PreGE2025 Fuatilia LIVE Kesi dhidi ya Tundu Lissu. Inasikilizwa muda huu mahakamani

PreGE2025 Fuatilia LIVE Kesi dhidi ya Tundu Lissu. Inasikilizwa muda huu mahakamani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Tundu Lissu inasikilizwa leo Mei 6, 2025 na itakuwa kwa njia ya mtandao.

===
UPDATE

Link imekatwa na hivyo haitakuwa rahisi kufuatilia
 
Safi kabisa mambo ya kisasa haya tunayapata lives bila kwenda kujazana kisutu.
NO REFORM NO ELECTION, BUT ELECTION IS A MUST!
 
Pi no. 8897 Jamhuri vs Tundu Lissu mbele ya Mh. Kiswaga RM. Hapa Kisutu Mahakamani ile kesi ya Uhaini.

Hakimu Kiswaga anauliza kama Jamhuri wako tayari wanaanza kuongea kwa kukoroma.

Upande wa Jamhuri mtandao wao unasumbua hawasikiki vizuri. Tunazo dakika kadhaa hapa kesi inashindwa kuendelea. Hakimu anawaambia wahakikishe vifaa vingine wamezima kama vile simu ndio maana mtandao na mawasiliano yao yanasumbua.

*******************

#MUENDELEZO_WA_KESI_YA_UHAINI_JAMUHURI_DHIDI_YA_LISSU_02

Kama kawaida hapa mahakamani wapo Mabarozi kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Jumuiya ya Ulaya. Nao wamefika na kufuatilia kesi hii. Hawa mabarozi hawajawahi kukosa hata siku moja kufika mahakamani. Wanapaswa kupewa maua yao. Pamoja na kwamba mawakilinwa serikali huwa wanaongea kiswahili lakini wao wanaelewa maana huwa wanakuja na wakalimani wao. Wamejipanga vizuri wanaelewa kila kitu. Wanakabia juu kwa kifupi.

Wanasikika sasa Jamhuri, I kupendeza Hakimu Thawabu Yahaya yupo pia Job Mrema, Cathbert Mbiringi na Harrison lukosi. Sisi wote tunaiwakilisha serikali kwenye shauri hili.

Na kabla hatujaendelea naomba upande wa utetezi wajitambulishe.

Anajitambulisha kiongozi

1. Mpale Mpoki
2. Dr. Nshala
3. Jebra Kambole
4. Hekima Mwasipu
5. Jeremiah Mtobesya
6. Maria Mushi
7. Catherine Michael
8. Michael Mwangasa
9. Michael Lugina
10. Sisty Masawe
11. Deogratias Mahinyila
12. Jacob Mogendi
13. Deus Singa
14. Edward Heche
15. Maduhu Kulwa William.
16. Glory Olomi
17. Peter Kibatala pia yupo walisahau kumtambulisha mahakama imeibua kicheko.

Thawabu Yahaya Wakili wa serikali anaulizia kama mtuhumiwa nae yupo au vipi wanaulizwa watu kutoka gerezani.

Mimi ni kamishna msaidizi Juma Mwaibago nimewasiliana na mshitakiwa anasema hawezi kupanda mahakamani kwa njia ya mtandao.

Anauliza kama amesikika. Mheshimiwa hakimu anamjibu kuwa amesikika.

*******************

#MUENDELEZO_WA_KESI_YA_UHAINI_JAMUHURI_DHIDI_YA_LISSU_03

Wakili wa serikali, Thawabu Yahaya anasema kwa vile mahakama ilisema tutakutana kwa njia ya mtandao na kwa majibu ya magereza kuwa mshitakiwa amegoma.

Sasa mahakama inao wajibu wa kuamua ni kwa namna gani inaweza kuamuru ili mshitakiwa aweze kufika mahakamani.

Lakini pia shauri lilikuwa kwa kutaja na upelelezi haujakamilika tunaomba tarehe nyingine.

Anaanza Mpale Mpoki, mheshimiw tunashangaa kuambiwa upelelezi hadi leo ni siku ya 27 kwanini upelelezi bado wakati mashtaka yenyewe yako wazi kabisa.

Hivyo kwetu sisi tunashangaa sana kwasababu mteja ana haki ya kesi yake kusikilizwa kwa haraka. Hati ya mashitaka inajieleza wanapeleleza nini? Hawahitaji kwenda forensic wala eneo lolote, naamini makarasi ya kutengeneza PI mnayo mengi tu na wino pia upo kwakweli. Siwaelewi.

Jamhuri wanaulizwa na hakimu nini kinakwamisha upelelezi.

Anajibu shauri hili linahitaji mambo mengi kwahiyo bado tunaendelea na upelelezi na ukikamilika tutawasilisha.

Wakili wa serikali anasema sheria haitulazimishi tuseme ni lini tutakamilisha upelelezi.

Mpale Mpoki anasema Mheshimiwa tunapotoa maelezo ya jumla kuwa hawalazimishwi kusema wamefikia wapi na watakamilisha lini.

Committal maana yake wanakusanya ushahidi sasa watuambie walichoshindwa kukusanya huo ushahiidi. Tunadeal na maisha ya mtu hapa. Wanaposema hakuna sheria inayosema watakamilisha lini kwahiyo wanataka kukaa na Lissu miaka 300?

Ukiwa tayari.... ni lini utakamilisha ndio tunachotaka sisi waseme hapa. Tafadhali

Mtobesya anaongeza kuwa Mheshimiwa baada ya kutoa ombi la kuahirisha kesi kwa mujibu wa kifungu cha 248 kuwa ukiomba ahirisho that one is not a free lunch. Kwamba utaenda kula tu bila kugharamia.

Hakuna cha bure katika kuahirisha ahirisha kesi. Ni lazima useme kwanini unataka kuahirisha na kwasababu gani unataka ahirisho.

Sisi tunasema kwa nature ya kesi hii kuahirisha sio reasonable na wanasema hawalazimiki kusema wamefikia hatua gani.

Msimamo wetu ni kwamba hawana reasonable cause ya kuahirisha hii kesi

Thawabu wakili wa serikali anasema sisi tumesema upelelezi bado tunaomba ahirisho na taratibu za upelelezi hatuko tayari kuzisema hadharani kwani sheria haitulazimishi na wao wanalalamika tu.

Mpoki anasema hawa watu hawako serious kama hawana makaratasi na vitabu vya committal waseme twende mahakamani.

Mpoki anasema Tone Tone itachangia hizo karatasi kama hawana. Maana hapa huyu wakili wa Serikali anasema hizo karatasi watatoa wao tukitaka. Jibu hilo hapo la Tonetone amepatiwa na Mpale Mpoki.

INAENDELEA..!
 
Back
Top Bottom