Full Text: Ripoti ya PAC Bungeni kuhusu Tegeta Escrow Account

Full Text: Ripoti ya PAC Bungeni kuhusu Tegeta Escrow Account

Kwa mujibu wa taarifa ya kamati ya PAC inayoendelea kuwasilishwa bungeni jioni hii,mojawapo wa watu waliotajwa kuingiziwa fedha za escrow ni pamoja na Askofu msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba Methodius Kilaini na Askofu msaidizi Jimbo Katoliki Dar-es-salaam Eusebius Nzigilwa.kwa hakika hii ni kashfa kubwa kwa taasisi kubwa kama Kanisa Katoliki..je wadau mnalionaje hili?
 
Nimepita mahali watu wametulia wanafatilia bunge.... wengine kwenye vigenge na radio wakisikiliza

uku kwetu leo kuanzia vibanda umiza, dereva wa bodaboda, kwakuchezea bao na drafti na hata vijiwe vya mafundi nguo-viatu-baiskeli kama hawana Tv basi wana redio wapo wanawasikiza mjengoni
 
Kama mkatoliki, nimefedheheshwa na suala la baba askofu KILAINI kuhusishwa nayo! Hii kashfa kwa kanisa hapa Tanzania na Dunia kwa ujumla, Kardinali Pengo tupe mmaelekezo wa kwanza kwa nini Askofu ajihusishe na taratibu hizo za kifisadi! Na kwa nini benki ya kanisa ya mkombozi ihusishwe kashfa na transaction ya pesa chafu.
 
Kauli ya Deo kumnukuu Kambarage ni kama anamgusa na mkulu vile....ila ndio hagusiki kwa kuwa kanchi ketu katatikisika

Kweli. Hao waliochini yake wote wakiadhibiwa itatosha kwa leo. Rais si mchezo kufanya kama burkina faso yataka kamsaada ka wajeda ambao nao hawatabiriki
 
Habari za Escrow zimeshaisha, Watanzania kesho watakuwa wamesahau
 
Benki ya Mkombozi inaonesha majina isipokuwa ile ya Benki ya Stanbic haina majina zaidi ya nambari za akaunti pekee...

Ilipaswa walau majina yawe wazi hata kwa wabunge pekee maana hakuna sababu ya kuwatuhumu kwa kuwaficha hao wakwapuaji waliopewa fedha na JR...


Mkuu kuna yale matransaction ambayo hayaonyeshi beneficiaries, hapo ndipo TAKUKURU wanapoingia kiuchunguzi na kufuatilia ili kujua hizo pesa zilienda kwa watu gani. Watatambulika tu.

Kamati ya bunge isingeweza kufika huko ama CAG naye asingefika huko. Madaraka hayo yapo kwa TAKUKURU
 
Back
Top Bottom