First leg ya kule Mali aliyekuwa anafokewa sana ni Mudathir sio Aziz K. Aziz Ki aliingia Sub na ndiye aliyeongeza uhai kwenye kutengeneza mashambulizi kama sikosei yeye ndiye aliyehusika kwenye pasi ya mwisho kwenye goli la Mayele kule Mali.
Kuhusu kiwango chake, sikatai kuna baadhi ya mechi kaonesha kiwango kisichoridhisha kwa kosa la kujirudia rudia la kupoteza mipira ovyo. Lakini hilo ni kawaida kwa wachezaji kwavile ni binadamu haiwezekani kuwa na ufanisi ule ule kila siku. Kwenye mpira wa miguu kuna wachezaji ambao hutokea kutopendwa na mashabiki wa timu mahasimu halafu kuna wachezaji hutokea kutopendwa na wa timu husika.
Mwanzoni alikuwa Mayele ndiye mchezaji anayeongoza kwa kupondwa na mashabiki wa Simba, maneno yakawa ni mengi na wakiangalia mpira wao wanaangalia tu makosa ya Mayele. Sasa baada ya kumalizana na Mayele wameamua kubadilika na kuwa match analyst wa Aziz Ki na wanachofurahia kuona ni makosa na kisha kuyakuza ila yale mazuri hayakuzwi.
Aziz Ki mara nyingi sana anaifanya timu itengeneze nafasi, akipata mipira anaitenga kwenye maeneo yenye nafasi lakini unakuta hakuna mtu, anachukua mipira kisha anaachia na kuifungua ngome ya wapinzani na huwa anarudi hadi nyuma kusaidia katika ukabaji. Mchezo unaweza kumkataa mchezaji akawa yupo nje na mchezo..
Kwanini Mayele anayekosesha nafasi za wazi kibao sana tena kwenye mechi zaidi ya nne hamuuimbi kuwa Yanga imepigwa?