Fumbo linaloumiza walimwengu ni maisha baada ya kifo

Fumbo linaloumiza walimwengu ni maisha baada ya kifo

Aliekudanganya kwamba binadamu ana thamani ni nani?
Kipi kinakufanya ujione special kuliko viumbe Wengine?
Au kuvaa nguo na kua na utashi ndio unaona ndio una thamani sana Kuliko viumbe hao,
Bila shaka Bado hujaijua kanuni ya Maisha wewe Kila kiumbe kinasurvive Kwa destiny yake hata sisi hiyo ndio destiny yetu nje ya Hapo ni hekaya za kujifariji!
Mtu kazaliwa kawakuta fisi, mbwa, funza n.k halafu anatoa hitimisho kuwa ana thamani kuliko wao sababu ana uwezo wa kutumia smartphone na fisi hawezi.
 
Kwanza tunatakiwa tujue kuwa uhai ni nn, na je uhai ulio nao ukiwekwa kwenye mwili wa mende utakuwa mende au bado utakuwa na uwezo ulio nao sasa?

Uwezo wa akili ya utambuzi unatokana na ubongo wako ambao ni sehemu ya mwili wako au uhai wako?

Kama ni ubongo ukifa ndo basi maana na ubongo unakufa hata kama uhai wako utaenda kwenye mwili mwingine au kiumbe kingine utakutana na ubongo mwingine usio na kumbukumbu.
 
Mtu kazaliwa kawakuta fisi, mbwa, funza n.k halafu anatoa hitimisho kuwa ana thamani kuliko wao sababu ana uwezo wa kutumia smartphone na fisi hawezi.
Tuachane na imani. Tutumie akili tu tulizoumbwa nazo. Wewe ukitengana na huo ubongo wako unaohifadhi kumbukumbu utakumbuka nn kuhusu nyakati zilizopita?

Inafahamika kwamba kifo ni baada ya ubongo kufa.
 
Kama hujui unakoenda lazima uogope,lakini km anajua huwezi kuogopa!
Heaven is real
Hell is real!
Chaguo ni lako, kumbuka uwe na dini ama huna njia ni moja tu nayo ni Yesu!
Yesu alisema "mimi ndie njia ya kweli na ya uzima mtu haji kwa baba bila ya mimi"...
Naomba tujadiliane kuhusu hili andiko vizuri...wakristo wengi huwa mnasoma biblia ila huwa hamuielewi

Naomba tuanzie andiko lako ulilonukuu kipande ,toka linapoanzia Yohana 14:1

Yesu akawaambia, “Msifadhaike mioyoni mwenu. Mwaminini Mungu, niaminini na mimi pia. 2 Katika nyumba ya baba yangu mna nafasi nyingi. Kama sivyo, nisingeliwaambia kwamba nakwenda kuwaandalia makao. 3 Na nikishawaandalia, nitarudi kuwachukua mkae pamoja nami; ili mahali nilipo, nanyi mpate kuwepo. 4 Ninyi mnajua njia ya kufikia ninakokwenda.” 5 Tomaso akamwuliza, “Bwana, hatujui unakokwenda; tutaijuaje njia?” 6 Yesu akawaam bia, “Mimi ndiye Njia na Kweli na Uzima; mtu hawezi kufika kwa Baba bila kupitia kwangu.


Mtume Yesu anaongea na wana wa israel akiwaambia kuwa wamwamini kwanza MUNGU kisha wamwamini ya yeye (Mtume).Maana hakuna atakaefanikiwa kufika kwa Mungu ikiwa hatamwamini Mtume wa Mungu ambae ni (Yesu) kwa wakati huo. Haya ni mafundisho sahihi kabisa kuwa kila watu waliletewa mtume/nabii wao...ila lengo lilikuwa ni lile lile kuwa wamwamini Mungu mmoja tu na kisha wamwamini mtume/nabii wao. Pia sheria ya kila Mtume/Nabii huwa zinatofautiana.Kila Nabii au Mtume na zama zake na watu wake. Watakaomtii nabii au Mtume wao waliyeletewa kwa wakati huo na kumuamini Mungu basi bila shaka watapata nafasi ya kwenda katika ufalme wa milele. Napia Yesu akawaambia kuwa Mbinguni katika Nyumba ya baba yaani (MUNGU) kuna nafasi nyingi ( kwa kila watu na Mtume wao).Na akwaambia kuwa watakaomuamini MUNGU pamoja na yeye (mtume wa MUNGU) basi ataenda kuwaandalia Makao (Miongoni mwa nafasi nyingi zilizopo huko kwa MUNGU) . So kizazi cha wana wa israel waliomuamini Yesu wana nafasi yao kwa MUNGU , na wale waliomuamini Musa pia wana nafasi yao, waliomuamini Daudi pia wana nafasi yao, waliomuamini Eliya nao wana nafasi yao, waliomuamini Yona na Ayubu nao wana nafasi zao. Kila Mtume/Nabii na watu wake waliomuamini wana nafasi kwa MUNGU.

