Full Time: Tanzania 0- 2 DR Congo | Qualification AFCON 2025 | Benjamin Mkapa Stadium | 15 Oktoba, 2024

Full Time: Tanzania 0- 2 DR Congo | Qualification AFCON 2025 | Benjamin Mkapa Stadium | 15 Oktoba, 2024

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Leo Jumanne, Taifa Stars itakuwa dimba la Benjamin Mkapa kwa kazi moja tu kusaka ushindi dhidi ya DR Congo katika mechi ya kuwania kufuzu AFCON 2025 nchini Morocco.

Mechi hii itachezwa saa 10:00 jioni

Snapinsta.app_463344307_1112347970891075_8236581409681366406_n_1080.jpg

Mpira umeanza kipindi cha kwanza na DR Congo ndiyo wameanzisha gozi.

Dakika, 2 Stars wanapata kona.

Dakika, 4 Stars wanafanya shambulizi zuri sana na kupata kona.

Dakika 6 Taifa Stars wamefanya shambulizi zuri kutoka kwa Mzize.

Dakika,12 Sammata anakosa goli hapa.

Dakika, 18 DRC wamefanya shambulizi zuri.

Dakika, 38 Mpira umekuwa kasi sana

Dakika, 39 Kibu anakosa nafasi ya wazi

Dakika, 42 Ali Salmu anafanya save nzuri na kuwaweka salama Taifa Stars.

Zimeongezwa Dakika 3 kukamilisha dakika 45 za kipindi cha kwanza.

Dakika 45 za kipindi cha kwanza zimekamilika Tanzania 0 - 0 DR Congo.

Kipindi cha pili kimeanza

Dakika,52 Taifa Stars wamefanya majaribo mawili lakini wameshindwa kutumia nafasi vyema.

Dakika, 73 DR Congo na Taifa Stars wamefanya Mabadiliko ya wachezaji

Ametoka Mudathri anaingia Mao. Kwa upande wa DRC anaingia Mayele.

Dakika 84 Mzize anatoka nafasi yake inachukuliwa na Mwalimu Hassan.

Dakika, 86 DRC wanapata goli

Dakika,93 DRC Meshakc Anawapatia goli la pili
 
Nadhani leo ule ujinga wa kihalaiki (Mass stupidity) aliosema Profesa Assad hautakuwepo.

Tunaamini wana CCM hawatageuza hii mechi kuwa sehemu yao ya kuweka mabango ya kumtangaza Samia.

Nakumbuka mechi ya kwanza Taifa stars kucheza kwa Mkapa, maelfu ya watanzania walifurika na wakawa wanaishangilia timu yao kwa hamasa kubwa Sana.

Tatizo lilianza CCM walipoiteka nyara timu na kutaka kugeuza mafanikio yake kuwa ni ya CCM. Baadhi ya watanzania wakaisusa timu.

CCM acheni kuharibu hii timu kwa kuweka mambo ya chama chenu mbele kuliko maslahi ya nchi.

Tunajua mnapenda kuonekana mnafanikisha Kila jambo, lakini mambo mengine mnayoyafanya ni ya kijinga na kishamba.

Leo tunataka kuona uzalendo wa kitanzania kwenye hii mechi na siyo mbwembwe za machawa wa chama chenu.

Na mashabiki wa Simba na Yanga acheni ubwege wa kushutumu ama kushangilia mchezaji kutokana na timu atokako.

Wachezaji wote kwa mechi hii ni wachezaji wa timu ya Taifa na si timu watokazo.
 
Back
Top Bottom