Tate Mkuu
JF-Expert Member
- Jan 24, 2019
- 33,092
- 96,127
Hayo ni maoni yangu tu. Binafsi naona kama kuna kitu hakipo sawa kwa upande wa benchi la ufundi. Hivyo mabadiliko hayakwepeki ili timu irejee kwenye ubora wake.Mbona mapema hivi nyie mashabiki wa Yanga? Mbona hata Ulaya timu kubwa kabisa huwa zinafungwa na timu ndogo na na huwa inachukuliwa kama sehemu ya mchezo. Kufungwa mechi 2 tu, Mnataka benchi la ufundi lifukuzwe?
Majuzi tu hapa Barcelona imefungwa magoli 4-2 na timu inayodhaniwa kuwa ndogo. Hamuwezi kuwa mnashinda tu kila mchezo. Kuna kupanda na kushuka. Tuwe wavumilivu tunapofungwa kama tunavyofurahia timu inaposhinda.
