Mheshimiwa Spika,
Kutokana na mahojiano kati ya Kamati na
Kamishina Mkuu wa TRA ilibainika kwamba Kampuni ya Piper Links
haijulikani sio tu British Virgin Islands bali hata nchi nyingine.
20
Kamati haielewi ni jinsi gani taasisi kubwa kama Benki Kuu ya
Tanzania, Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Fedha, Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali na nyingine zilizohusika katika suala
hili, na ambazo tunaamini zimesheheni Watendaji wenye weledi,
zimewezaje kushindwa kufanya uchunguzi wa kina (
due diligence)
ambao ungewezesha utata huu kugundulika na kuepuka
kudanganywa na PAP.