Full Time: Simba SC 2-1 CS Sfaxien | CAF Confederation Cup | Benjamin Mkapa National Stadium | Disemba 15,2024

Full Time: Simba SC 2-1 CS Sfaxien | CAF Confederation Cup | Benjamin Mkapa National Stadium | Disemba 15,2024

Sitegemei mtu kama wewe unaweza kusema huifahamu CS Sfaxien, timu ambayo ni mabingwa wa kihistoria wa hili kombe la Shirikisho kwa kulitwaa mara tatu ikiwa Yanga kwa kufika fainali tu viongozi na mabiki wao wanatamba na medali kila siku
Sawa; Sfaxien ni timu kubwa sana
 
Sitegemei mtu kama wewe unaweza kusema huifahamu CS Sfaxien, timu ambayo ni mabingwa wa kihistoria wa hili kombe la Shirikisho kwa kulitwaa mara tatu ikiwa Yanga kwa kufika fainali tu viongozi na mabiki wao wanatamba na medali kila siku
Kwani wanaujua hata huo mpira?Wanahangaika na ushabiki maandazi.Waishauri timu yao inapumulia mashine.Mechi 3 pointi 1.
 
Kundi la SImba bado nni gumu sana pamoja na kuwa la timu zisizojulikana kama Sfaxien, Constantin na Bravos. Kwenye grupu hilo timu inayojulikana ni Simba tu; hizo nyinine zote ni za uchochoroni. Mpaka sasa wote wana point 6 kasoro Sfaxien mwenye point 0.

View attachment 3177472
sawa,ni maoni yako hayo!Ila ila MC Alger iliyomkamda Yanga 2-0 ni ya 5 kwenye ligi huko Algeria wakati unayoidharau Constantine inaongoza Kigi!
Screenshot_20241210-081139.png
 
Hawa Utopolo ni makenge mpaka yatoke damu ndio yanajua yameumia.Uko wa mwisho kwenye kundi lako.Unapumulia mashine na kipointi kimoja kwenye michezo mitatu bado ngebe nyingi.
 
Wewe unayejua kusoma ulete msimamo tofauti.
Ulete na wa Kundi lenu ili utufundishe kusoma msimamo wa hilo kundi.
Hujui kusoma tebo; kubali unyonge huo usamehewe
 
Leo ndio leo kwenye kipute hiki cha Kombe la Shirikisho Africa kati ya wenyeji Simba ya Tanzania na wageni Sfaxien ya Tunisia.

Hii ni Match Day 3 kwa timu hizi na mechi zilizopita wote walichezea kichapo ugenini (2-1 na 3-2). Leo kila mmoja anatafuta ushindi kufufua matumaini ya hatua ya makundi.

Mechi hii itapigwa saa 10 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Nini kitatokea katika Dimba la Benjamin Mkapa leo? Kuwa nami mwanzo hadi mwisho wa mchezo huu kupitia JamiiForums.

Azam na DStv pia watarusha mechi hii.
View attachment 3177038

---------------------------------------------
Updates : 1500 Hours Vikosi vya leo
View attachment 3177287View attachment 3177288
________________________________________________

1' Mpira umeanza kwa Simba kuanzisha mpira hapa... wanashambulia lango la Sfaxien lakini Zimbwe anapiga pasi kuuubwa inaenda nje

2' Goooaaaal Sfaxien wanapata goal hapa kupitia Hazem Hassen

06' Simba wanashambulia hapa Kibu Denis anaangushwa... Freekick inapigwa na Jean Ahoua.. Kibu anafungaaaaa goal 1-1

09' Simba wametulia wanafanya shambulizi la Kushtukiza lakini Sfaxien wanaokoa shambulizi hilo

14' Simba wanamiliki mpira kwa Kiasi kikubwa kwa chenga za hapa na pale wanajaribu kuingia lakini mpira unatolewa nje

19' Musa Conte anamdondosha Awesu Awesu na Simba anapata freekick, Jean Ahoua anapiga ndefu ila kipa wa Sfaxien, Dahmen anaidaka

24' Kapombe anapress kuelekea Sfaxien anampasia Ateba lakini control yake inakuwa sio nzuri anadhibitiwa na mabeki wa Sfaxien matokeo bado ni 1-1


29' Kapombe anachezewa faulo hapa inakuwa ni freekick nje kidogo ya 18.. Kibu anapiga inagonga ukuta, Zimbwe anaiwahi lakini anapiga inatoka nje

