FULL TIME: Simba Vs TP Mazembe(0-1) | Simba Day | Mkapa Stadium

FULL TIME: Simba Vs TP Mazembe(0-1) | Simba Day | Mkapa Stadium

Kitu ningependa tufanye tuanze kupunguza wakongwe ambao viwango vyao vinaendelea kushuka tu kila msimu na kuongeza damu mpya changa kama Banda na Sakho

Ingekuwa vyema kama huu ungekuwa msimu wa mwisho kwa;
  • Kagere
  • Boko
  • Ajibu
  • Mkude
  • Nyoni
  • Wawa
 
Shida na gundu limeanzia hapa, kuna watu hawafai kuwa wageni
IMG_20210903_090439.jpeg
 
Tuna timu changa sana aisee tukubali tu ile chemistry ya mazembe tusingeiweza
Mi naona hata hivyo Simba ni nzuri na imejitajidi sana, wale Mazembe hakuna mwenye mapungufu wanaupiga sana
 
Tukifanikiwa kuingia makundi tujiandae tu kisaikolojia hatuna timu ya kufika robo labda mwakani....
Mkuu hii timu mapungufu yake ni madogo, we Mazembe umewaonaje , tukutane na timu nyingine utawaona simba ni wazuri, mbona hata Mazembe tumekaza
 
Mkuu ndo nimefika muda si mrefu bahati nzuri nimejikuta mechi kwenye dk ya 35, tangu hiyo dk naona tunapigwa msako hatari, team haikai kabisa na mpira.

Inamaana Chama na Miquisone ndo walikuwa na impact kubwa kiasi hiki??? [emoji15] Maana team imebadilika kabisa.

Binafsi kwa uchezaji huu, inabidi tukaze mazoezi kuelekea CCL.

Utopolo pole kwa maumivu huko Nigeria
 
Mpira hauko Hivyo Mkuu, Chama Ilimchukua Muda gani Kujihakikishia Namba Simba Na Kuingia Kwenye Mfumo?, Luis Ilimchukua Muda Gani? Hatujacheza Hata Mechi Moja Ya Ushindani Mnaanza Kusema Kuna Pengo La Chama Na Luis! Mtakapo Kosea Ni Kuwafananisha Wachezaji Waliopo Na Walio Ondoka, Tulieni Kocha Atengeneze Wachezaji Wengine. Na Kwa Jinsi Walivyocheza Leo Wachezaji Wetu Wapya Ni Dhahiri huu ni Usajiri Bora, Angalia Pass anazopiga Kanute, Angalia Namna Sakho Anavyotengeneza Nafasi Angalia Uchezaji Wa Banda! Simba Ni Suala La Muda Tuuu Japo Pale Mbele Ndio hatuna Striker si Kagere, Si Mugalu si Bokko
Inawezekana wote mnapoint lakini mnashindwa kuelewana. Ukweli ni kwamba Chama na Miquissone walikuwa ni zaidi ya wapishi. Walikuwa wana full package, naposema full package namanisha wana uwezo kuanzisha mashumbulizi, wana uwezo wa kupiga pasi za mwisho, wana uwezo wa kufosi kupenya katikati ya mabeki, wana uwezo wa kufunga. Ni watu ambao wakubadilisha mchezo
 
Back
Top Bottom