Wildchild
JF-Expert Member
- Aug 29, 2018
- 19,411
- 21,938
Wewe suburi Saa kumi na moja na busy tuu,🤸🤸Ukadhani kuashinza uzi ndio mtashinda? Utopolo subiri saa 1
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe suburi Saa kumi na moja na busy tuu,🤸🤸Ukadhani kuashinza uzi ndio mtashinda? Utopolo subiri saa 1
Huo ni utabiri was atakavyo kufa mikia fc🦁
Yanga nimewaona kwa mzee Maarifa bagamoyo wanaoga mitishambaSaa sita usiku,siku ishabadilika mtopolo umejiwai kuweka uzi,wenzio usiku huu wapo Pemba wanaroga.
Hivi kuna app yoyote naweza kucheki hii mech live kupitia simu?Naaam, wasalam wakuu,
Ile siku maalumu iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu hatimaye imefika. Pambano lenye hadhi la watani wa jadi katika soka la bongo, Yanga na Simba.
Karibuni katika matukio mubashara (live updates) ya mtanange huu wa kukata na shoka baina ya mahasimu wa soka la Bongo #KariakooDerby Yanga na Simba, utakaochezwa saa 11 jioni Estadio De Benjamin Mkapa leo jumapili 23-10-2022.
Huu ni mchezo wa namba 64 wa Ligi Kuu ya NBC 2022/2023, Yanga akiwa ni mwenyeji wa mchezo wa leo dhidi ya mtani Simba.
Mchezo uliyopita wa Ligi Kuu msimu wa 2021/2022 uliochezwa April 30, 2022, timu hizi zilitoshana au kuchoshana nguvu kwa sare ya bila kufungana/suluhu ya 0-0. Kwa maana hiyo huu ni mchezo wa mzunguko wa kwanza kwenye msimu wa 2022/2023.
Timu hizo zinaingia uwanjani zikiwa na alama 13 kila moja, lakini Simba ipo kileleni kutokana na wingi wa mabao ya kufunga na kufungwa dhidi ya Yanga ambayo inashika nafasi ya pili, kila moja amecheza mechi tano.
Pia michezo mingine (Derby) ya hivi karibuni ni ule wa Mei 28, 2022 kwenye nusu fainali ya Azam Sports Federation Cup ambapo, Simba alifungwa goli moja bila majibu, ambapo shuti kali la Feisal Salum ‘Fei Toto’ liliwalaza na viatu mashabiki wa Simba siku hiyo.
Vilevile mnamo Agosti 13, 2022 kwenye mechi ya ngao ya Hisani, Simba alitepeta tena kwa Yanga kwa kufungwa goli 2 kwa moja. Fiston Mayele "Mzee wa kutetema" akiingia kambani mara mbili siku hiyo na mashabiki wa Simba wakitoka vichwa chini.
Kwa miaka ya karibuni Simba imekuwa ikishindwa kupata ushindi mbele ya Yanga katika michezo ya Ligi Kuu Bara kwani mara yao ya mwisho kushinda ilikuwa bao 1-0, Februari 16, 2019 lililofungwa na mshambuliaji, Meddie Kagere.
Kwenye mechi za kimataifa, tarehe 16/10/2022 Yanga imetolewa kwenye michuano ya CAF CL na Al Hilal baada ya kufungwa 1-0 na kushukia kwenye michuano ya CAF CC ambapo pia amepangiwa Club Africain kwenye mchezo wa Play off kuelekea makundi.
Pia Simba mechi ya mwisho kimataifa imetoka kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya Primeiro De Agosto ya Angola na hivyo kufuzu hatua ya makundi ya CAF CL.
Je, leo itakuwaje baina ya miamba hii miwili? Nani ataibuka kidedea? kaa nami hapa mwanzo, kati na mwisho kupata kila kinachojiri kutoka katika dimba hili lenye kumbukumbu nzuri ya Hayati Benjamin Mkapa Dar es Salaam.
Azam Sports 1 HD wataurusha mpambano huu mubashara (live).
Je, "Watatetema" au "watapiga saluti?" Hahaha #𝑯𝒂𝒊𝒏𝒂𝑴𝒃𝒂𝑴𝒃𝒂𝑴𝒃𝒂
Aise hii comment ya dhahabu[emoji123][emoji126][emoji126]Simba ikicheza Tanzania mpka caf wanakuwa na furaha last born wa caf [emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]
Safi sana mwananchi kwa kuwawahi makolo kuanzisha uzi, leo watapoteana.
Umeandika mikojo mitupu kama ulivyo ubongo wako uliojaa mafilifili kima weweTukutane hapa saa Moja Usiku...
Waliaji na washangiliaji wote turudi humu baada ya Mechi. Hii Mechi imebeba zaidi hatima ya Kocha Nasreddine Nabi (Professa feki) kuliko Juma Mgunda (Guadiola Bonge).
Simba wameshapunguza Presha ya mchezo kwa kujiweka nafasi ya kufungwa wakati Yanga wao wamejiweka kwenye nafasi ya kushinda kutokana na Historia mbovu ya Simba mbele ya Yanga kwa miaka mitano iliyopita.
Matokeo yake Simba ikifungwa hakutakuwa na la ajabu, wakati Yanga ikifungwa Nabi atakumbushiwa na Zigo la kutolewa Klabu Bingwa Afrika. Kiuhalisia Simba wameshaishinda vita ya Kisaikolojia wakati Yanga Presha iko juu 220/110. Yanga Ikifungwa lazima watu wapigwe Stroke leo!!
Andiko liko juu ya uwezo wako wa kuelewa. Yanga ikifungwa Nabi Out, Simba ikifungwa Mgunda anakwenda "Kurekebisha makosa". Subiri uone.Umeandika mikojo mitupu kama ulivyo ubongo wako uliojaa mafilifili kima wewe
Andiko liko juu ya uwezo wako wa kuelewa. Yanga ikifungwa Nabi Out, Simba ikifungwa Mgunda anakwenda "Kurekebisha makosa". Subiri uone.
Hahahaha. Ghazwat akianzisha uzi aghalabu mnyama anashinda.Huyu akianzisha uzi huwa Yanga anafungwa.
Wapinga Mungu wanasema mambo yote hutokea kwa sababu na si kwa kudra ya Mungu. Ila wao hata hawajui nani atafungwa ama kushinda.Hapo ndipo Mungu anapoonyesha uweza wake, haujui siku wala saa utakaposhinda au kupata kichapo, just wait and see.