FT: Yanga 5-0 Zalan (Agg 9-0) | Caf Champions League | Mkapa Stadium | 17-09-2022

FT: Yanga 5-0 Zalan (Agg 9-0) | Caf Champions League | Mkapa Stadium | 17-09-2022

Teko Modise

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2017
Posts
2,331
Reaction score
7,733
Mchezo wa pili baina ya Yanga dhidi ya Zalan kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, leo Jumamosi Septemba 17, 2022, ni Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mchezo wa kwanza Yanga ilishinda kwa mabao 4-0.

Kumbuka mshindi wa mchezo huu ataenda kukutana na mshindi kati ya Saint George ya Ethiopia na Al Hilal ya Sudan.

Timu zimeshaingia uwanjani kwa ajili ya mchezo huu.
Fc3bf4_WAAEjTmj.jpg
Mchezo umeanza...

10' Yanga wanatawala muda mwingi

18' Zalan wanaonekana kucheza kwa utulivu lakini muda mwingi mpira upo kwa wachezaji wa Yanga

45' Mpaka sasa Yanga imepiga jumla ya mashuti 11 ambayo hayajalenga lango la Zalan

45' Mashuti ya Yanga ambayo yamefika langoni mwa Zalan ni mawili

MAPUMZIKO: Yanga 0-0 Zalan

Kipindi cha pili kimeanza

46' Yanga wameendelea walioishia wanapiga pasi nyingi

GOOOOOOOOOOOOOOOO

47' Farid Musa anaipatia Yanga bao la kwanza
Farid amefunga kwa shuti kali akimalizia pasi nzuri ya Fei Toto.
Fc3ybvKWYAIwZ2H.jpg
50' Yanga wameongeza presha na wanafika langoni kwa Zalan mfululizo

56' GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Azizi Ki anaipatia Yanga bao la pili

59' GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Fiston Mayele anafunga bao la tatu kwa shuti la mbali, kipa anabaki anautazama mpira

62' GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Mayele anafunga bao la nne kwa Yanga

64' Yanga imetawala mchezo, wanapiga pasi muda mwingi na mpira wanaumiliki wao.

66' GOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Mayele anafunga bao la tatu kwake na la tano kwa Yanga

76' Kasi imepungua kwa timu zote

80' Mayele anaomba kutoka baada ya kuumia. Anaonekana akishika sehemu ya nyuma ya paja

81' Mayele ametolewa uwanjani akichechemea

90' Zimeongezwa dakika 4 za nyongeza

Mwamuzi anamaliza mchezo

FULL TIME: Yanga 5-0 Zalan FC
 
Zalan ni mbovu ila Yanga ndio mbovu zaidi

Aziz Ki ye na kipa kakosa

Mayele kakosa magoli zaidi ya manne

Yanga wangekutana na hii timu ambayo inacheza na Geita nadhani tungekuwa tunaongea habari nyingine
 
Hawa Zalan nadhani hata njaa ina olay part yake washindwe kuwa na ubora kwenye mchezo

Wanaanguka anguka sana unaweza hisi miguu imekosa uloto
 
Back
Top Bottom