Wakuu leo ndiyo leo, mtoto hatumwi dukani, ngoma ya mtoto haikeshi, usiku wa deni haukawii kukucha.
Leo majira ya saa 10:00 jioni, katika dimba la Benjamin Mkapa, Yanga watashuka dimbani katika mchezo wao dhidi ya Al Hilal ya Sudan katika Ligi ya Mabingwa Afrika. Ikumbukwe, katika michezo yao ya awali, Yanga waliwatoa Zalan na Al Hilal wakawatoa St. George ya Ethiopia.
Yanga inafundishwa na Kocha Prof. Nabi huku wapinzani wao wakinolewa na Kocha Ibenge. Iwe jua iwe mvua timu ya Yanga inahitaji ushindi wa kuanzia goli 3 ili kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele.
Mechi itakuwa mubashara kupitia Azam Sports 1HD.
Sent from my Infinix X657 using
JamiiForums mobile app