PreGE2025 Fuatilia LIVE Kesi dhidi ya Tundu Lissu. Inasikilizwa muda huu mahakamani

PreGE2025 Fuatilia LIVE Kesi dhidi ya Tundu Lissu. Inasikilizwa muda huu mahakamani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Teknolojia, TEKNOLOJIA
Kama imewashinda si warudi kwenye jadi yetu? Kwani tunaweza nini sisi??

479667084_1255440875940864_7068794020907267846_n.jpg
 
Pi no. 8897 Jamhuri vs Tundu Lissu mbele ya Mh. Kiswaga RM. Hapa Kisutu Mahakamani ile kesi ya Uhaini.

Hakimu Kiswaga anauliza kama Jamhuri wako tayari wanaanza kuongea kwa kukoroma.

Upande wa Jamhuri mtandao wao unasumbua hawasikiki vizuri. Tunazo dakika kadhaa hapa kesi inashindwa kuendelea. Hakimu anawaambia wahakikishe vifaa vingine wamezima kama vile simu ndio maana mtandao na mawasiliano yao yanasumbua.

*******************

#MUENDELEZO_WA_KESI_YA_UHAINI_JAMUHURI_DHIDI_YA_LISSU_02

Kama kawaida hapa mahakamani wapo Mabarozi kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Jumuiya ya Ulaya. Nao wamefika na kufuatilia kesi hii. Hawa mabarozi hawajawahi kukosa hata siku moja kufika mahakamani. Wanapaswa kupewa maua yao. Pamoja na kwamba mawakilinwa serikali huwa wanaongea kiswahili lakini wao wanaelewa maana huwa wanakuja na wakalimani wao. Wamejipanga vizuri wanaelewa kila kitu. Wanakabia juu kwa kifupi.

Wanasikika sasa Jamhuri, I kupendeza Hakimu Thawabu Yahaya yupo pia Job Mrema, Cathbert Mbiringi na Harrison lukosi. Sisi wote tunaiwakilisha serikali kwenye shauri hili.

Na kabla hatujaendelea naomba upande wa utetezi wajitambulishe.

Anajitambulisha kiongozi

1. Mpale Mpoki
2. Dr. Nshala
3. Jebra Kambole
4. Hekima Mwasipu
5. Jeremiah Mtobesya
6. Maria Mushi
7. Catherine Michael
8. Michael Mwangasa
9. Michael Lugina
10. Sisty Masawe
11. Deogratias Mahinyila
12. Jacob Mogendi
13. Deus Singa
14. Edward Heche
15. Maduhu Kulwa William.
16. Glory Olomi
17. Peter Kibatala pia yupo walisahau kumtambulisha mahakama imeibua kicheko.

Thawabu Yahaya Wakili wa serikali anaulizia kama mtuhumiwa nae yupo au vipi wanaulizwa watu kutoka gerezani.

Mimi ni kamishna msaidizi Juma Mwaibago nimewasiliana na mshitakiwa anasema hawezi kupanda mahakamani kwa njia ya mtandao.

Anauliza kama amesikika. Mheshimiwa hakimu anamjibu kuwa amesikika.

*******************

#MUENDELEZO_WA_KESI_YA_UHAINI_JAMUHURI_DHIDI_YA_LISSU_03

Wakili wa serikali, Thawabu Yahaya anasema kwa vile mahakama ilisema tutakutana kwa njia ya mtandao na kwa majibu ya magereza kuwa mshitakiwa amegoma.

Sasa mahakama inao wajibu wa kuamua ni kwa namna gani inaweza kuamuru ili mshitakiwa aweze kufika mahakamani.

Lakini pia shauri lilikuwa kwa kutaja na upelelezi haujakamilika tunaomba tarehe nyingine.

Anaanza Mpale Mpoki, mheshimiw tunashangaa kuambiwa upelelezi hadi leo ni siku ya 27 kwanini upelelezi bado wakati mashtaka yenyewe yako wazi kabisa.

Hivyo kwetu sisi tunashangaa sana kwasababu mteja ana haki ya kesi yake kusikilizwa kwa haraka. Hati ya mashitaka inajieleza wanapeleleza nini? Hawahitaji kwenda forensic wala eneo lolote, naamini makarasi ya kutengeneza PI mnayo mengi tu na wino pia upo kwakweli. Siwaelewi.

