FT: Yanga 1-1 Al Hilal Club (CAF Champion League) | Mkapa Stadium | 8-10-2022

FT: Yanga 1-1 Al Hilal Club (CAF Champion League) | Mkapa Stadium | 8-10-2022

Kwann Simba wako bize na mechi Yanga.....huku wakiamini Yanga wanafungwa.....wkt mechi yao ni kesho ....Je wana uhakika wao wanashinda?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hizi ndio zile game za ukipata nafasi itumie instantly, hazina muda wa kukupa nafasi ya kurekebisha makosa yako kipindi cha pili, kazi kwenu.
Ukimuona Mwamnyeto kwenye lineup ya leo, basi tegemea lawama nyingi sana leo. Hizi ndio zile mechi za kuwakataa baadhi ya wachezaji na kushangaa imekuwaje wapo klabuni mpaka leo.
 
Kabla haijafika saa 12 Jioni ya Leo wewe utakua wakwanza kutoa shutuma dhidi ya Al Hilal.
Wewe una risiti yako niliitunza kitambo sana, kabla ya saa 12 kila mwanasoka asiyekuwa na mihemuko atakuja kucheka hapa.
Screenshot_20221007-215423.jpg
 
Yamebaki masaa ma3 nchi iingie kwenye wingu la aibu
Tusubiri kaka maana mpira ni dakika 90.

Acha tusubiri tuone tulichoandaliwa na professor Nasridine Nabi na Ibenge Flolentine ndani ya dk 90.
 
Washabiki wengi wa Simba wanatafuta furaha maana timu Yao haiwapi furaha na ndo maana unaona wanahangaika na kukosoa kila kitu.
Unapata nini kuongea uongo?
 
Wakuu leo ndiyo leo, mtoto hatumwi dukani, ngoma ya mtoto haikeshi, usiku wa deni haukawii kukucha.

Leo majira ya saa 10:00 jioni, katika dimba la Benjamin Mkapa, Yanga watashuka dimbani katika mchezo wao dhidi ya Al Hilal ya Sudan katika Ligi ya Mabingwa Afrika. Ikumbukwe, katika michezo yao ya awali, Yanga waliwatoa Zalan na Al Hilal wakawatoa St. George ya Ethiopia.

Yanga inafundishwa na Kocha Prof. Nabi huku wapinzani wao wakinolewa na Kocha Ibenge. Iwe jua iwe mvua timu ya Yanga inahitaji ushindi wa kuanzia goli 3 ili kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele.

Mechi itakuwa mubashara kupitia Azam Sports 1HD.



Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Hadi sasahivi huna picha za uwanjani halafu unakuwa na haraka ya kuanzisha uzi
 
Hadi sasahivi huna picha za uwanjani halafu unakuwa na haraka ya kuanzisha uzi
Hili swala la picha kutowekwa linatupa tafsiri tofauti sana kwa sisi ambao tuliaminishwa ticket zimejaa na kwamba itawekwa rekodi ya uwanja kujaa saa 4
 
Kila la heri Alhilal piga 5-0 hao young African sports Club
 
Back
Top Bottom