FT: Yanga SC 4-1 Mtibwa Sugar | NBC Premier League | Azam Complex | 16.12.2023

Kwahiyo Simba nayo mbovu?
Sasa Hilo swali? Simba NI kikundi cha wahuni Tu waliookotana.

Mpaka sasa Saido hayupo katika orodha ya wafungaji, utashangaa bado mechi 3 Ligi iishe wakicheza na wahuni wenzao Saido atafunga goli 10 mechi moja naye utaambiwa anagombea ufungaji Bora.
 
Tuwaulize nyie ambao ndiyo huwa mnalilia hizo mambo ya clean sheet au sasa hivi haina maana kwa kuwa hamzipati tena?
Kumfunga mtu 5-1 au 4-1 hakuwezi kuwa sawa na aliyeshinda 2-1 au 3-2 kwasababu ya kitu kinachoitwa goal difference. Pamoja na Yanga kumzungumzia kuwa anapata tabu kupata clean sheet lakini mpaka sasa ana goal difference ya 24 kwa michezo 10 huku timu yako ya Simba ikiwa na goal difference ya 10 kwa michezo 9. Huku Azam fc akiwa na goal difference ya 21 kwa michezo 12. Yanga ana mtaji mkubwa wa nagoli akiwa ameruhusu magoli machache na kufunga mengi.
 
Tulikataza kujielezea sana. Msimu uliopita mlivyokuwa mnaambiwa Simba ana hizo takwimu za kufunga magoli mengi na kufungwa machache mkawa mnakejeli leo inakuwaje mnaona ni jambo muhimu.

Na clean sheet ni clean sheet haijalishi umefunga goli 2 au goli 10 au umetoka suluhu, haina uhusiano wowote na hayo mambo mengine maana hata Simba alipokuwa anashinda 3-1 bado mlisema ina beki mbovu kisa haikupata clean sheet
 
Tulikataza kujielezea sana. Msimu uliopita mlivyokuwa mnaambiwa Simba ana hizo takwimu za kufunga magoli mengi na kufungwa machache mkawa mnakejeli leo inakuwaje mnaona ni jambo muhimu
Hizo takwimu zikawasaidia nini kwa mwaka jana hadi uje kutamba nazo hapa?
 
Hizo takwimu zikawasaidia nini kwa mwaka jana hadi uje kutamba nazo hapa?
Kwani wewe hizo takwimu una uhakika gani zitakusaidia hadi unatamba nazo hapa. Unaongea utadhani siyo mtu wa mpira
 
Kwani wewe hizo takwimu una uhakika gani zitakusaidia hadi unatamba nazo hapa. Unaongea utadhani siyo mtu wa mpira
Nimetamba au nimekuelewesha ujue maana ya goal difference wewe uliyekuja na wimbo wa Yanga hapati clean sheet
 
Nimetamba au nimekuelewesha ujue maana ya goal difference wewe uliyekuja na wimbo wa Yanga hapati clean sheet
Unahoji kwa kejeli GD imeisaidia nini Simba halafu wakati huo huo "unaelewesha" Yanga ina GD bora. Haujitambui dogo
 
Unahoji kwa kejeli GD imeisaidia nini Simba halafu wakati huo huo "unaelewesha" Yanga ina GD bora. Haujitambui dogo
Hiyo kejeli umeiona wapi zaidi ya wewe kujistukia kuwa una upeo mdogo wa kuujua mpira? Kama ungekuwa unajua mpira, usingehoji habari za clean sheet kwa timu yenye wastani wa kufunga magoli zaidi ya mawili kwa kila mchezo. Ungehoji habari za clean sheet kama timu zingefungana 2:1 au 4:3 lakini sio kwa ushindi wa 5:1 ( goal difference ni sawa na 4 hapo) au 4:1 ( ni sawa na 3 kwa 0)
 
Unajitungia sheria zako. Clean sheet ni clean sheet bwashee
 
Unajitungia sheria zako. Clean sheet ni clean sheet bwashee
Naona nampigia mbuzi gitaa, nazungumzia goal difference wewe umekazana na clean sheet haya kazana na clean sheet tuone kama ligi inaangaliwa clean sheet au goal difference.
 
Nazungumzia goal difference wewe umekazana na clean sheet haya kazana na clean sheet tuone kama ligi inaangaliwa clean sheet au goal difference.
Post yangu ilihusu clean sheet wewe ukaingiza hoja ya GD halafu ukibanwa unasema haviingiliani wakati wewe ndiyo umechanganya madesa. Cha kushangaza zaidi unabeza kitu hicho hicho unachotaka kionekane ni muhimu
 
Huu ni msimamo, je unaona kwenye huo msimamo kuna clean sheet hapo?
 
Huu ni msimamo, je unaona kwenye huo msimamo kuna clean sheet hapo?
View attachment 2844967

Sipendagi kudhalilisha mtu ila ukinilazimisha nitafanya hivyo na uzuri JF wamefanya rahisi sana kudhalilisha watu kama nyie. Embu pitia hizo post uangalia ulivyokuwa unaziongelea hizo clean sheet.
 
Sipendagi kudhalilisha mtu ila ukinilazimisha nitafanya hivyo na uzuri JF wamefanya rahisi sana kudhalilisha watu kama nyie. Embu pitia hizo post uangalia ulivyokuwa unaziongelea hizo clean sheet.
Unataka tuanze kujadili kila comment? Haya twende kazi tuanze na comment yangu ya kwanza nanukuu "Huu msimu tusipoangalia ipo siku tutakuja kupigwa kipigo kibaya mno, kuna mashimo mengi sana kwenye safu yetu ya ulinzi.

Tunakoenda huko ndio kugumu zaidi maana tunakutana na timu bora zaidi. Timu ya Yanga imekuwa ni timu isiyoweza kupata clean sheet hata kwa Mbuni FC. Hilo siyo jambo zuri kabisa kwenye mchezo unahitaji kuvuka kwa aggregate.

Litibiwe mapema hili tatizo."

Mwisho wa kunukuu.
Hiyo ni comment umeitoa kwenye uzi wangu Yanga tuna matatizo ya mipira ya kutengwa
Ambapo nilikuwa nazungumzia madhaifu ya Yanga katika mipira ya kutengwa hasa timu ikielekea katika mashindano ya CAF champions league mwaka jana 2022.. Zingatia hapo niliposema "aggregate " kwasababu mimi ni mtu wa mpira najua athari ya kuruhusu goli ni shida linapokuja swala la aggregate na ndicho kilichokuja kutokea tukatolewa na Al hilal na kwenye CAFCC magoli mengi Yanga ilifungwa kwa mipira ya kutengwa hapo mwanzoni rejea mechi ya Monastir, Tp Mazembe.
Kwahiyo nilichokiandika kwenye huo uzi kilienda kutokea kwenye michuano ya CAF. Una lingine kabla sijaenda kwenye comment nyingine?
 
Sikushangai maana najuaga una kichwa kigumu mixed na ukweli kuwa ulishaapa kwa katiba ya Yanga kuwa bishana hadi ufe. Halafu hauna hata chembe ya aibu. Najua umesoma ukaona jinsi post zako mwenyewe zilivyokuumbua unatafuta pa kutokea haupaoni. Sasa hivi unabeti nichoke nikuache.

Soma hapa ulipokuwa dalali wa IFFHS

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…