Full Time: Fountain Gates FC 1-1 Simba SC | NBC Premier League | Kwaraa Stadium, Babati | 06-02-2025

Full Time: Fountain Gates FC 1-1 Simba SC | NBC Premier League | Kwaraa Stadium, Babati | 06-02-2025

Attachments

  • downloadfile-5.jpg
    downloadfile-5.jpg
    64.4 KB · Views: 1
Kikosi cha Simba jioni ya leo kitashuka uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Manyara kumenyana na Fountain Gate katika mchezo wa ligi kuu ya NBC

Simba iliwasili Manyara mapema jana na jioni kikosi kikapata nafasi ya kufanya mazoezi ya mwisho katika dimba hilo

Soma, Pia: Kocha wa Fountain Gate: Mimi ni shabiki wa Simba, asema mechi ya leo ni kuonana kwa Simba na Simba

Ni mechi nyingine kwa Simba kuzisaka alama zote tatu ili kurejea katika nafasi yao, juu ya msimamo

1738844922007.png
Lakini ni wazi haitakuwa mechi nyepesi, Fountan Gate, wamepata muda wa kujipanga zaidi huku wakifanya maboresho kadhaa katika dirisha dogo ikiwa ni pamoja na kuleta kocha mpya

Timu hizo zilipokutana katika duru ya kwanza uwanja wa KMC Complex, Simba iliibuka na ushindi wa mabao 4-0

Katika duru hii ya pili ya lala salama, kila alama tatu zina thamani kubwa, kwa Simba hakuna nafasi ya kudondosha alama katika mawindo ya ubingwa msimu huu

Usikose kuitazama mechi hii live kabisa kupitia simu yako download app hapa chini inayoonesha mechi za ligi kuu tz bara na ulaya

VIKOSI VYA TIMU ZOTE


1738844853005.png


1738844798407.png
Mechi imeanza

6' Fountain Gate 0-0 Simba SC
8' Fountain Gate wanakosa goli, huku mechi ikionekana kuwa ni kali kwa pande zote wakishambuliana kwa zamu

10' Fountain Gate 0-0 Simba SC
18' Simba SC wanapata kona ya pili katika mchezo
20' Milango bado ni migumu pande zote
21' Simba SC wanapata kona
32' Noble anatibiwa baada ya kupangua shuti kali la Chasambi lililozalisha kona ambayo Simba wameshindwa kuitumia vizuri
41' Malone anakosa goli baada ya kupiga fyongo kichwa mpira wa adhabu uliochongwa na Ahoua
45' dakika 4 imeongezwa kukamilisha kipindi cha kwanza

HT: Fountain Gate 0-0 Simba SC
 
Km 6 ndogo basi kunywa chai na Chapati 6 halafu tuone
 
Nimemsikiliza kocha WA fountaine geti loh

Sitoshangaa kuona Simba akipiga 7 na kusema amekutana na kitu kizito

Kocha ANASEMA yeye n Simba damu na anaipenda siku nyingi

Niko kwa wakala. Mieeee
 
Kila la kheri timu bora barani Afrika Simba sports club.
Tuko pamoja
 
Back
Top Bottom