FULL TIME: NBC PL | Young Africans 6-1 Ken Gold | KMC Complex | 05/02/2025

Kitambi chakufutia tachi

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2019
Posts
1,063
Reaction score
2,566
Ligi NBC kuendelea leo majira ya saa kumi na robo alasiri katika uwanja wa KMC Complex ambapo Yanga watakuwa wenyeji wa Ken Gold.

Yanga wanaingia katika mchezo huu wakiwa katika nafasi ya pili wakiwa na wamecheza michezo 16 wakishinda michezo 14 na kupoteza 2 huku wakifunga magoli 36 na kuruhusu magoli 6 wakiwa wamejikusanyia alama 42.

Ken Gold wanaingia wakiwa katika nafasi ya 16 wakiwa wamecheza michezo 16 wakishinda mchezo 1 sare 3 na wamepoteza michezo 13 huku wakifunga magoli 11 na kufungwa magoli 29 wakiwa na alama 6.

Vikosi vinavyoanza leo.
FB_IMG_1738759467245.jpg

1738757695347.jpg

Muda wowote kipute kitaanza wachezaji wapo uwanjani.

Dk3 Goaaaal Prince Cube anawafungia Wananchi bolo LA kuongoza.

Dk6 Gooaaal Clement Mzize anawafungia wananchi goli LA pili.

Dk ya 27 matokeo back ni 2-0 na Yanga wanacheza mpira wa kuvutia hapa.

Dk39 Pacome anawafungia wananchi goli LA 3.

Goooaaaaaaal Mzize Anafunga goli LA nne.

HT: Young Africans 4 vs 0 Kengold.

Dk 46 Dube anafunga goli la 5 kwa Yanga

Dk 84 Abuya anaifungia Yanga goli la 6

Dk 86 Rashis anaifungia goli Ken Gold
 
Kikosi cha Yanga jioni ya leo kitashuka uwanja wa KMC Complex kuikabili KenGold katika mwendelezo wa ligi kuu ya NBC

Yanga leo itashuka KMC Complex kucheza mechi hiyo ikiwa na benchi jipya la ufundi baada ya Sead Ramovic aliyekuwa Kocha Mkuu kuondoka pamoja na Kocha Msaidizi Mustafa Kodro

Hata hivyo tayari Yanga imemuajiri Kocha Miloud Hamdi aliyeinoa Singida Black Stars kwa siku 36 ambapo atasaidiana na AbdulHamid Moallin ambaye licha ya majukumu yake ya Ukurugenzi wa ufundi, Yanga ilimuongezea majukumu mengine ya kusaidia katika benchi la ufundi

Ni wazi mabadiliko hayo ya benchi la ufundi yaliyofanywa jana hayawezi kuwa na athari kwa Yanga kuelekea mchezo dhidi ya KenGold kwani Ramovic alikamilisha maandalizi yote ya mchezo huo kabla ya kuaga jioni ya jana

Ni mechi ambayo Yanga inahitaji kushinda ili kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi

Usikose kuitazama mechi hii Live kupitia simu yako download app itakayokuwezesha kuitazama mechi hii LIVE BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD APP
 
Back
Top Bottom