Wakuu
Nimepitia ripoti ya PAC uk 63 inasomeka hivi "Tarehe 6/2/2014 Pesa Cash Shs3.3Bilis zilichukuliwa kutoka Mkombozi Benk na Siku hiyo hiyo Shs 73.3Billions Zilichukuliwa kutoka Stan Bic Benk.
Ni jambo la hatari kwa taasisi za usala kushindwa kuzuia wizi huu hata kama walikuwa wanachukua pesa zao lakini pia hata sheria za Kibenk haziruhusu jambo hili.
Swali langu kwa wadau wapenda haki , ni kwa nini PAC wametaja majina kadha ya watu waliochukua fedha kutoka Benk ya Mkombozi ambako pesa kitogo zimetoka 3.3bls lakini hawajataja hata jina moja kutoka StanBic benk ambapo zimetoka 73.3ls .
Kuna nini huko?
Je Zitto kahongwa??
Naomba mwenye majina hayo aweke hapa kwa maslahi ya umma , Sisi tujadili kwa pamoja huu ndo uzalendo!!