Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Mchezo wa Ngao ya Jamii kutafuta mshindi wa tatu mchezo unachezwa uwanja wa Benjamin Mkapa kati ya Coastal Union dhidi ya Simba SC.
Dakika 2, Mpira umeanza kwa kasi kubwa sana.
Dakika 5, Simba wanaumiliki mpira sana na kufanya mashambulizi kwenye lango la Coastal.
Dakika 8, Mutala anakosa goli akiwa katika nafasi nzuri sana .
Dakika ya 11, gooooool ,Kalabaka anawapa uongozi Simba SC
Dakika 15, Simba bado wapo kwenye kilele cha kumiliiki mpira.
Dakika 17, Masoud Kalabaka anapiga shuti kali sana ila mpira unapenda kutoka nje.
Dakika 22, Simba wanaendelea na mashambulizi makali sana kwenye lango la Coastal
Dakika 24, wanafanya shambulizi kali kupitia Lucas Kikoti ila wanashindwa kuitumia nafasi hiyo ili kuzawazisha goli.
Dakika 27, Steven Kukwala anakosa nafasi ya wazi kabisa hapa oh.
Dakika 31, Hadi sasa Simba wameendelea kufanya vyema mbele ya Coastal
Dakika 32, John Makwata anaruka kichwa safi sana lakini mlinda mlango wa Simba anawaweka Simba salama baada ya kudaka mpira huo.
Dakika 38, Mukwala anakosa nafasi ya wazi tena yeye na kipa.
Dakika 40, Mukwala anakosa tena nafasi hii sasa ni balaa kutoka kwake.
Zimeongezwa dakika 3 ili kutamatika dakika 45 za kipindi cha kwanza.
Dakika 45 za kipindi cha kwanza zimetamatika na Simba anatoka akiwa kifua mbele Coastal Union 0- 1 Simba SC.
Kipindi cha pili kimeanza tusubiri dakika 90 zitakuwaje je ni Simba SC au ni Coast Union ataibuka mshindi wa 3.
Dakika 46, Coastal wanafanya mabadiliko Gwalala anaingia anatoka Baraki.
Dakika 49, Charles Ahoua anafanya shambulizi kali sana ila golikipa wa Coastal anawaokoa wenzie
Dakika 54, Coastal wamepata faulo freekik hiyo inapigwa na Kikoti lakini mpira umegonga mwamba.
Dakika 55 Simba wanafanya mabadiliko Mashaka anaingia anatoka Mukwale lakini Ngoma anaingia Mavambo anatoka.
Dakika 63, Coastal Union wanafanya mabadiliko Lucas Kikoti anakwenda nje Cosmas anachukua nafasi yake.
Simba wanafanya mabadiliko Shabalala anatoka nafasi yake inachukuliwa na Numa.
Dakika 68, Kelvin Kijili anakosa nafasi nzuri sana hapa ya kuwapatia timu yake Simba SC goli la pili
Dakika 78, Coastal wanakosa nafasi ya wazi kabisa ya kusawazisha
Dakika 79, Ngoma anapata kadi ya njano.
Dakika 80, Simba wanafanya mabadiliko, Joshua Mutale anatoka nafasi yake inachukuliwa na Kibu Denis.
Dakika 83, Ngoma anapata kadi nyekundu baada ya kumfanyia faulo mchezaji wa Coastal Union.
Dakika 85, Mashaka anapata kadi ya njano baada ya kufanya faulo kwa mchezaji wa Coastal Union
Dakika 86, Banza anapata kadi ya njano baada ya kumchezea faulo Kijili.
Dakika 89, Gwalala anapata kadi ya njano.
Dakika 4 zimeongezwa kumalizika kwa dakika 90 za mchezo wa leo.
Dakika 90 zimekamilika Simba SC wanaibuka na ushindi goli 1 kwa 0 dhidi ya Wagosi wa kaya Coastal Union na Kuwa mshindi wa nafasi ya Tatu ya Ngao ya Jamii.