FT: Zambia 0-1 Tanzania | Kufuzu Kombe la Dunia | Levy Mwanawasa Stadium | 11/06/2024

FT: Zambia 0-1 Tanzania | Kufuzu Kombe la Dunia | Levy Mwanawasa Stadium | 11/06/2024

Taifa stars imecheza vizuri mno na kushinda japo baada ya Mao kutoka katikati kulikuwa na gap kubwa mno hasa second half Zambia wakatawala mchezo na kushambulia sana na kupiga shuti hatari mno, huyu Mtasingwa bado sana bora hata angecheza Mkude. Alikaa nyuma sana na kukaribisha mashambulizi hatari karibu na goli letu, ilikuwa roho mkononi!!

Kitu cha pili Taifa stars ijifunze kukaba kitimu kwa nguvu kama Yanga hatutafungwa ovyo.

Balua alipambana ila hakuwa na wa kuchezeshana nae. Hilo wakaliangalie

Fei alicheza vizuri mno japo alileta utoto alipopata nafasi nzuri ya kushoot badala yake akaanza mbwembwe kutaka kupiga chenga timu nzima, akue sasa, akumbushwe mchezo mkubwa nafasi za kufunga ni chache asizichezee.

Lusajo ni beki imara sana basi asaidiwe maana upande wake hakupata msaada mara nyingi akikaba wachezaji wawili.

Otherwise Hemed Morocco ameprove ni bonge la kocha na anaweza kuibeba Taifa stars. Nilitamani kumuona Msindo pia.
Andiko zuri, ila limechafuliwa na hao vyura uliowasifia himid mao na faisal.. himid hamna k2, yupo slow sn, faisal kacheza chini y kiwango, utoto mwingi
 
Back
Top Bottom