Jamhuri wanaulizwa na hakimu nini kinakwamisha upelelezi.

Anajibu shauri hili linahitaji mambo mengi kwahiyo bado tunaendelea na upelelezi na ukikamilika tutawasilisha.

Wakili wa serikali anasema sheria haitulazimishi tuseme ni lini tutakamilisha upelelezi.

Mpale Mpoki anasema Mheshimiwa tunapotoa maelezo ya jumla kuwa hawalazimishwi kusema wamefikia wapi na watakamilisha lini.

Committal maana yake wanakusanya ushahidi sasa watuambie walichoshindwa kukusanya huo ushahiidi. Tunadeal na maisha ya mtu hapa. Wanaposema hakuna sheria inayosema watakamilisha lini kwahiyo wanataka kukaa na Lissu miaka 300?

Ukiwa tayari.... ni lini utakamilisha ndio tunachotaka sisi waseme hapa. Tafadhali

Mtobesya anaongeza kuwa Mheshimiwa baada ya kutoa ombi la kuahirisha kesi kwa mujibu wa kifungu cha 248 kuwa ukiomba ahirisho that one is not a free lunch. Kwamba utaenda kula tu bila kugharamia.

Hakuna cha bure katika kuahirisha ahirisha kesi. Ni lazima useme kwanini unataka kuahirisha na kwasababu gani unataka ahirisho.

Sisi tunasema kwa nature ya kesi hii kuahirisha sio reasonable na wanasema hawalazimiki kusema wamefikia hatua gani.

Msimamo wetu ni kwamba hawana reasonable cause ya kuahirisha hii kesi

Thawabu wakili wa serikali anasema sisi tumesema upelelezi bado tunaomba ahirisho na taratibu za upelelezi hatuko tayari kuzisema hadharani kwani sheria haitulazimishi na wao wanalalamika tu.

Mpoki anasema hawa watu hawako serious kama hawana makaratasi na vitabu vya committal waseme twende mahakamani.

Mpoki anasema Tone Tone itachangia hizo karatasi kama hawana. Maana hapa huyu wakili wa Serikali anasema hizo karatasi watatoa wao tukitaka. Jibu hilo hapo la Tonetone amepatiwa na Mpale Mpoki.

INAENDELEA..!
Inasikitisha sana
 
Mbinu za Dola ni zilezike za kipuuzi siku zote.

Yaan siku 27, bado unasema upelelezi bado, Hawa wajinga hawana kesi yoyote ya msingi isipokua wanataka kumcheleweshea LISSU tu.

Na niwaambie, atakapoachiwa tu, hiyo mikutano itakavyojaa , Traore hatofikia.


Nahisi, wanataka waulazimishe uchaguzi kufanyika, alafu wakishajitangaza, WATOE Zuio la mikutano.
 
Mbinu za Dola ni zilezike za kipuuzi siku zote.

Yaan siku 27, bado unasema upelelezi bado, Hawa wajinga hawana kesi yoyote ya msingi isipokua wanataka kumcheleweshea LISSU tu.

Na niwaambie, atakapoachiwa tu, hiyo mikutano itakavyojaa , Traore hatofikia.


Nahisi, wanataka waulazimishe uchaguzi kufanyika, alafu wakishajitangaza, WATOE Zuio la mikutano.
Ni kweli kabisa
 
#MUENDELEZO_WA_KESI_YA_UHAINI_JAMUHURI_DHIDI_YA_LISSU_04

Hakimu anasema mawakili wote wazingatia language of the Court.

Hakimu anaendelea, Natoa wito fanyeni upelelezi na tarehe ijayo mtupatie status. Hatuwezi kutoa tarehe kila siku bila kujua shauri limefikia wapi wapi. Natoa siku 14 kwahiyo itakuwa tarehe 20/05/2025 mje na status ya upelelezi na sio maneno matupu. Lazima kuwe na ukomo wa kupeleleza.

Kwahiyo naahirisha shauri hadi tarehe hiyo.

Hakimu Kiswaga anashauriana na MAWAKILI wanakubaliana tarehe 19/05 ndio kesi itakuja badala ya Tarehe 20/05. Kwasababu tarehe hiyo Dr. Nshala hatakuwepo.

