Mwanadiplomasia Mahiri
JF-Expert Member
- Nov 4, 2019
- 685
- 2,355
Usiku wa leo saa 6:30 timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars itashuka dimbani kuwakabili wenyeji wao Morocco.
Ni mchezo wa aina yake kwani Morocco anaongoza kundi E akiwa na alama 12 huku Taifa Stars ikiwa nafasi ya 3 ikiwa na alama 6.
Je Taifa Stars itaondoka na alama 3 au ni Morocco?
Mchezo utakuwa live kupitia Azam Sports 1HD na DStv 227
================================================
1β Mpira umeanza kwa Taifa Stars kuanzisha mtanange
3β Morocco wanapata kona lakini kipa wa Stars wanaondosha hatari
4β Stars wamekuja na mbinu ya kupoozesha mashambulizi huku muda mwingi wakiwa nyuma ya mpira
5β Morocco wanaliandama lango la Stars kama ugomvi, wanapata kona nyingine
7β Morocco 0-0 Tanzania
9β Golikioa wa Stars yupo chini baada ya kufanyiwa madhambi na mchezaji wa Morocco
10β Stars bado wana uoga wa mechi na wameamua kuwaheshimu wenyeji wao, muda mwingi wapo nyuma ya mpira, bado ni 0-0
11β Ally Salim Katoro anapasha wakati huu kipa namba akigangea na jopo la madaktari wa Stars
13β Kipa amesimama sasa na mbungi inaendelea
15β Morocco 0-0 Tanzania
17β Tanzania bado tunacheza soka la kujihami muda mwingi hii ni hatari kwetu maana tunakaribisha mashambulizi zaidi
19β Shomari Kapombe leo anageuzwa tu kama chapati hapa
20β Kipa wa Stars japo ni mgeni kwenye mechi za kimataifa ila anajiimini vizuri na anacheza krosi kwa utulivu, ni hazina ya baadae
21β Kikosi chote cha Stars kimerudi kukaba huku kikitegemea counter attack kwa Kibu na Msuva
22β Mohamed Hussein anamchezea faulo Diaz nje ya box la Stars
23β Morocco wanaenda kupiga faulo hiyo na mpigaji ni Diaz ila wanakosea na ukuta wa STARS unakaa uzuri
24β Mohamed Hussein anapewa kadi ya njano baada ya kumchezea madhambi Mazroui
25β Morocco wanapiga faulo lakini mabeki wa Stars wanaokoa hatari langoni mwao
25β Morocco 0-0 Tanzania
28β Morocco licha ya kumiliki mpira kwa asilimia kubwa ya mchezo wanashindwa kuifungua beki ya Stars
29β Golikipa wa Stars yupo chini tena akigangwa huku mchezo ukiwa umesimama, kwa mujibu wa sheria za soka, kipa ana dakika 6 za kutibiwa kabla ya kufanyiwa sub uwanjani
30β Mtanange unaendelea kipa amekwashasimama
31β Wachezaji wa Stars muda mwingi wa mchezo wanacheza faulo za hapa na pale
32β Offside kwa Kibu Denis Prosper
33β Mashabiki wa Morocco wameanza kuhanikiza ili timu yao ipate goli
35β Morocco 0-0 Tanzania
37β Msuva anapiga shuti lakini anashindwa kulenga lango
39β Kibu yupo chini amefanyiwa madhambi na wachezaji wa Morocco
40β Morocco 0-0 Tanzania
41β Feitoto anapata nafasi ya wazi lakini mkeaju aliopiga unaenda nje
43β Umiliki wa mpira Morocco 78% na Tanzania ni 22%
45β Zinaongezwa dakika 4 ili kufidia muda uliopotea
45β + 01 Amrabat wa Morocco anapiga shuti lakini linapaa, iankuwa salama kwa Stars
HTβ Morocco 0-0 Tanzania
46β Morocco wanaanza mpira kuashiria kipindi cha pili kimeanza
47β Morocco wameanza kwa kasi na washafika langoni mwa Stars
51β Morocco wanapata goli kupitia beki wao Aguerd anayekipiga Real Sociedad
53β Morocco wanashambulia lango la Stars mfululizo
54β Amrabat anawekwa chini na Feitoto
55β Morocco wanapata penati baada ya Iba Bacca kuunawa mpira ndani ya box
58β Brahm Diaz anaweka goli la pili kwa Morocco kwa mkwaju wa Penati
59β Mlima wa matokeo ushakuwa mkubwa kwa Taifa Stars
60β Morocco 2-0 Tanzania
62β Goli la tatu la Morocco linakataliwa mfungaji ameotea
63β Mchezaji wa Tanzania ambaye walau ameonyesha uwezo leo mpaka sasa ni Fei toto
64β Shuti lililopigwa na Mzize linafakwa kirahisi na Bono
70β Taifa Stars wanafanya sub tatu, Mzize, Mudathir na Mohamed Hussein wanatoka, nafasi zao zinachukuliwa na Yusuph Kagoma, Charles Mβmombwa na Pascal Msindo
72β Taifa Stars wanakosa nafasi baada ya shuti la Kibu kupanguliwa uzuri na golikipa Bono na kushindwa kutumia rebound vizuri
74β Ball Possession Morocco 77% kwa Tanzania 23%
76β Msuva anapaisha shuti lake baada ya kumegewa nafasi nzuri na mwenzake
80β Morocco 2-0 Tanzania
82β Msuva anatoka na nafasi yake kuchukuliwa naa Selemani Mwalimu
85β Morocco 2-0 Tanzania
87β Morocco wanaliandama goli la Stars kama wanatudai vile
88β Mpaka sasa Taifa Stars imepuga shuti moja tu lililolenga lango
90β Kutakuwa na dakika 4 za nyongeza
90+01β Feitoto anapiga shuti lakini anapaisha
90+02β Kibu anatoka nafasi yake anaingia Haji Mnoga
FTβ Morocco 2-0 Tanzania