FT: Wydad Casablanca 1-0 (Penati 4-3) Simba S.C | CAF Champions League | Simba yaondolewa kwa mikwaju ya penati

FT: Wydad Casablanca 1-0 (Penati 4-3) Simba S.C | CAF Champions League | Simba yaondolewa kwa mikwaju ya penati

Kama ambavyo mlimuona TP Mazembe mchovu kwa kuwa kapigwa na Yanga bila kujali Yanga ni wazuri pia
 
Hapa ndio wengi mnapofeli

Yani kwasababu Simba imecheza vizuri na kuwazuia Wydad washindwe kufanya kile ambacho wengi walikifikiria, ndio sababu ya kufanya waonekane dhaifu?

Kabisa hujaona nafasi ya kutoa appreciation kwa Simba badala yake unaona Wydad ndio walikuwa dhaifu?
Ni wewe huyo leo unaona umuhimu wa appreciation??lini uliwahi kuitoa kwa wananchi walipofanya vizuri?kila anaefungwa na Yanga kwako ww unamuona dhaifu leo umeambiwa wydad ya msimu huu dhaifu unakaza meno.
 
Usisahau kuwa ni yaleyale mliyowashia moto uwanjani mkala faini
Tabia za wachezaji zisizo za kimaadili si msimamo wa Club. Wachezaji wanasajiliwa,wanakuja na kuondoka na tabia zao.
 
Tabia za wachezaji zisizo za kimaadili si msimamo wa Club. Wachezaji wanasajiliwa,wanakuja na kuondoka na tabia zao.
Ni club ndio maana iliwajibika kwenye kulipa faini.. kwanini caf hawakumpiga mchezaji mmojammoja?
 
Hahahaa! Ujue hadi nikawaza hivi hawa ndo MaChampions kweli ama.

Ila hawa mlipaswa kuwamalizia Kwa Mkapa.

#PoleMtani.
Yah dawa Yao ni kuwachakaza nyumbani goli za kutosha. Hao ndo Machampion ni kwamba Simba ubora umeongezeka na mbinu za Kocha.
 
Hapa ndio wengi mnapofeli

Yani kwasababu Simba imecheza vizuri na kuwazuia Wydad washindwe kufanya kile ambacho wengi walikifikiria, ndio sababu ya kufanya waonekane dhaifu?

Kabisa hujaona nafasi ya kutoa appreciation kwa Simba badala yake unaona Wydad ndio walikuwa dhaifu?
Wewe hukufuatilia michezo yote ya CAF mwaka huu. Sijui unatumia TV services zipi lakini tuliofuatilia michezo yote ya CAF tutakuambia kuwa Wydad walikuwa wanamtegemea mchezaji mmoja tu, ambaye akibanwa basi wanashindwa kutoboa. Mbinu iliyoptumia na timu za AS Vita za kumbana mchezaji huo ndizo pia zilizotumiwa na Simba. Timu inayotegemea mchezaji mmoja ni timu dhaifu, na kwa vile timu zote zilozobaki zimeshaujua udhaifu huo; ngoja tusubiri matokeo.

Kuhusu appreciation yangu kwa simba tafuta utaikuta huko nyuma.
 
Back
Top Bottom