Tukutane Tar. 19/05/2025 asubuhi saa tatu.

Tunaanza kesi ya pili sasa ile ya kusambaza taarifa za uongo. Sauti ya askari imetoka kinyongee sio kama ya siku zote

Courttttttttt sijui hajala huyu askari leo.

Hakimu amekaaa. Anafungua laptop yake.

Anasubiriwa kalani aseme neno

Hakimu anasema shauri la jinai anataja namba ya kuwakaribisha Mawakili na pande zote. Anauliza kama magereza wanampata na mawakili wa serikali wapo.

Anaanza Wakili wa Serikali anajitambulisha.

Hakimu anauliza kuhusu mshitakiwa?

Anasimama JUMA KAPILIMA Mkuu wa Gereza Ukonga anawakilisha huko.

Anasema Mshitakiwa alijulishwa na alisema hawezi kuendelea na shauri lake kwa njia ya mtandao. Amejulishwa na amesema hawezi kufika kwenye eneo hili kushiriki katika shauri hili kwa njia ya mtandao.

Hakimu anasema imetosha imetosha tulia kidogo. Inaonekana huyu magereza yuko vibe sana aiseee.

Haya Jamhuri wanaanza.

Naitwa Thawabu Issa, Wakili wa serikali Mwandamizi, Job John Mrema, Cathbert Mbiringi na Harrison Lukosi.

Wakili wa utetezi naitwa 1. Mpale Kaba Mpoki
2. Ruge Nshala
3. Jebra Kambole
4. Peter Kibatala
5. Hekima Mwasipu
6. Jeremiah Mtobesya
7. Peter Kibatala.
8. Maria Mushi
9. Deogratias Mahinyila
10. Michael Mwangasa
11. Michael Lugina
12. Sisty Masawe
13. Jacob Mogendi
14. Deus Singa
15. Edward Heche
16. Maduhu William.
17. Glory Olomi
18. Edson Kilatu
19. Ikoti Lissu
20. Matthias Mlimi
21. Ferdinand Makore

Thawabu Yahaya Issa Wakili wa serikali anasema shauri linakuja kwa maamuzi madogo na sisi tuko tayari.

Mpale Mpoki na sisi tuko tayari kama wewe uko tayari na umeandika pamoja na matatizo ya Bungeni na huko mitaani maana mambo yaliyosemwa na akina Bashungwa na Mwanasheria wa Serikali. Mpoki anasema tuko tayari kusikiliza makatazo yako. Hakimu anasema mbona kama una pre empty maamuzi sasa? Hapana ndio iko hivyo anakazia Mpoki.

Haya tusikilize sasa maamuzi madogo ya Hakimu kuhusu hoja ambazo ziliibuliwa na mawakili wa utetezi. Tunaenda hatua kwa hatua.

Kama kawaida mabalozi wapo hapa nawaona.

INAENDELEA..!
 
#MUENDELEZO_WA_KESI_YA_UHAINI_JAMUHURI_DHIDI_YA_LISSU_05

Na waandishi kadhaa pia wako ndani ya mahakama humu nao wanafuatilia.

Tunaambiwa kuna Wakili mmoja pia amekamatwa pale getini kapelekwa central alikataa kuserchiwa na watu asiowafahamu. Amewahoji nyie ni akina nani huwa hatuwaoni kila siku.

Hakimu anasema nikishasoma baada ya dakika 20 mtapata nakala ya uamuzi wangu.

Anajiandaa kuanza kusoma na anasema atasoma kwa kifupi sana.

Anauliza kama tunaiskilizana vizuri.

Shauri lilikuwa kwa hoja za awali wakati linakuja na zikaibuka hoja kadhaa ikiwemo kuwa hoja hizo zilipaswa kusomwa kwenye mahakama ya wazi na sio kwa mtandao, Mshitakiwa ni lazima awepo mahakamani mwenyewe na sio kwa utaratibu huu, Je hasa nini maana ya mahakama ya wazi na mahakama ilikosea kusema isikilize kwa njia ya mtandao na mwisho hoja za awali zikishasomwa lazima kuna nyaraka zitolewe na pia kuna nyaraka lazima ziandaliwe na zisainiwe na mshitakiwa na mawakili wake. Je mambo hayo yatafanyikaje wakati mshitakiwa hayupo.

