Full Time: Simba 0-2 Yanga Taifa 26/9/2015

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Wakuu yamebaki masaa takribani 16 kipenga kipulizwe kuashiria mtanange mkubwa kuanza kati ya Simba na Yanga zote za Dar. Mbali na kuwa ni watani wa jadi timu hizi zina historia kubwa katika mpira wa Tanzania. Mashabiki wana hamasa kubwa wakitegemea mpira na ufundi wa hali ya juu. Kamanda wako ninaahidi kukuletea live updates hapahapa JF kila dakika itakayocheza. Tulia
========

00' Mpira umeanza hapa uwanja wa Taifa

06' Kipa wa Yanga, Mustapha anapiga mpira nje kuashiria kuumia baada ya kudaka mpira wa kona

28' Kiiza anakosa goli baada ya kupewa pasi nzuri na Mustapha kufanikiwa kuutoa

30' Bado milango yote migumu, faulo ya haraka baada ya Awadh wa Simba kuwekwa chini

35' Yanga wanafanya mabadiliko ya wachezaji na Msuva anatoka

39' Hamis Tabwe anaangushwa chini na kugaagaa lakini anaweza kuinuka na kuendelea na mtanange

41' Yanga wanakosa goli baada ya kipa kufanikiwa kuutoa na kuzaa kona ambayo hata hivyo haikuleta mafanikio.

44' :A S soccer:Hamis Tambwe anafanikiwa kuiandikia Yanga bao la kwanza

45+2' Mpira unaenda mapumziko

45' Mpira umerejea baada ya mapumziko

64' Mbuyu Twitte anapewa kadi ya manjano baada ya kucheza ndivyo sivyo

79' :A S soccer:Bao la pili kwa Yanga kupitia kwa Malimi Busungu, Simba 0-2 Yanga

90' Kipa wa Yanga, Mustapha yuko chini na anapewa kadi ya njano kwa kupoteza muda, dakika saba zinaongezwa.

90+8' Mbuyu anapewa kadi ya pili ya manjano na kuwa kadi nyekundu

90+9' Kipenga kinapuliza kuashiria mwisho wa mechi ya leo, Simba 0-2 Yanga.

 
Last edited by a moderator:
Bado kama masaa ka 10 ivi Kiiza Diego ajipigie Yanga yake
 
Yanga wakisikia Simba wanaingia wamelegea wanasema ohh kwani Simba akitufunga anachukua ubingwa ...
 
nitaenda ili nione SIASA,najua haziepukiki kwa wakati huu.......
 
Hatutaki siasa

WALIZIANSHISHA TFF kwa kumwalika Magufuli mara tu alipoteuliwa na chama chake,wakazilea walipomruhusu Makamba (akijua ni miongoni mwa ''mitume'' 32) aliponunua mashabiki mechi ya Taifa Stars...Ni siasa pekee zitawaunganisha Mashabiki wa Simba na Yanga...Amini nakwambia...
 
Tayari Yanga wana mgogoro wa nani akae langoni. Barthez ameumia na Dida alishaapa tangu zamani hatakaa langoni mechi yoyote dhidi ya Simba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…