FT: Yanga SC 0-0 Mamelodi Sundowns | CAF CL | Mkapa Stadium | 30/03/2023

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610

Match Day 1st Leg.
Robo fainali

Yanga vs Mamelodi

Muda ni Saa 3 Usiku.

Kuwa hapa nami kwa update za kabla na wakati wa mchezo


Kikosi cha Yanga


Kikosi cha Mamelodi Sundowns

Mchezo umeanza
10' Mchezo bado una Kasi ndogo, timu zinasomana
20' Wageni wanamiliki mpira muda mwingi lakini Yanga wanafanya mashambulizi ya kushtukiza
27' Yanga wanafanya shambulizi Kali, shuti la Musonda linadakwa
30' Mchezo unaendelea kwa ushindani mkali
31' Shambulizi lingine langoni kwa Mamelodi lakini kipa anaudaka mpira.
32' Mapumziko ya dakika moja
42' Mamelodi wanapiga shuti la kwanza golini
45' Zinaongezwa dakika 3

MAPUMZIKO

Kipindi cha pili kimeanza
50' Mchezo umeanza kuchangamka, timu zote zinafunguka
55' Yanga wamefanya mashambulizi mawili makali lakini yote walikuwa wameotea
61' Kipa wa Yanga, Diarra anafanya kazi nzuri ya kuokoa mpira wa krosi uliokuwa na hatari
62' Timu zote zinapeana zamu kumiliki mpira
75’ Shambulizi kali langoni kwa Yanga lakini mpira unaondolewa
77’ Dakika moja ya mapumziko kwa timu zote
83’ Yanga wanaongeza presha ya kutafuta goli
87' Kasi ya mchezo imeongezeka
90' Zinaongezwa dakika 5

FULL TIME
 
Mwamba kawawin Wanajangwani Wote!!

Hii ya leo ni halali, amewatangulia wote!!
Nilikuwa nacheki tu for the records.

Suley2019 alikuwa wakwanza kupost.
Check screenshot zangu!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…