Hiyo ndio maana ya kuwa katika nyumba ya Baba (MUNGU) kuna nafasi Nyingi...na yesu ameenda kuwaandalia watu wake waliomuamini nafasi miongoni mwa nafasi nyingi zilizopo huko kwa Mungu...huwezi kumuamini MUNGU ikiwa kama hujamuamini Mtume/Nabii wa Mungu wa wakati wako.
 
Iha
Kwanza tunatakiwa tujue kuwa uhai ni nn, na je uhai ulio nao ukiwekwa kwenye mwili wa mende utakuwa mende au bado utakuwa na uwezo ulio nao sasa?

Uwezo wa akili ya utambuzi unatokana na ubongo wako ambao ni sehemu ya mwili wako au uhai wako?

Kama ni ubongo ukifa ndo basi maana na ubongo unakufa hata kama uhai wako utaenda kwenye mwili mwingine au kiumbe kingine utakutana na ubongo mwingine usio na kumbukumbu.
Uhai ni Roho...Roho inapotolewa ina maana nafsi (Mimi/wewe) haina uwezo wa kuendelea kuishi katika ulimwengu huu tena.
 
Kutoka kwa Abuu 'Abdir-Rahmaan 'Abdillaah bin Mas-‘uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: “Ametusimulia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye ni mkweli mwenye kuaminiwa: “Hakika kila mmoja wenu hukusanywa umbo lake katika tumbo la mama yake siku arubaini akiwa ni mkusanyiko wa mbegu (za uzazi za mama na baba), kisha arubaini zifuatazo huwa ni donge la damu, kisha arubaini zijazo huwa pande la nyama, kisha Allaah Humtuma Malaika kwake na kumpulizia roho (yake). Na (Malaika huyo) anaamrishwa maneno manne; Kuandika rizki yake, ajali yake (umri atakaoishi duniani), amali zake, mtu muovu au mwema. Wa-Allaahi naapa kwa Yule Ambaye hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Yeye, hakika mmoja wenu huenda afanye ‘amali za watu wa Jannah hadi ikawa baina yake na Jannah ni dhiraa na kile kilichoandikwa kikathibiti akafanya ‘amali ya watu wa motoni akaingia motoni. Na mmoja wenu hufanya ‘amali za watu wa motoni hadi ikawa baina yake na moto ni dhiraa na hapo kile kilichoandikwa kikathibiti akafanya ‘amali ya watu wa Jannah akaingia Jannah)) [Al-Bukhaariy na Muslim
 
The measure of human standard ni mind..
Kama mbwa anathaman kuliko wewe ni sawa.
😂😂😂
Akili ya ubongo wako inatoa thamani ya universe na viumbe vyake ila haijui hatma ya maisha ya hao viumbe visivyo na thamani kuliko wewe.

Mbwa mwenyewe humuelewi logistic za uumbaji wake umeipima thamani yake kwa uwezo wako wa akili ambayo nayo huielewi logistic ya uumbaji wake. PATHETIC THINKING.
 
😂😂😂
Akili ya ubongo wako inatoa thamani ya universe na viumbe vyake ila haijui hatma ya maisha yake sawa tu na Mbwa.

Mbwa mwenyewe humuelewi logistic za uumbaji wake umeipima thamani yake kwa uwezo wako wa akili ambayo nayo huielewi logistic ya uumbaji wake. PATHETIC THINKING.
Wewe ndio hujui ndio maana mbwa anathamani kuliko wewe.
Mimi najua even before ya sijakuwepo kwa dunia.
Never generalize kama wewe ni idiot its only you.
 
Wewe ndio hujui ndio maana mbwa anathamani kuliko wewe.
Mimi najua even before ya sijakuwepo kwa dunia.
Never generalize kama wewe ni mjinga its only you.
Huna lolote. Mwoga tu. Akili yako inakupa matumaini.

Halafu hakuna sehemu yoyote nimesema mbwa ana thamani kuliko binadamu ila nimehoji kwann tunadhani ss ni wa thamani kuliko mbwa, panya na viumbe wengine linapokuja suala la kifo. Wewe ni muoga.
 
Huna lolote. Mwoga tu. Akili yako inakupa matumaini.

Halafu hakuna sehemu yoyote nimesema mbwa ana thamani kuliko binadamu ila nimehoji kwann tunadhani ss ni wa thamani kuliko mbwa, panya na viumbe wengine linapokuja suala la kifo. Wewe ni muoga.
Unadhani wewe na nani?
Kama akili yako inakupa matumaini ni wewe.
Kuna knowledge huwezi kuwa nazo except by exprience we are not the same dude.
 
Soma Quran mkuu,kile kitabu kimeeleza kila kitu kuhusu hiyo safari,kitakueleza ulitoka wapi,kwanini upo hapa Duniani na je ukifa nini kitaendelea....soma Quran yenye tafsiri ya kiswahili na soma ukiwa free minded utaelewa kila kitu mkuu.

