Full Text: Ripoti ya PAC Bungeni kuhusu Tegeta Escrow Account

Full Text: Ripoti ya PAC Bungeni kuhusu Tegeta Escrow Account

Nimepita mtaaani huku mkoani Rukwa kila kona watu wapo katika redio wafanyabiashara wadododo maarufu kama machinga wamepanga bidhaa zao huku kila mmoja akifuatilia hotuba za zitto kupitia Radio
 
Kama kawaida lazima kuwe na kampuni hewa na kukwepa kodi zinye thamani ya billion 6
 
Msaada please natetemeka while listening to PAC report sijui y
 
Leo nimekaa hapa sebuleni na familia nzima. Wife, mwanagu wa miaka mi 4 shemeji, dada wa nyumbani, house boy, kijana wa jirani na kuna jamaa wawili siwajui vizuri lakini poa tu tutaulizana baada ya repoti hii bungeni!
Kama mnacheki mpira vile,kweli watu wanauchungu na salio...
 

[h=2]Ukawa wataka fedha zilizoporwa zirejeshwe
[/h]
Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), umeendelea kuibana serikali kurudisha rasilimali na fedha za umma zilizoporwa zirejeshwe nchini.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambacho ni miongoni mwa vyama vinavyounda Ukawa vya CUF, NCCR –Mageuzi na NLD, kimetangaza kuanza maandalizi ya oparesheni ya kudai kurejeshwa kwa fedha hizo itakayofanyika nchi nzima.

Kimesema fedha ambazo zimekuwa zikiporwa katika kashfa mbalimbali za ufisadi, serikali imeshindwa kuwachukulia hatua stahiki wahusika wake kwa kuwaficha au kuishia kujiuzulu nafasi zao.

Akizungumza katika mikutano ya ziara iliyopewa jina la ‘Operesheni Delete CCM' katika vijiji vya Hayderer na Luxmanda; wilayani Mbulu na Babati Mjini katika Uwanja wa Kwaraa, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zanzibar, Salum Mwalimu aliwataka Watanzania wa mijini na vijijini kujiandaa kwa operesehni hiyo aliyosisitiza itakuwa maalum kuwakomboa wananchi kuondokana na minyororo ya ufisadi unaosababisha wawe maskini.

Alisema operesheni hiyo ni maalum kwa ajili ya wananchi kudai kurejeshwa kwa fedha zao zinazoporwa katika ufisadi wa kitaasisi, katika maeneo nyeti ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), wizarani na katika miradi mbalimbali, ambayo italenga kuuamsha umma kutovumilia wizi wa rasilimali zao, huku kukiwa hakuna hatua stahiki zinazochukuliwa.

Aliongeza kuwa operesheni hiyo haitalenga fedha za kashfa za hivi karibuni pekee, bali kashfa mbalimbali za wizi wa fedha za umma.

Alisema haitoshi kwa viongozi kukiri kuhusika au kulazimishwa kukubali ama kutolewa kafara ili kuiokoa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kila kunapotokea kashfa kubwa ya wizi wa fedha zinazowanufaisha watu wachache huku Watanzania wengi wanakufa kwa njaa, bali nguvu ya umma inapaswa kutumika kuwaokoa Watanzania juu ya tatizo hilo.

"Naomba kutumia fursa hii ya mikutano yangu ya vijijini, kutoa kauli ya kuwataka Watanzania, wananchi wenye uchungu na nchi yao, wenye uzalendo wa dhati kwa nchi yao, kuwa tayari kwa operesheni maalum ambayo italenga kuzidai fedha zetu ambazo tumekuwa tukiibiwa katika kashfa mbalimbali za ufisadi, ikiwamo hii ya Escrow na IPTL na wizi mwingine tangu ilipoanza miaka ya 90," alisema na kuongeza:

"Sote tunajua, chini ya utawala wa serikali ya CCM taifa limekuwa katika misiba mingi, kama anavyosema Mwenyekiti wa Chadema Mbowe, kwamba taifa lina misiba mingi, hakuna aliyepona, wakulima wana kilio, wafugaji, wavuvi , wamachinga, mama ntilie, wafanyabiashara wakubwa, wafanyakazi, msiba kila mahali kwa kila kundi."

"Moja ya misiba hiyo ambayo sasa hatuna budi kuufikisha mwisho ni msiba wa ufisadi. Taifa liko kwenye msiba wa ufisadi ambao hatujui CCM watatuondolea lini.

Tunawataka Watanzania kujiandaa kuzidai fedha zao," alisema. Kadhalika, Mwalimu alisema kuwa CCM inajua fedha zinazoibiwa serikalini zinakwenda wapi kwa kuwa mojawapo ya njia zake za kutafuta fedha za kampeni za chama hicho ni kupitia kashfa za ufisadi, na kutolea mfano kashfa ya wizi wa fedha za EPA zilizoporwa kabla ya kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.

Viongozi wengine wa Ukawa waliozungumzia kuandaa maandamano ya kupinga wizi wa fedha za Escrow ni Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba, ambaye juzi alisema wataandamana nchi nzima ili wahusika wawajibishwe.


SOURCE: NIPASHE
 
Back
Top Bottom