Fumanizi la mama mwenye nyumba

Fumanizi la mama mwenye nyumba

Hapo kwenye mpangaji kukaa sehemu mpaka akaanza kufuga nimecheka sana. Kuna jamaa yangu hapo mwanza kapanga mahali kafuga mbuzi kama 60 nilivyoenda kwake nilicheka sana anajiita mwenye nyumba msaidizi since wapangaji wote wamemkuta.
Unakaa kwenye nyumba muda mrefu hadi mwenye nyumba anakupa kazi ya kumkusanyia kodi
 
Duuh!!! Umenifanya niogope kualika demu magetoni aisee, kama akifa si balaa[emoji28][emoji28]

Ni mwendo wa Lodge tu akizima naondoka akiamka atajua mwenyewe [emoji28]
Wakitaka kukupata wanakupata tu. Maana hata hiyo lodge lazima muende kwa mawasiliano
 
5th Portion:


..... Kati ya watu ambao inner voice huwa zinawasumbua au kuwasema endapo pakitokea msala, basi ni Mimi. Baada ya Maza house kuondoka, sauti ndani yangu ikaanza kunisuta "Haya sasa, madhara ya tamaa ndio hayo" . "Jifunze kuridhika" " Jela inakuita" n.k

Pale kitandani K alitulia, ila nikawa naogopa kumsogelea. Mawazo yananiambia nikimbie, ila sasa nitakimbilia wapi. Kila kitu changu kipo mle ndani. Nikapitisha mawazo ya kuondoka pale gheto kwa muda soo lipoe, then nitawatafuta wazazi wa Binti tuyajenge. Kabla hata sijanyanyua mguu, mlango ukafunguliwa. Nikaduwaa tu kusubiria faza house aingie nijue hatma yangu. Akawa ameingia Maza house peke yake, inaonekana faza house alienda kupiga ulabu, so alimkosa. " Ushamuua mwanangu?" Hiyo ndio ilikuwa kauli ya kwanza ya Maza house. K nae fahamu zikawa zimemrudia anashangaa shangaa pale kitandani. Maza house alimsogelea akamtandika bonge la kofi, yani hakujali kama muda mfupi uliopita alikuwa kwenye hali gani.

K akatoka nje huku analia japo sio kwa sauti, nikabaki na Maza house. Aliniangalia kama vile anakinyaa, akasikitika sana "Naomba kesho uhame, sitaki kukuona tena kwenye nyumba yangu". Nikamwambia lakini siku sio nyingi nimetoka kuwalipa Kodi ya miezi 6. Maza house aliniangaliaa, alaf akasema "Kumbe wewe akili huna, hiyo Kodi ilibidi uifikirie kabla ya kufanya ushenzi wako". Nikajaribu kutaka kujitetea, akanikatisha "Nimekwambia kesho uhame, sitaki kuyaona tena mapua yako kwenye hii nyumba". Huwa sielewagi, mtu yeyote akiwa na hasira na Mimi au tukikwazana, kitu cha kwanza anakimbilia kuisema pua yangu, inamaana siku zote hakuiona? Nikasema liwalo na liwe, hapa ngoja na Mimi nikaze, nikamwambia "Mimi sihami mpaka Kodi yangu iishe, ukimwambia faza house kuhusu tukio la leo, na Mimi naweka hadharani kuhusu sisi", akacheka "Kumbe we tahira eeh?" " Unadhani unamjua mume wangu kuliko Mimi?. Haya sawa, nimekuruhusu, kesho tutakuwa na kikao, njoo kila mmoja aweke kalata zake mezani". Hakunipa nafasi ya kuongea tena, akaondoka.

Nikabaki nimekaa juu ya meza, najiuliza maswali kibao "Anajiamini nini huyu mama?". Nikaona hapa nikijifanya mjuaji litanikuta jambo. Nikamtumia msg "Kesho mapema nitasafiri, nipatie kama wiki moja niweke mambo yangu sawa, alaf nitahama bila vikao wala ugomvi". After kuituma, nikapanda kitandani nasubiria jibu lake, ili nijue hatma yangu. Dakika 30 zikapita, Kimya! Nikaamua kulala. Asubuhi na mapema nikaamsha.

