Full Time: Simba SC 2-1 CS Sfaxien | CAF Confederation Cup | Benjamin Mkapa National Stadium | Disemba 15,2024

Full Time: Simba SC 2-1 CS Sfaxien | CAF Confederation Cup | Benjamin Mkapa National Stadium | Disemba 15,2024

Na ndio kinaweza kuja kutokea second half

Simba watashambulia kizembe jamaa watakuja kuvizia shambulizi moja tu la hatari kamba
Mchezo utaishia hapo hapo
Unapiga ramli ndugu tambitambi
 
Leo ndio leo kwenye kipute hiki cha Kombe la Shirikisho Africa kati ya wenyeji Simba ya Tanzania na wageni Sfaxien ya Tunisia.

Hii ni Match Day 3 kwa timu hizi na mechi zilizopita wote walichezea kichapo ugenini (2-1 na 3-2). Leo kila mmoja anatafuta ushindi kufufua matumaini ya hatua ya makundi.

Mechi hii itapigwa saa 10 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Nini kitatokea katika Dimba la Benjamin Mkapa leo? Kuwa nami mwanzo hadi mwisho wa mchezo huu kupitia JamiiForums.

Azam na DStv pia watarusha mechi hii.
View attachment 3177038

---------------------------------------------
Updates : 1500 Hours Vikosi vya leo
View attachment 3177287View attachment 3177288
________________________________________________

1' Mpira umeanza kwa Simba kuanzisha mpira hapa... wanashambulia lango la Sfaxien lakini Zimbwe anapiga pasi kuuubwa inaenda nje

2' Goooaaaal Sfaxien wanapata goal hapa kupitia Hazem Hassen

06' Simba wanashambulia hapa Kibu Denis anaangushwa... Freekick inapigwa na Jean Ahoua.. Kibu anafungaaaaa goal 1-1

09' Simba wametulia wanafanya shambulizi la Kushtukiza lakini Sfaxien wanaokoa shambulizi hilo

14' Simba wanamiliki mpira kwa Kiasi kikubwa kwa chenga za hapa na pale wanajaribu kuingia lakini mpira unatolewa nje

19' Musa Conte anamdondosha Awesu Awesu na Simba anapata freekick, Jean Ahoua anapiga ndefu ila kipa wa Sfaxien, Dahmen anaidaka

24' Kapombe anapress kuelekea Sfaxien anampasia Ateba lakini control yake inakuwa sio nzuri anadhibitiwa na mabeki wa Sfaxien matokeo bado ni 1-1


29' Kapombe anachezewa faulo hapa inakuwa ni freekick nje kidogo ya 18.. Kibu anapiga inagonga ukuta, Zimbwe anaiwahi lakini anapiga inatoka nje

33' Ateba na Kapombe wanaonana vyema kushambulia Sfaxien, wanakwenda pale inamiminwa Cross lakini Jean Charles Ahoua anakosa umakini anapaisha juu

38' Sfaxien wanatibua jaribio la Simba mpira unakwenda nje, Simba wanatawala Dimba ila Sfaxien wanakuwa makini

43' Sfaxien wanaachia kombora kali hapa kuelekea langoni kwa Simba ila Camara analipangua na Zimbwe anaokoa

45' Zimeongezwa dakika 5 kuelekea Mapumziko, timu zinashambuliana kwa zamu (1-1)

45+5' Afisa mmoja wa Sfaxien anaoneshwa kadi ya njano..
Halftime... Ni mapumziko SSC 1 - CSS 1
Wa lunyasi tunashinda mechi hii misa ya kwanza tu. Utopilo mkae kwa kutulia, nyie jana mlitagishwa!
 
Ndo uhalisia wa team lenu bovu.
Simba sio mbovu ila inaleta utoto kwenye mechi ambazo wapinzani wanaonekana kuwa ni dhaifu.

Angalia game zote ambazo Simba amekutana na timu ngumu jinsi alivyocheza.

Leo hii wachezaji wengi wanacheza kwa kujiamini utadhani wanaongoza bao 3.
 
Ila hii timu ina hitaji kuboreshwa zaidi tunacheza kiunderdog kinoma ,tuna kocha mzuri ila wachezaji wengi average.
 
Walikua wanaboaaaa...yani mpira haueleweki...madhembe kafunga kimoja yuko hoii huyo utopolo sasa nani afunge...mpk dkk za jionii
Tundumwiko alikuwa anaruka ruka tu kama mtu anayetembea kwenye lami wakati wa jua kali.
 
Tatizo mashabiki wa Simba huwa wanafunga magoli wakiwa nje ya uwanja. Na ndiyo maana hata Simba wafunge 4 bado watalaumiwa maana huku nje mashabiki wanakuwa wamefunga bao 7
Mwenzako anazungumza uhalisia, we unaleta ngonjera.
 
Kipindi cha pili kimeanza 1-1

Ateba katoka , Mukwala kaingia
 
Mqtarajio ya mashabiki ni makubwa kuliko uwezo wa timu kudeliver.
 
Tatizo mashabiki wa Simba huwa wanafunga magoli wakiwa nje ya uwanja. Na ndiyo maana hata Simba wafunge 4 bado watalaumiwa maana huku nje mashabiki wanakuwa wamefunga bao 7

😃😄😀
Kwasababu tunaijua uwezo wao ni beyond hicho wanachotuonesha
 
Hawa CS Sfaxien huyu ndio kipa wao chaguo la kwanza ama? Mbona kipa mbovu kiasi hiki
 
Back
Top Bottom