33' Ateba na Kapombe wanaonana vyema kushambulia Sfaxien, wanakwenda pale inamiminwa Cross lakini Jean Charles Ahoua anakosa umakini anapaisha juu

38' Sfaxien wanatibua jaribio la Simba mpira unakwenda nje, Simba wanatawala Dimba ila Sfaxien wanakuwa makini

43' Sfaxien wanaachia kombora kali hapa kuelekea langoni kwa Simba ila Camara analipangua na Zimbwe anaokoa

45' Zimeongezwa dakika 5 kuelekea Mapumziko, timu zinashambuliana kwa zamu (1-1)

45+5' Afisa mmoja wa Sfaxien anaoneshwa kadi ya njano..
Halftime... Ni mapumziko SSC 1 - CSS 1


Updates 1707 Hours

46' Kipindi cha pili kimeanza hapa, Ateba nje.. Mukwala kaingia

50' Kibu Denis anashambulia kwenda Sfaxien, anaingia kwenye 18 anaanguka refa anamwambia nyanyuka, no penalty

57' Kadi ya njano kwa Che Malone baada ya kucheza faulo, free kick inapigwa na sfaxien lakini inatoka nje

62' Haboub anaoneshwa kadi ya njano kwa kumzuia Musa Camara kuanzisha goal kick

64' Sub kwa Simba
Mutale
Chamou
Kagoma... Hawa wanaingia

Ahoua Jean
Che Malone
Mavambo Debora ... Hawa wanatoka

66' Steve Mukwala anapiga shuti moja kali mpira unaokolewa na Kipa inakuwa kona... Kipa analala chini kwa maumivu, anatibiwa.. Kona inapigwa na Mutale simba wanaicheza kona tena mabeki wanaokoa, Zimbwe anaitoa nje.. Goal kick

70' Sub kwa Sfaxien

Sekouhi anatoka anaingia Traore Boubacar
Daouhi nje na Becha Yusuf ndani
1-1 bado ndio matokeo

77' Sub kwa Simba

Nouma Valentin anaingia kuchukua nafasi ya Mohamed Hussein

79' Kibu anaangushwa baada ya kupress , inapigwa faulo na Nouma kipa anapangua na mabeki wanaokoa shambulizi lile

84' Simba wanaonana vizuri kuelekea Sfaxien kwa pasi fupi fupi, Wanakosa chance ya goal hapa inapigwa kona Hamza Abdulrazak anaitoa nje kwa kichwa.. Goal kick

88' Simba wabashambulia, inatolewa nje ..inarushwa kuelekea SFAXIEN namna gani pale shuti la Kapombe wa Simba linaokololewa.. Kona.. Inapigwa fupi nayo inaokolewa...

90' Dakika 7 za nyongeza kuelekea Full time

90+3' Joshua Mutale anakosa utulivu anatoa mpira nje kwa shambulizi ambalo angetulia wangepata goal

90+6' Simba wanashambulia hapa wanapata kona inapigwa inaokolewa kona tena

Kona inapigwa lakini Simba wanautoa nje

90+8' Goooooalll Simba wanapata kupitia Kibu Denis

90+9' Mpira umeisha SIMBA SC 2 CS SFAXIEN 1
This is simba guvu moya
 
Hakuna uzuri wowote kaonesha wazi wazi kuwa kaibetia Simba. Mchezaji wa CS Sfaxien alikuwa kachezewa faulo na Melon lakini alifanikiwa kuwin mpira na alikuwa anaenda kufunga kwanini hakuacha advantage pale badala yake kaona Che Melon kaachwa kapuliza kipyenga cha faulo na kumpa che Melon kadi ya njano wakati alikuwa ni mtu wa mwisho aliyezuia goli kufungwa.

Kaongeza dakika 7 bado haitoshi, hakuna tukio lolote la mpira kusimama kwenye hizo dakika lakini hakuridhika mpaka aone Simba inapata goli ili mkeka utiki
Umeumia sana na haya matokeo.😳😳
Pole sana, kunywa maji upumzike.
Siku nyingine usifuatilie mechi za Simba utakuja pata kiharusi😎😎
 
Leta msimamo utuonyeshe ufundi wako wa kusoma table standings.
Kubishana na watu wapumbavu ni mzigo sana. Angalia; hiyo tebo uliyoleta inaonyesha kuwa Timu yako imeshacheza michezo 11 na ina point 19 wakati timu unayoponga imecheza michezo 10 na ina point 17 yaani tofauti ya point mbili tu wakati mchezo mmoja una point tatu. Mpaka hapo hujaona udhaifu wa hoja yako?
 
Back
Top Bottom