Mods nawashauri mngeset standard ya kuanzisha nyuzi za Live Match ziweje, sio kila mtu tu akimbilie kuanzisha thread ambazo hazina nyama za kutosha
Kwa mfano kwa hii thread ilitakiwa:
1. Itoe maelezo mafupi kuhusu profile ya Mashujaa Fc ni kina nani, inamilikiwa na nani, wapo mkoa gani, inashika nafasi ya ngp ktk msimamo wa ligi,, hvyo hvyo kwa Yanga
2. Itoe maelezo kwa ufupi kuhusu status ya game zao atleast tatu za mwisho zilizopita za NBC PL, na point walizokusanya ktk ligi
3. Ielezee head to Head baina ya hizi timu mbili ilikuwaje, angalau kwa kuangazia hata game 3 baina yao
4. Uimara na udhaifu wa baina ya timu hizi mbili pía kwa kuangazia wachezaji/washambuliaji wao wa kuchungwa /hatari
Kwa hayo machache tukifanya hivi itaongeza thamani na mvuto wa thread zinazoanzishwa kuhusiana na hizi live games zinazofunguliwa kila mara kiholela holela tu
Nawasilisha