Zikapita siku 3 sijatafutwa, wiki sijatafutwa. Baada ya wiki mbili nikarudi. Naingia tu getini, mtu wa kwanza kuonana nae ni faza house, akanichangamkia vizuri tu, nikapata picha huyu hajaambiwa chochote, amani ya moyo ikarudi.

Nikaingia gheto kwangu, usalama kama wote. Nikajilaza. Nikaanza kuishi kama digidigi au panya, naondoka alfajir, narudi night kali hii yote ni kumkwepa Maza house. Siku moja nipo mishe mishe, akanitumia msg "We mpuuzi, unahama lini?" Nikamjibu "Nimeshapata chumba sehemu nyingine, ila ningependa tuongee kabla sijahama". Akajibu "Sina cha kuongea na wewe tena, beba vitu vyako, uende". Nikajitahidi kumsihi anipatie dakika 5 tu zitanitosha. Akakubali, akasema baadae atakuja.

Nafsi inaniambia "Ole wako akija uharibu, hiyo ni last chance" Sauti nyingine inaniambia "Achana na hayo mambo wewe, icho ni kifo" Sauti ya kwanza inarudi tena "Wote tutakufa". Nikaona zote zinanichanganya tu, nikaachana nazo nikaamua kujiskiliza mwenyewe.

Mida ya usiku nilivyofika gheto, nikawasha kisabufa changu, alafu nikaweka track ya Simi on repeat, ili Maza house akija inisaidie kubembeleza na kurudisha hisia. Mishale ya saa nne, akatokea, yuko very cool, no kuchangamka. Nikajaribu kubembeleza na kuomba msamaha, Maza house kakaza, sisikilizwi Mimi wala Simi.

Unajua uzuri wa haya mashangazi yanajua sana kupenda na yanaweza kufanya uhisi ule upendo uliopo. Ila tatizo lao kubwa ni kwamba mapenzi hayawapelekeshi hata kidogo, Yani Wana uwezo wa kutenganisha hisia na mambo mengine. Hawa rika letu hata mzinguane vipi, ukijirudi na kumpeti peti, analegeza, ila mashangazi akisema No ni No, na huwezi tawala hisia zake kwa 100%

Akili zao kwa kiasi kikubwa zipo kwenye utafutaji. Mfano lile lishangazi langu la kwanza, nakumbuka katikati ya shoo alikuwa anaweza kupokea simu za wateja wake au za biashara. Nakumbuka kuna siku katikati ya shoo alishawahi kuniwasha kofi la kichwani kisa nilisahau kufunga mlango wa ofisi.

Sasa na Maza house ni hivyo hivyo, jitihada zote ziligonga mwamba nikaambiwa nihame. Sikuwa na jinsi, nikakubali kuhama. Akanipa wiki 1 niwe nishatekeleza ili swala, kinyume na hapo nisimlaumu.

Nikaanza jitihada za kutafuta chumba sehemu nyingine. Kila chumba ninachooneshwa ni kibaya. Mpaka wiki niliyopewa ikaisha, sijapata chumba. Asubuhi moja Maza house akaniambia "Bado upo? Shauri yako". Sikumtilia maanani nikiamini hana anachoweza kufanya.

Baada ya kama siku 3, nikamtext kuwa natamani tuagane kabla sijahama, hakujibu.Baadae nipo zangu gheto mida ya usiku. Nikasikia purukushani nje huko. Nikaamua kwenda kuangalia. Naskia sauti ya faza house ndani anafoka sana. Nikamuuliza mke wa mpangaji mwenzangu "Kuna Nini?. Nae anasema hajui kitu. Nikamuuliza jamaa mwingine ambae nae alikuwepo, ila nae haelewi. Hatujakaa sawa, tunaona Maza house katoka ndani speed, kapitiliza hadi nje ya geti anakimbia. Dakika chache, tunaona watoto wa faza house nao wametoka nje speed. Ghafla akatokea faza house akiwa kavimba,panga mkononi. Wapangaji wote tukasambaratika, kosa nililofanya,badala ya kwenda nje, nikakimbilia ghetto. Nikaona faza house anakuja upande wangu. Au kaona ile msg niliyotuma?. Yote kwa yote Nikajua, tayari pashaharibika hapa.....
Aiseee msala haujapoa unaanza msala mwingine hapo ndipo unajua shetani akifungua dozi kabla haijaisha anapandisha nyingine tena
 
Back
Top Bottom