Freeman Mbowe, Wakili Marando, CHADEMA, UKAWA...
Baada ya majaribio ya mara kadhaa ya kutaka kuanzisha mijadala ya kumhusisha Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, watu wale wale jana na leo wameendelea kujaribu kutuondoa kwenye mtitiriko wa tuhuma za ufisadi zinazoikabili Serikali ya CCM zinazozidi kukisukumia chama hicho tawala kwenye kingo za maporomoko makubwa ya kisiasa nchini.
Mfano;
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-aitisha-kikao-cha-siri-sakata-la-escrow.html
Kama hiyo haitoshi, imeanzishwa mijadala ya kutaka kuihusisha CHADEMA kwa hoja ya kutunga kwamba Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama, Wakili Msomi Mabere Marando ameshiriki kufungua kesi ili kuzuia Bunge lisijadili Ripoti ya CAG kuhusu matokeo ya ukaguzi maalum kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa BoT.
Hawakuishia hapo. Wakaenda mbali na kuhusisha UKAWA kuwa umeenda mahakamani kuweka zuio la Bunge kujadili ripoti ilitotajwa hapo juu.
Ufafanuzi;
Kujaribu kumhusisha au kumtuhumu Mwenyekiti na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mbowe kuhusika katika kashfa ya ufisadi wa Akaunti ya Escrow ni upuuzi wa kupuuzwa. Kwa sababu mbali ya kuwa ni propaganda nyeusi za kuinusuru CCM kwa kutumia falsafa ya tuchafuke wengi, ili kwaondolea uhalali viongozi wa UKAWA wanaoongoza na kusimamia mapambano haya ya kuiondoa CCM, pia ni matumizi mabaya ya uwezo wa kujua kusoma na kuandika.
Kwanza misimamo ya Mwenyekiti na KUB Mbowe kwa masuala ya ufisadi iko dhahiri wala haihitaji mtu kuinama uvunguni kuipata. Akiwa ni mwenyekiti wa chama (akiwepo jukwaani) kilichosimama mchana hadharani kwenye mkutano wa hadhara na kutaja Orodha ya Aibu ya Mafisadi 11 nchini, akiwemo Rais aliyeko madarakani, Rais Mstaafu, mawaziri waandamizi kwenye serikali ya CCM na makada waandamizi wa chama hicho na watendaji waandamizi serikalini.
Kupitia kauli zake na maamuzi ya vikao anavyovisimamia, iwe katika chama, KUB na sasa UKAWA, amekuwa consistent juu ya jambo lolote (ikiwemo ufisadi ambalo ni zao la mfumo na utawala mbovu) lile linalozidi kudhihirisha kuwa CCM inapaswa kuondoka madarakani la sivyo taifa hili litaangamia.
Kama ni kwenye suala mahsusi la kashfa ya ufisadi wa Escrow Account; Mwenyekiti Mbowe kwa nafasi yake ya KUB, hivi karibuni akiwa mkoani Kigoma alikwenda hatua kadhaa mbele na kumtaka Rais Kikwete kumfukuza kazi Waziri Mkuu na aunde baraza jipya la mawaziri walau limsaidie katika hali yake ya kuchoka (alisema akiwa China), ili taifa lifike uchaguzi mkuu na wananchi wafanye maamuzi. La sivyo Kambi ya Upinzani Bungeni itaanza maandalizi ya kuandaa hoja ya kutokuwa na Rais yeye mwenyewe.
Kwenye mikutano yake ya ziara iliyopewa jina la Operesheni Delete CCM na wananchi wa Kijiji cha Nata, mbali ya kufichua ufisadi mwingine ambao unaelekea kuvunja rekodi, unaohusisha
trilioni 1.2 zilizopigwa kwenye ujenzi wa bomba la gesi, aliwataja wahusika ambao hadi sasa hakuna mtu amediriki kuwasema kuwa ni sehemu ya watuhumiwa, ikiwemo royal family.
Kwa suala la Wakili Mabere Nyaucho Marando, nadhani ni suala la uelewa tu. Wakili huyu maarufu na mpiganaji mzoefu wa siku nyingi katika mapambano ya kisiasa, kisheria wana ushirika na Wakili Mnyele kwenye Kampuni maarufu ya uwakili, Marando, Mnyele &Co Advotates.
Ukweli wa ushirika huo hauondoi ukweli mwingine wa kisiasa, kijamii na kisheria unaoweza kuwahusu watu hao wawili kila mtu kivyake kabisa. Wakili Mnyele ni mwanaCCM kwa maana ya political affiliation.
Amewahi kugombea uongozi; Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) akashindwa. Ni factual pia kuwa Mnyele ni swahiba au ni mtu anayefahamiana kwa karibu na Waziri Mkuu. Yaweza kuwa kikazi; kisiasa, kisheria au kijamii kwa kuwa wanatokea sehemu moja.
Ni Waziri Mkuu huyo huyo ambao mbali ya hivi karibuni kutajwa kuwa mmoja wa watuhumiwa katika kashfa hiyo, lakini pia naye amejipambanua kuwa kiongozi ambaye asingependa suala la Escrow lijadiliwe ndani ya bunge kwa sababu liko mahakamani.
Lakini pia kwa taratibu za kisheria, si jambo la ajabu kuwa Mnyele anaweza kabisa kuchukua kesi na kwenda kuisimamia kama yeye kwa kushirikiana na watu wengine bila Marando ambaye ni mshirika wake kwenye kampuni nyingine ya uwakili kujua. Ipo mifano mingi sana katika hoja hii.
Mbali ya facts hizo, nimezungumza na Wakili Marando ambaye amesema wazi kuwa nyaraka ya kesi hizo hazikuandaliwa ofisini kwao. Haziko kwenye kompyuta yeyote pale ofisini.
Wakili Marando hakuwepo mahakamani kwa keshi hiyo jana. Wala hatakuwepo. Mawakili walioomba order hiyo ni wanachama wa CCM.
Wakili Marando ni mwanachama wa forums mbalimbali katika mitandao ya kijamii. Ingawa hapendi ku-comments kupitia huko. Ninajua, mathalani anayo kawaida ya kupitia JF asubuhi na jioni. Kujisomea, kupata updates, kupata mawazo na fikra mbalimbali juu ya mijadala ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Kuhusu UKAWA, CHADEMA tutaeleza kw akifupi sana;
Ni jambo la ajabu kweli kweli kujaribu kuwadanganya watu eti kwamba walioko upinzani ghafla wamekuwa na nguvu za watawala kiasi cha kwenda kutumia vibaya uhuru wa mahakama kuzuia jambo ambalo linakwenda kuiangusha Serikali ya CCM kwa mara nyingine; jambo ambalo linazidi kuifukua CCM namna kilivyo na nasaba ya damu na ufisadi unaoliangamiza taifa.
Yeyote anayejaribu kueneza uongo huo maana yake ni kwamba hajawahi kumsikia Prof. Lipumba, Freeman Mbowe, James Mbatia, Dk. Slaa (aliyetaka International Auditing kama wakati wa EPA ili ukweli wote ufumuliwe) na wabunge wengine wanavyosimama kidete kuhakikisha si Escrow Account pekee, bali kashfa nzima ya IPTL (kuanzia 1990s) inafumuliwa; suala ambalo likifanyika leo hakuna mtu ndani ya CCM atakayebaki bila kuchutama. Walioko madarakani na waliostaafu! Maana watakuwa wamevuliwa nguo!
Makene