Full Time: AL Hilal 0-1 Young Africans | CAF Champions League | Stade de la Capitale | 12/1/2025

Full Time: AL Hilal 0-1 Young Africans | CAF Champions League | Stade de la Capitale | 12/1/2025

Joseverest

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2013
Posts
52,812
Reaction score
71,392
Karibuni katika Matchday 5 Kati ya Al Hilal Omdurman' na Yanga katika dimba la Stade de la Capitale lililoko mjini Nouakchott, Mauritania, mechi hii itachezwa saa 4 usiku kwa saa za Africa Mashariki (1900Hours GMT/UTC)

Nini kitatokea katika mechi hii ambayo Yanga anahitaji matokeo ya ushindi zaidi ili ajiweke mguu sawa kutinga Robo fainali ilihali Al Hilal wanahitaji sare kufuzu hatua inayofuata na kuongoza kundi?

Kuwa nami mwanzo, kati hadi mwisho wa mchezo huu..

#TotalEnergiesCAFCL

View attachment 3200059View attachment 3200061

--------------------------------------------
Updates 2200 Hours

0'+ Mpira umeanza hapa katika dimba hili la Stade de Capitale kwa Yanga kuanzisha Boli

7' Gooooooooaaal, Stephane Aziz Ki anawatanguliza Yanga hapa kwa shuti kali lililomshinda Kipa Issa Fofana

15' Al Hilal wnashambulia lango la Yanga lakini Khalid Aucho anakata umeme ule na kuwaweka Yanga salama

22' Yanga wanapata Faulo hapa kuelekea Al Hilal, Aziz Ki anapiga kwa Mudathir anaaiingiza ndani lakini inatolewa..Baka pia anamdondosha mchezaji wa Hilal kwa hiyo inakuwa freekick

25' Jean claude Girumugisha anashambulia kwenda Yanga lakini inaokolewa inakuwa kona...kona inapigwa inaokolewa hapa

32' Yanga wanapata kona, inapigwa na Pacome lakini wachezaji wawili wa Hilal wanagongana vichwa na refa anasimamisha mpira ili watibiwe

34' Al Hilal wanapata kona inapigwa ila Guessoma Fofana anapiga kichwa kikubwa inaenda nje..Goal kick

38' Aime Tendeng wa Hila anawekwa chini, wanapata faulo, inaanzishwa haraka haraka lakini Yanga wanainasa fasta na kuondoa hatari

42' Al Hilal wanafanya counter attack ya hatari kwenda Yanga lakini Guessoma Fofana anafanya faulo inakuwa free kick

44' Aziz Ki anakosa goli hapa baada ya Issa Fofana kuugusa mpira kwenda nje...Daah chupuchupu

Dakika 2 za nyongeza kwenda Half time

2247 Hours Half time, Al Hilal 0 Yanga 1

2305 Hours Kipindi cha pili kimeanza kwa Al Hilal kuanzisha mpira

49' Dube anashambulia hapa, Adama Coulibali anautoa nje inakuwa ni kona..inapigwa lakini Fofana Issa anaokoa

52' Pacome na Aziz Ki wanaonana vizuri kushambulia lango..wanampa Dube, Dube anapiga mpira unakataa unatoka nje hapa, shambulizi linakataa

59' Aziz Ki anajaribu shuti kali lakini Kipa Fofana analificha kihodari

65' Dube anamuangusha mchezaji wa Al Hilal baada ya shambulizi kali, inakuwa faulo..inapigwa kuuuubwa inakwenda nje inakuwa Freekick

70' Sub kwa Al Hilal

Yasir Mozamil ndani
Abdelrahamn Mohd . Nje

Coulibali nje
Pokou ndani

73' Steven Ebuela anapiga faulo kwenda Yanga, inaokolewa.. Hilal wanaupata Tena ila shuti la Jean Claude linadakwa na Diarra Djigui

78' Sub kwa Hilal
ndani
Abdulrouf Omer
El din

Nje
Alhadj Kane
Tendeng

82' Aucho wa Yanga yupo chini baada ya kugongana mguu na mchezaji wa Hilal na inaonesha kutakuwa na Mabadiliko kama akiridhia

87' Sub kwa Yanga

Musonda anaingia ndani

Ki Aziz anatoka nje

Wakati huo Djigui Diara yupo chini anatibiwa baada ya kuangushwa

90' Dakika 5 kumaliza mchezo huu wa leo

91' Sub kwa Yanga

Duke Abuya ndani

Mudathir Yahya nje

93' Sub kwa Yanga
Chama ndani
Pacome nje

Boka anarusha mpira ule kwenda Hilal ila unaokolewa

94' Chama anaangushwa chini alipokuwa akishambulia, wanaanza faulo harakaharaka..Mzize anaupata ila kipyenga kinaliaaa

95' FULL TIME MPIRA UMEISHA...
AL HILAL 0 YANGA 1
 
Hatimae mpo nafasi ya pili, hongera kwa aliyegundua calculator
IMG_4950.jpeg
 
So leo Pacome yupo ulingoni
 
Karibuni katika Matchday 5 Kati ya Al Hilal Omdurman' na Yanga katika dimba la Stade de la Capitale lililoko mjini Nouakchott, Mauritania, mechi hii itachezwa saa 4 usiku kwa saa za Africa Mashariki

Nini kitatokea katika mechi hii ambayo Yanga anahitaji matokeo ya ushindi zaidi ili ajiweke mguu sawa kutinga Robo fainali ilihali Al Hilal wanahitaji sare kufuzu hatua inayofuata na kuongoza kundi?

Kuwa nami mwanzo, kati hadi mwisho wa mchezo huu..

#TotalEnergiesCAFCL
Yanga atashinda kwa goli nne (4) kwa zero (0).
 
Back
Top Bottom