Full Time: Yanga SC 1 - 3 Tabora United | NBC Premier League | Azam Complex | November 7,024

Full Time: Yanga SC 1 - 3 Tabora United | NBC Premier League | Azam Complex | November 7,024

Mbona mapema hivi nyie mashabiki wa Yanga? Mbona hata Ulaya timu kubwa kabisa huwa zinafungwa na timu ndogo na na huwa inachukuliwa kama sehemu ya mchezo. Kufungwa mechi 2 tu, Mnataka benchi la ufundi lifukuzwe?
Majuzi tu hapa Barcelona imefungwa magoli 4-2 na timu inayodhaniwa kuwa ndogo. Hamuwezi kuwa mnashinda tu kila mchezo. Kuna kupanda na kushuka. Tuwe wavumilivu tunapofungwa kama tunavyofurahia timu inaposhinda.
Hayo ni maoni yangu tu. Binafsi naona kama kuna kitu hakipo sawa kwa upande wa benchi la ufundi. Hivyo mabadiliko hayakwepeki ili timu irejee kwenye ubora wake.
 
Wachezaji wa Yanga muache kudharau timu zingine. Mtaweka historia ya kufungwa na timu zote zinazoibukia ligi kuu. Nyinyi mazoezi makali kwa madunduka tu timu zingine aaahhh.
Ila Tabora nao wachawi, pale kipa alikuwa anaona mishale tu, wee kuweza?
 
Kesho tukutane pale Jangwani kwa ajili ya supu. Supu hii ni maalumu kwa ajili ya kujipoza na maumivu ya kufungwa. Kama ambavyo huwa tunafanya tukiwa na furaha, tufanye hivyo pia wakati huu wa maumivu. Au tubadilishe kesho tunywe kahawa chungu, bila kashata.😎🤓

Daima mbele nyuma Mwiko.
Mapambano bado yanaendelea
 
Kasongo Yeyee, Mbona wewooo alibeti leo akaipa Yanga.
images - 2024-11-07T202836.695.jpeg
 
Ninachokiona ni uchovu tu wachezaji wametumika sana week hizi mbili non stop na majeraha kadi tena sehemu zile muhimu muhimu sana.

Yaani aucho ndiyo wa kuzima beki ya kati kweli?
Mkude na Sure Boy wana uwezo wa kucheza namba ya Aucho! Lakini hawapewi nafasi. Kwa hali hiyo baadhi yao watahindwa vipi kuwa na fatique!! Wachezaji kila mechi ni wale wale! Na wanacheza mpira ule ule!!

That means kocha ameishiwa mbinu.
 
Wachezaji wa Yanga muache kudharau timu zingine. Mtaweka historia ya kufungwa na timu zote zinazoibukia ligi kuu. Nyinyi mazoezi makali kwa madunduka tu timu zingine aaahhh.
Ila Tabora nao wachawi, pale kipa alikuwa anaona mishale tu, wee kuweza?
Lakini mashabiki wao huwa wanadai kipa wao hata mishale huwa anadaka! Sijui leo imekuwaje?
 
Back
Top Bottom