Full interview: Diamond amesema kuhusu Ommy Dimpoz, Ali Kiba, nani mkali, Rihanna na Ross

Full interview: Diamond amesema kuhusu Ommy Dimpoz, Ali Kiba, nani mkali, Rihanna na Ross

STUNTER

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Posts
13,076
Reaction score
17,247

Diamond amefunguka kuhusu jitihada zilizowahi kufanywa ili kumaliza bifu lake na Ommy Dimpoz. Ni muda mrefu wawili hao wamekuwa hawaelewani japo hakuna aliyewahi kuweka wazi chanzo cha ugomvi huo.

Akiongea na kipindi cha XXL cha Clouds FM, Diamond amethibitisha kuwa aliwahi kutafutwa na Dimpoz pamoja na kuwatuma watu ili wayamalize.

“Kashatuma watu wengi sana, kashamtuma Sallam, alishanipigia mpaka na simu nikashindwa kupokea nitaongea naye nini,” alisema.

“Mipaka ilivuka halafu mimi ni muislam. Mimi sina matatizo na watu ndio maana wakijaribu kushindana na mimi huwa wanashindwa. Hata ukiniangalia sina hata pete ya kijani kwenye vidole vyangu,” aliongeza.

Hata hivyo wakati Diamond akihojiwa, Ommy Dimpoz alitweet kukanusha alichokisema.

“Aisee kumbe @Sallam_SK kila siku unavyonibembeleza tuyamalize na Mwana kumbe nakutuma, kweli nyie profeshenooo ,” ametweet Ommy.

“Wazee @BDozen @CloudsMediaLive Naombeni Kipindi Kesho ,” ameongeza.

Wakati huo huo Sallam amemjibu Ommy:

Sijakuomba mie! Kumbuka aliyekwambia nani Na mie nilijibu nini? Hata wakati ulipokuja kuomba yaishe na mie kumbuka nani alikuleta!

Bifu ya Ommy na Diamond imeongezeka zaidi kuanzia jana baada ya kutoka kwa wimbo wa Rich Mavoko ‘Kokoro.’ Wawili hao wametupiana vijembe kwenye Instagram.
 
Kawaelezeni sasa yeye anapata pesa nyie imbeni na sauti zenu nzuri zitawasaidia baadae
 
Ingekuwa muziki ni sauti,basi ningemsainisha wema sepetu >>>DIAMOND.
Mimi sina pete ya kijani vidoleni >>>> DIAMOND.
Ningekuwa nanunua viewers nisingepewa tuzo na Youtube >>>DIAMOND.
Mimi ninafanya shoo karibia Afrika nzima,sasa wewe masikini ya Mungu hata kenya unaenda kwa msaada wa jamaa yako>>>DIAMOND.
 
Nilishawahi kuwaomba tufanye shoo ya nani zaidi,wakakataa hata January makamba nilimuomba uzamini na hata Babu Tale shahidi >>>DIAMOND.
Mimi nataka kama wanataka busta kutoka kwangu basi waje live sio kujificha ficha,na ndio maana nataka kama vipi tutengeneze busta la pesa >>>>DIAMOND.
 
Naona pembe zinazidi kutoka,na dimpoz kaomba interview huko inaonekana umevuta kamba kwako sana km mkali kushinda wao tuliza jicho unataka kushindana ya nn ??mm team netanyahu napita tu waafrika oyeeeee!!!
 
Nilishawahi kuwaomba tufanye shoo ya nani zaidi,wakakataa hata January makamba nilimuomba uzamini na hata Babu Tale shahidi >>>DIAMOND.
Mimi nataka kama wanataka busta kutoka kwangu basi waje live sio kujificha ficha,na ndio maana nataka kama vipi tutengeneze busta la pesa >>>>DIAMOND.
shoo hiyo ingewapa mpunga mrefu sana.
 
ommy aache kumuonea wivu Mavoko, amemuogopa na kwenda kwa Diamond hata kama ana wivu nae

Ni inaonyesha inamuuma sana maendeleo ya Mavoko kwa kusubiria hadi alipotaka kutoa winbo wake na siku aliyoutoa tena baada ya kutolewa.
 
diamondplatnumz-1479933736066.jpg


diamondplatnumz-1479933743964.jpg


Picha za tarehe 23 November 2016
 
Back
Top Bottom