Fuata haya kulinda mahusiano na watu wenye pesa au hadhi zaidi yako

Fuata haya kulinda mahusiano na watu wenye pesa au hadhi zaidi yako

safuher

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2019
Posts
12,312
Reaction score
18,194
1. Ukitaka kuzoeana na watu wenye pesa zao kamwe USIWAZOWEE

2. Usije kumpigia simu kumsalimia kila baada ya siku kadhaa ikawa ndo desturi yako, acha hiyo atakuwa hapokei simu zako.

Kumbuka thamani ya salamu ni pale tunapowasalimia watu ambao wanaona umuhimu wetu na sio ambao tunaona umuhimu wao"

3. Ukitaka kumtembelea usimpe taarifa kama unaenda, wewe nenda ukimkuta piga stori kama hujamkuta aga ondoka.

4. Ikiwa umemkuta ulipomtembelea chonde chonde chonde usijaribu kukaa muda mwingi; kaa muda mchache zaidi ujifanye una haraka ulipita mara moja tu.

Usije ukala chakula baada ya kwenda ghafla, labda iwe walikualika

Kumbuka "kuwatembelea matajiri ni kama kuwatembelea wagonjwa" kwa maana hawataki usumbufu

5. Kama kakuita kwa shida fulani nyumbani kwake hakikisha unaifanya kwa ucheshi na bashasha na kuipenda kazi hiyo lakini ukimaliza usikae tena ondoka hapo.

6. Ukitaka matajiri wakuheshimu basi jifanye huna muda nao.

7. Hakikisha kabla ya kuonana nae uwe na mambo ya msingi ya kuongea nae, sio unaonana nae mara mnakaa kimya alafu wewe ndo umemfuata na hajakuita, unampotezea muda wake.

8. Usije kumlalamikia shida yoyote ile hata kama huna nia ya kumuomba,kwa maana usilalamikie chochote mbele yake yeye atahisi unamuomba kijanja atakuona mzushi hufai kuwa karibu nae.

acha yeye ndo ajue shida yako kupitia yeye mwenyewe kuona au asimuliwe na wengine kwamba wewe una shida.

Kulalamika shida mbele ya tajiri ni mwiko!

9. Usiwe unakubali vipesa anavyokupa kwa kumsaidia kazi ambazo hazina utaalamu kama vile kusukuma gari,kumsaidia kuingiza mzigo ndani n.k

Akikupa chochote mwambie usijali mkuu kawaida tu kusaidiana sisi wanadamu.

Hapo kiakili ataona na yeye ana deni la kukusaidia wewe kwa wema unaomfanyia hivyo inaweza kumpa fikra akupe mchongo fulani wa pesa na mambo mengine.

Ataona kwamba mali sio ishu kubwa kwako na kumbuka matajiri hawapendi watu wanaopenda mali zao,wanapenda watu wasiojali mali zao matajiri.

10. Usimhoji kabisa kuhusu mali zake kazipata vipi ili na wewe upite njia hizo, usimhoji usimhoji usimhoji!

Kufanya kinyume na haya ni kutaka kuonekana msumbufu na atakuepuka alafu utapoteza malengo yako kama ulitaka kupata connection ama msaada wake.
 
11. Tajiri hana urafiki na maskini, ukipata chance ya kupiga mpige kiswasawa ukaanze mbele! Ukisubiri huruma utasubiri sana, narudia tena utasubiri sana!

Matajiri wenye huruma walipotea miaka 10 iliyopita!

Teknolojia imekuja na matajili wenye roho mbaya tupu
 
Urafiki na tajiri hujengwa kinyume na vile unavyojengwa urafiki na masikini.
 
11. Tajiri hana urafiki na maskini, ukipata chance ya kupiga mpige kiswasawa ukaanze mbele! Ukisubiri huruma utasubiri sana, narudia tena utasubiri sana!
Matajiri wenye huruma walipotea miaka 10 iliyopita!
Teknolojia imekuja na matajili wenye roho mbaya tupu
Unampigaje mtu kizembe?..

no wonder inabidi ukiwa tajiri uwe mkax tu
 
10.usimhoji kabisa kuhusu mali zake kazipata vipi ili na wewe upite njia hizo,usimhoji usimhoji usimhoji !!.
Hii point naielewa vzr..

Kuna tajiri mmoja mtaani alikuwa rafiki yangu sana.... Tuliweza kuwa marafiki nadhani kwasababu sikuwahi kumuomba pesa wala kumueleza shida yangu yoyote....
Urafiki wetu uliisha baada ya kumuuliza swali njia alizopitia mpaka kuwa na biashara kubwa ( ili nijifunze na mm ) ,,

Kwanzia hio siku akawa ananikwepa
 
Binafsi huwa naona ni bora kuwa na marafiki wachache wenye tija, kuliko kuwa na marafiki/jamaa wengi wasio na tija.

Mbinu moja huwa naitumia, ili kupima utija wa rafiki/jamaa kwangu; Huwa namuomba msaada!

Rafiki mwenye tija, hutoa majibu mazuri hata kama hana na urafiki unaendelea. Lakini rafiki asiye na tija, huvunja urafiki hapo hapo. Kama ulituma sms ndiyo haitajibiwa kamwe.
 
Njia za kujaribiana zilishapitwa na wakati.

Ukiwa na shida mtu anajua.

"Shida ya uongo haiwezi kuleta msaada wa kweli"

Usijaribu kuwapoteza marafiki kwa vipimo vya uongo aise.

Subiri upate shida kweli alafu uone nani atakusaidia mkuu
 
9. Usiwe unakubali vipesa anavyokupa kwa kumsaidia kazi ambazo hazina utaalamu kama vile kusukuma gari,kumsaidia kuingiza mzigo ndani n.k
Aisee hii huwa nafanya sana... Yaan kwa sehemu nayopigia job, kwa siku 5000 Tshs. inaingia!

Itakuwa nakosea kumbe!?
 
Njia za kujaribiana zilishapitwa na wakati.

Ukiwa na shida mtu anajua.

"Shida ya uongo haiwezi kuleta msaada wa kweli"

Usijaribu kuwapoteza marafiki kwa vipimo vya uongo aise.

Subiri upate shida kweli alafu uone nani atakusaidia mkuu
Binadamu wa sasa hivi hatueleweki, bila kujaribiana unaweza kuachwa kwenye mataa. Ukajua nina rafiki kumbe hamna mtu!

Zamani ndio ilikuwa rahisi kusaidiwa na rafiki ukipata shida. Lakini siku hizi, baadhi ya marafiki wanadumisha urafiki pale tu, mnapokuwa wote hamna changamoto. Ukipata changamoto kidogo, rafiki anaingia mitini hata simu hapokei. Hivyo, lazima nimjaribu mapema rafiki nijue mwelekeo wake kuliko kupoteza muda kujenga urafiki usio na tija.
 
Sawa mkuu nimekuelewa japokuwa kwangu haimake sense ila nimekuelewa mtazamo wako mkuu
 
Back
Top Bottom