Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Utambulisho huo utakamilishwa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya mabingwa wa Kagame Cup, Red Arrows kutoka Zambia.
=====
00' Kipenga kimepulizwa kuashiria mwanzo wa mchezo uwanja wa Benjamin Mkapa, Yanga 0-0 Red Arrows.
04' Red Arrows wanapata free kick ya kwanza kuelekea Yanga baada ya Boka kumdondosha Anthony.
06' ⚽ Rick Banda anaitanguliza Red Arrows kwa bao la mapeeema, ni mpira wa kichwa.
07' Almanusura Pacome airejeshe furaha ya wanayanga baada ya gonga kadhaa, juhudi zinashindwa kuzaa goli.
13' Aucho yuko chini baada ya kuwania mpira wa juu na Banda. Anarejea uwanjani baada ya kupata huduma ya kwanza.
15' Mzize anajaribu shuti kali kutoka nje ya 18 lakini mpira unapaa juuu ya lango la Red Arrows.
21' Yanga wanapata kona na kuianzisha chap chap, mipango yao inashindwa kufanikiwa.
24' Red Arrows wanapata kona mbili mfululizo, Diarra anauweka mikononi barabara.
25' Baleke anapata mpira maridhawa lakini filimbi ya offside inalia.
26' Yanga wanaumiliki mpira langoni kwa Red Arrows bila kupata bao.
28' Boka anaingiza krosi ya kasi lango la Red Arrows, mpira unatoka upande wa pili bila kuguswa.
29' Dickson Job anatoa boko, Red Arrows wanashindwa kutumia nafasi
30' Chama anapambana peke yake, mabeki wa Arrows wanamzidi ujanja
31' Abuyaaaa, mlinda mlango anatema shuti kali la Abuya.
33' Pacome anapunguza mtu ndani ya box na kumpa Mzize, mpira wa kichwa unaenda juu ya lango.
35' Abuya anajaribu tena, mpira unaenda pembeni ya lango.
37' Mzizee anakwenda kwa kasi, anamkuta mlinda mlango wa Arrows amekaa imara anamsubiri.
39' 🟡Mubili analamba kadi ya njano ya kwanza kwenye mchezo
39' Chama anafanya kile anachoweza zaidi, mpira wa free kick unagonga mtambaa wa panya. Chama alidondoshwa nje kidogo ya 18
41' Pacome anaingia mwenyewe kwenye 18, beki anamchomoa.. Kona
45' 🟡Mchee anapewa kadi ya njano baada ya kudunda mpira chini akiashiria kutokubaliana na maamuzi ya refa. Alitumia ugali kumtoa Pacome kwenye njia.
45+2' Duke Abuya anapasua mkwaju wa tatu, mlinda mlango wa Arrows anamwambia hajaribiwi.
45+3' Mpira unaenda mapumziko, Yanga 0-1 Red Arrows
45' Mbugi imerejea, Yanga wamerudi na uzi wa njano huku Arrows wakivaa nyekundu.
47' Yanga imerejea na mabadiliko makubwa kwenye kikosi, hadi mlinda mlango, Diara ameenda benchi.
57'🔴 Mubili anapewa nyekundu baada ya kupata kadi ya pili ya njano, aliumia akiwa nje ya uwanja lakini alirejea kutibiwa ndani ya uwanja