FT: Wydad AC 1 - 0 Simba SC | CAFCL | Stade de Marrakech | 09.12.2023

FT: Wydad AC 1 - 0 Simba SC | CAFCL | Stade de Marrakech | 09.12.2023

Huyu kocha akipewa wachezaji wazuri kisha waamini katika project badala ya mihemuko ya muda mfupi, ataisuka vizuri mno Simba Sc.
 
Kibu ni mkabaji mzuri tu.
Tangu nimeanza kumuona, akikaba Kati ya mara 5 basi mara 3 lazima acheze faulo! Anaonekana ni striker anayependa sana kuisidia timu kurudisha mpira lakini kukaba penyewe hajui.... Anatumiaga manguvu mengi sana kuliko maarifa.

Kibu akiwa anawania mpira wa juu na beki ni mara chache sana atau win bila kusababisha faulo.

Afanye kuangalia sana video za idol wake Didier Drigba aone jinsi gani alivyokuwa anakaba.

Binafsi nafikiri angebadilisha aina ya uchezaji akafocus zaidi kwenye finishing kuliko kujiongezea majukumu ambayo hayawezi.
 
Back
Top Bottom