Maisha hayana mshindi pambana kutafuta peace of mind. Maisha halisi ni yale ambayo unayaishi yanayokupa furaha na amani, kwa kujikubali ulivyo na kufanya yale yaliyo ndani ya uwezo. Pambana jichunguze ujielewe wewe ni nani hapa duniani then do your thing pambana na maisha haya na mahitaji yake lakini usiyaruhusu yakuzuie kupractise ule utu wako wa asili uliozaliwa nao, ile talanta, kile kipaji, ule uwezo wako, ile sifa yako unique, kwa ufupi maisha huwa tunatafuta peace of mind, na hiyo peace of mind haiwezi kuja kwa kuwa na mambo mengi ya duniani, katika maisha ukishakuwa na nyumba yako nzuri ya kuishi, ukaishi kwa amani na upendo na familia yako, hausumbuki na kuwaza pesa ya kula, una uwezo wa kusomesha watoto wako pasipo mashaka, uko na usafiri wako (kwa maisha ya kibongo bongo), ukawa na afya njema na mengineyo yafananayo na hayo hakika utakuwa na furaha ya maisha yako.
emmyta habari za muamko dadake?