na za Simba zote 4 mlizokutana??
Binafsi leo nilitaka kuangalia zaidi maingizo mapya kama yako sawa au la, na niseme wazi Yanga imeimarika sana, tena sana tu.
BIGIRIMANA 8/10 amepiga pasi za uhakika nyingi, anatulia, nguvu na ball control nzuri. Kwa nafasi yake ya kiungo, naona katikati patakuwa na mchuano mkubwa sana. Naona wazi Mwamnyeto akilizoea benchi taratibu sambamba na Sure boy na nafasi zao zikitawaliwa na BANGALA NA BIGIRIMANA.
AZIZ KI 8/10 Jamaa ana nguvu, ball control, speed na macho makali mno, kwa nafasi yake na kwa nilivyomuona Feisal akiwa mzito kuendana na kasi ya KI itakuwa ngumu mno kucheza pamoja, kama KI ataanza basi namba 10 asimame KAMBOLE mwenye Speed na mikimbio yenye kuhisi pasi kutoka kwa kiungo wake. KI atokee kulia na MOLOKO benchi linamuhusu vizuri sana.
LOMALISA 8/10 Hatimaye tumeweza kuwa na beki 3 bora kwa miaka ya karibuni kwa tuliomuona MARCELO basi tunasema hapa Yanga wamepata mtu, mtulivu, mwenye speed, pasi sahihi na hata nguvu ya Kubattle.
MORRISON 5/10 Hajacheza vizuri leo, ingawa ni mchezaji machachari na mjanja sana, inatakiwa sasa mtu kama Mayele na Feisal wawe sharp sana kusoma akili na mikimbio ya huyu jamaa. Welldone boys.
KWA NILIVYOINGALIA YANGA LEO HII, NAWEZA KUSEMA KIKOSI CHA KWANZA CHA MSIMU UJAO KITAKUWA IFUATAVYO.
Hii ni kwa CAF
1. DIARRA
2. DJUMA
3. LOMALISA
4. BANGALA
5. MWAMNYETO
6. BIGIRIMANA
7. KI AZIZ
8. AUCHO
9. MAYELE
10. FEISAL
11. MORRISON
Kwenye Ligi Kuu naona kuna nafasi zaidi kwa SURE BOY, JOB, KIBWANA, MOLOKO nk.