Kuna proof, maana mambo yote haya yako katika mustakabali wa imani.
 
Unadhani wewe na nani?
Kama akili yako inakupa matumaini ni wewe.
Kuna knowledge huwezi kuwa nazo except by exprience we are not the same dude.
Wewe ni muoga, na majibu yako yanadhihirisha uoga wako, hakuna experience yoyote uliyonayo zaidi ya hofu inatokana na kuhofia uendapo baada ya kifo inayopelekea your brain to play tricks with you.

Ushauri:

Kama hufahamu kuhusu viumbe hai vya ulimwengu huu na logistic behind existance yao basi usihitimishe lolote kuhusu wao maana hujui.

Binadamu hatujui hatma ya wanyama wanapokufa mpaka kuhitimisha hakuna lolote kwao zaidi ya kifo.

Thamani yetu imewazidi wao katika ulimwengu huu unaopimwa na akili zetu ambazo ni kubwa kuliko zao ila nje ya ulimwengu wa mwili na nyama hujui lolote kuhusu wao.

Hata paka huenda anaamini ana thamani kuliko panya katika ulimwengu wa akili yake.
 
Binadamu huzaliwa, kukua , kuzeeka na baadae kufa kama viumbe wengine...lakini binadamu ndo kiumbe mwenye akili nyingi kuliko viumbe wote duniani, na ndiyo maana Mwenyezi MUNGU alimpa uwezo wa kuitawala dunia na vilivyomo.

Wanasayansi, wataalamu, wavumbuzi, watafiti mahiri na mashuhuri kutoka mataifa yote duniani wameshindwa kuja na jibu linaloeleweka la nini kinafuata baada ya binadamu kufariki dunia.

Hata viongozi wa dini wameshindwa kuthibitisha fumbo hilo gumu duniani.

Wataalamu , Wanasayansi na viongozi wengi wa dini wamekuwa wakitoa majibu yao kwa hisia au ndoto zao...

Sote tunajua, wenzetu hufa kila siku majumbani, mahospitali, ajalini , usingizini, n.k n.k...

Mimi na wewe pia tutakufa kwa namna ambayo hatuijui.


Baada ya binadamu kufa, je

1. Huzaliwa upya ?

2. Huenda kuishi mbingu nyingine kama kiumbe kingine ?

3. Akifa basi amekufa kama ilivyo kwa viumbe wengine, kwamba hakuna kinachoendelea?
Wanasema eti mungu alimuumba binadamu lakini ukweli binadamu ndio aliyomuumba mungu.
Kutokana na akili kubwa ya binadamu tofauti na viumbe wengine, kwa akili yake akawa anasumbuliwa na swali kama akifa inakuaje. Ndio akaanza kua na hofu ya kifo na kuamini kuna mungu. Kila watu wakawa na mungu wao wakimuabudu na kuomba ulinzi.
Ulaya walipopata maendeleo na ujuzi kiasi wa sayansi wasomi wakaanza kupiga vita imani ya dini. Ila watawala mabwanyenye walipogundua inaweza kutumiwa kuwafanya raia kuzubaa na kukubali kunyonywa na mabwanyenye wakaitetea dini ya kikristo na kujenga makanisa. Na hata ilipofika enzi ya kugombea makoloni wakawatanguliza mamisionari afrika kuja kuzipiga vita dini na imani za waafrika wakubali ukristo uliyohimiza utii kwa mamlaka iliyopo kwamba imeweka na mungu aliyeko juu mbinguni na kwamba yuko kila mahali.
Ukweli wa kisayansi binadamu ni kama wanyama wengine. Kama vile hakuna mbinguni kwa kima, nyani ngombe na simba hakuna mbinguni kwa binadamu.
Nb: hili ni somo gumu mtu kuelewa ila tutaelewana tu siku moja.
 
Kabla ya kuzaliwa na kuja duniani unakumbuka ulikua unaishi maisha gani?
Ulipotoka hupajui na unapokwenda hupajui
 
Live and death are cyclic. The doctrine of re incarnation is real.

Roho haifi bali huzunguka mabara tofauti, viumbe tofauti ilikwa na pamoja na miti moto, maji hewa na viumbe vyote

Unaweza ukawa hujawahi kufika sehemu kabisa lakini ukifika kuna baadhi ya vitu unaviona kama uliwahi kuviona kumbe uliwahi kuishi pale ukiwa ama binadamu au kiumbe mwingine

Kuna baadhi ya kitu unadikia ndio kwanza kimegunduliwa au unasoma sehemu habari mpya lakini akili inakuonyesha kana kwamba uliwahi kukijua, kumbe uliwahi kuishi na jambo hilo.likawepo kwenye jamii hiyo muda huo
******* REINCARNATION *********
 
Back
Top Bottom