Pia, Mawakili wa utetezi wamezuiwa kumuona mteja wao kule Ukonga magereza, na pia mshitakiwa amegoma kuja mahakamani kusikiliza kesi yake kwa njia ya mtandao.

Mahakama iliwasikiliza pande zote na Mr. JOB MREMA aliongoza Jopo la Serikali na Mpale Mpoki aliongoza jopo la utetezi.

Katika kusikiliza shauri hili na mapingamizi haya mahakama ilisikiliza bila kuwepo mtuhumiwa.

Kwa kifupi yalisemwa mengi kuhusiana na mambo niliyosema hapo juu.

Kumbukeni anasoma ruling kwa Kingereza. Hata kama mimi sio mwanasheria lakini akili ninazo za kuwatafsiria mdogo mdogo kama hivi.

Preliminary hearing ( hoja za awali) zinapaswa kusomwa kwenye mahakama ya wazi ni matakwa ya sheria na mahakama hii ilishajifunga mikono kwasababu ilishasema tarehe inayofuata mahakama hii itakutana open court sasa iwaje tena tulikutana ghafla bila taarifa kuhusu kusikiliza kwa njia ya mtandao.

Na hata kama ilipaswa kusikilizwa kwa njia ya mtandao ilitakiwa kutolewa notice ya siku saba kabla ya tarehe ya kesi ili kesi iweze kusikilizwa kwa mtandao kwa sababu ndio kanuni za kusikiliza mashauri kwa mtandao inahitaji.

INAENDELEA..!
 
Live : Jaji Mkuu - Mahakama tuna wataalamu wazuri sana wa TEHAMA Teknolojia ya Habari na Mawasiliano


View: https://m.youtube.com/watch?v=SHb3-lEojFc

🎙️ Mgeni Rasmi: Mheshimiwa Prof. Ibrahim Hamis Juma,Jaji Mkuu wa Tanzania📍 Mahali: Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC), Dar es Salaam📅 Tarehe: 24 Aprili, 2025
Source : Mahakama ya Tanzania
 
#MUENDELEZO_WA_KESI_YA_MTANDAO_JAMUHURI_DHIDI_YA_LISSU_02

Suala kuhamishwa kutoka Keko kwenda ukonga pia nalo halikuwa kwa mujibu wa kisheria. Tulipaswa kuelezwa kuanzia mawakili hadi ndugu. Kitendo cha kuzuia Mteja wetu asikutane na Viongozi wake wa dini pia lilikuwa ni suala la kinyume cha sheria.

Wakaomba mtuhumiwa aletwe mahakamani, aruhusiwe kuonana na mawakili wake na ndugu zake. Pia wakaomba maafisa wa magereza waitwe na kusema kwanini wanamzuia mteja wetu kupata haki zake.

Upande wa Serikali Mrema alisema mahakama hii haina mamlaka ya kujadili mambo haya kwa mujibu wa sheria na walipaswa kwenda kufungua kesi ya Judicial Review na sio njia hii waliyoitumia hapa.

Kusikiliza kesi kwa mtandao inawezekana na mahakama hii iko sahihi na kuhusu kutolewa kwa vidhibiti vingetolewa kwa njia ya mtandao hivyo hivyo kwahiyo haiwezi kuwa kikwazo cha kusikiliza kesi kwa njia ya mtandao.

Kuhusu mahakaam ilishaaamua huko nyuma kuhsuu kesi kusikilizwa mahakama ya wazi wao wanaamini kuwa hata hii kwa njia ya mtandao ni mahakama ya wazi tu.

Kuhusu kuhamishwa kwa mtuhumiwa kutoka keko to Ukonga hakuna shida ni mambo ya magereza sisi hayatuhusu.

Kuhusu siku saba hilo sio jambo la msingi uzuri taarifa ilishapelekwa kwa pande zote kwahiyo ilikuwa sahihi na wakamaliza kwa kuomba kuwa mahakama iendelee na Hoja za awali isizingatie maombi ya utetezi.

INAENDELEA..!
 
Back
Top Bottom