FULL LIST: Rais Ruto amefanya uteuzi wa Baraza la Mawaziri, IGP na DCI wajiuzulu

FULL LIST: Rais Ruto amefanya uteuzi wa Baraza la Mawaziri, IGP na DCI wajiuzulu

Wenzetu ndio maana wapo mbele mnooooo
Yaani hadi Vyama vya ushirika wameviwekea wizara yake kabisa,huku kwetu blablah t ,na kubana sauti eti serikali ya awamu fulani,inasiida nn,ujinga mtupu
 
Leo Sept. 27, 2022 Rais William Ruto amefanya kikao cha kwanza na Baraza la Mawaziri wa Serikali iliyopita na kisha kufanya uteuzi wa Baraza lake jipya linalojumuisha Mawaziri 21 ambao watasimamia Wizara mbalimbali.

Ruto amemteua aliyekuwa Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi kuwa Mwanasheria Mkuu na Musalia Mudavadi kuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri

Pia, Rais Ruto amesema Mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi wa Jinai George Kinoti amejiuzulu na hivyo ameagiza Jeshi la Polisi kutangaza nafasi hiyo. Aidha, Rais William Ruto amemteua Japheth Koome Nchebere kuwa Inspekta Jenerali wa Polisi baada ya Hillary Mutyambai kutangaza kujiuzulu.

Katiba ya Kenya inataka Mawaziri kuomba nafasi hizo kupitia Tume ya Utumishi wa Umma (PSC) na kisha PSC itafanya usaili na kuwasilisha majina kwa Rais ambaye atateua anaowataka na kupeleka orodha hiyo Bungeni ili kuidhinishwa.

Hapa ni Orodha yote ya Mawaziri walioteuliwa.

1. Wizara ya Mambo ya Ndani - Prof Abraham Kindiki

2. Wizara ya Fedha - Prof. Njuguna Ndung'u

3. Jinsia na Utumishi wa Umma - Aisha Jumwa

4. Wizara ya Ulinzi - Aden Duale

5. Wizara ya Maji - Alice Wahome

6. Masuala ya Kigeni na Diaspora - Alfred Mutua

7. Biashara, Uwekezaji na Viwanda - Moses Kuria

8. Jumuiya ya Afrika Mashariki na Maendeleo ya Kikanda - Rebecca Miano

9. Barabara, Uchukuzi na Kazi za Umma - Kipchumba Murkomen

10. Mazingira na Misitu - Soipan Tuya

11. Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Miji - Zachariah Mwangi Njeru

12. Utalii, Wanyamapori na Turathi - Peninah Malonza

13. Kilimo na Maendeleo ya Mifugo - Mithika Linturi

14. Wizara ya Afya - Susan Nakumicha Wafula

15. Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Kidijitali - Eliud Owalo

16. Wizara ya Elimu - Ezekiel Machogu

17. Nishati na Petroli - Davis Chirchir

18. Wizara ya Vijana Michezo na Sanaa - Ababu Namwamba

19. Vyama vya ushirika na maendeleo ya MSME - Simon Chelugui

20. Wizara ya Madini, Uchumi na Masuala ya Bahari - Salim Mvurya

21. Wizara ya Kazi na Masuala ya Jamii - Florence Bore

Teuzi Nyingine:

1. Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri (Waziri Mkuu) - Musalia Mudavadi

2. Katibu wa Baraza la Mawaziri - Mercy Wanjau

3. Mwanasheria Mkuu - Justin Muturi

4. Mshauri wa Shirika la Haki za Wanawake - Harriet Chiggai

5. Mshauri wa Usalama wa Taifa - Monica Juma

===================

President William Ruto has named his cabinet on Tuesday, with ANC leader Musalia Mudavadi being appointed Prime Cabinet Secretary. Mr Mudavadi will be the most senior officer after the President and his DP Rigathi Gachagua.

Prof Kithure Kindiki has been appointed Interior Cabinet Secretary while Treasury will be headed by former CBK governor Prof Njuguna Ndung'u.

The Head of State also picked Aden Duale as Defence CS, Aisha Jumwa to Public Service and former Machakos governor Dr Alfred Mutua to head Foreign and Diaspora Affairs ministry.

The Lands docket will be headed by Zachariah Mwangi Njeru, Agriculture and Livestock Development by Mithika Linturi and Health by Susan Nakhumicha Wafula.

Dr Ruto named Alice Wahome as Water and Sanitation CS, Moses Kuria as Trade CS while the East African Community Ministry will be headed by Rebecca Miano.

The Roads, Transport and Public Works ministry will be headed by Kipchumba Murkomen while Soipan Tuya has been appointed CS of the Environment and Forestry ministry.

Ms Peninah Malonza will replace Najib Balala as Tourism CS, while Eliud Owalo has been appointed to the Communications docket.

Mr Ezekiel Machogu will replace George Magoha as Education CS as long-term Ruto ally Davis Chirchir heads to the Energy Ministry.

The Youth Affairs ministry will be headed by Mr Ababu Namwamba, Cooperatives by Simon Chelugui and Mining by Salim Mvurya. The Labour ministry will be headed by Ms Florence Bore.

President Ruto promised that other cabinet appointments will follow soon.

Other key appointments

Outgoing Cabinet Secretary for Energy and Petroleum of Kenya, Ms Monica Juma, will be retained by Dr Ruto's government as National security advisor.

Others given plum government positions include Justin Muturi who will be Kenya's next Attorney General while Mercy Wanjau has been appointed to serve as secretary to the cabinet.

NATION AFRICA
Kwamba kuna Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri na Katibu wa Baraza la Mawaziri? 😁😁😁😁
 
Ruto namkubali sana. Naamini ataiendesha kenya vizuri sana na kwa mafanikio makubwa. Mungu amsimamie
Amina.
Unaifahamu movie ya the last king of scotland?
Kuna sehemu wakati Eid amin anahutubia umati wa watu wanashangilia kale kamzungu kakamwambia mke wa mchungaji kuwa jamaa anaonekana ana machungu na nchi na raia wanamkubali sana.
Kale kamwanamke kakamjibu, ndivyo siku zote ikavyokuwa afrika anapoingia kiongozi mpya, ila mbeleni mambo uwa tofauti.
 
Yaani baraza limejaa wote waliomsupport kushinda uchaguzi na watu wake wa karibu. uhuru Kenyatta wakati anaingia madarakani aliweka watu wote wapya for various professional na sio wanasiasa na ilikuwa rahisi kuwabana coz hakuwa na interest zao....Sasa wengi Rutto aliowaweka wengi ni wapigaji...tutegemee wataiba Sana na waoneana aibu kufukuzana. Pili wengi hapo ni wateule magavana na maseneta na wabunge.so itabidi uchaguzi mdogo ufanyike baadhi ya maeneo ,ni gharama kubwa kwa serikali uchaguzi wa marudio...Imagine mtu mpigaji wa tender kama Dualle anapewa wizara ya ulinzi.,.unadhani akiiba Rutto atachukua hatua gani?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom