Goli zuri kabisa. Mpira una kanuni moja tu, ukifanya makosa utaadhibiwa, wachezaji wa Azam wa mbele walifanya makosa halafu wakawa wanatembea. Yanga ni timu inayoweza sana kutumia makosa. Mpira hautaki uvivu ndio maana huwezi kucheza kama umri umeenda.