Naomba tujadiliane kuhusu hili andiko vizuri...wakristo wengi huwa mnasoma biblia ila huwa hamuielewi
Naomba tuanzie andiko lako ulilonukuu kipande ,toka linapoanzia Yohana 14:1
Yesu akawaambia, “Msifadhaike mioyoni mwenu. Mwaminini Mungu, niaminini na mimi pia. 2 Katika nyumba ya baba yangu mna nafasi nyingi. Kama sivyo, nisingeliwaambia kwamba nakwenda kuwaandalia makao. 3 Na nikishawaandalia, nitarudi kuwachukua mkae pamoja nami; ili mahali nilipo, nanyi mpate kuwepo. 4 Ninyi mnajua njia ya kufikia ninakokwenda.” 5 Tomaso akamwuliza, “Bwana, hatujui unakokwenda; tutaijuaje njia?” 6 Yesu akawaam bia, “Mimi ndiye Njia na Kweli na Uzima; mtu hawezi kufika kwa Baba bila kupitia kwangu.
Mtume Yesu anaongea na wana wa israel akiwaambia kuwa wamwamini kwanza MUNGU kisha wamwamini ya yeye (Mtume).Maana hakuna atakaefanikiwa kufika kwa Mungu ikiwa hatamwamini Mtume wa Mungu ambae ni (Yesu) kwa wakati huo. Haya ni mafundisho sahihi kabisa kuwa kila watu waliletewa mtume/nabii wao...ila lengo lilikuwa ni lile lile kuwa wamwamini Mungu mmoja tu na kisha wamwamini mtume/nabii wao. Pia sheria ya kila Mtume/Nabii huwa zinatofautiana.Kila Nabii au Mtume na zama zake na watu wake. Watakaomtii nabii au Mtume wao waliyeletewa kwa wakati huo na kumuamini Mungu basi bila shaka watapata nafasi ya kwenda katika ufalme wa milele. Napia Yesu akawaambia kuwa Mbinguni katika Nyumba ya baba yaani (MUNGU) kuna nafasi nyingi ( kwa kila watu na Mtume wao).Na akwaambia kuwa watakaomuamini MUNGU pamoja na yeye (mtume wa MUNGU) basi ataenda kuwaandalia Makao (Miongoni mwa nafasi nyingi zilizopo huko kwa MUNGU) . So kizazi cha wana wa israel waliomuamini Yesu wana nafasi yao kwa MUNGU , na wale waliomuamini Musa pia wana nafasi yao, waliomuamini Daudi pia wana nafasi yao, waliomuamini Eliya nao wana nafasi yao, waliomuamini Yona na Ayubu nao wana nafasi zao. Kila Mtume/Nabii na watu wake waliomuamini wana nafasi kwa MUNGU.
Hiyo ndio maana ya kuwa katika nyumba ya Baba (MUNGU) kuna nafasi Nyingi...na yesu ameenda kuwaandalia watu wake waliomuamini nafasi miongoni mwa nafasi nyingi zilizopo huko kwa Mungu...huwezi kumuamini MUNGU ikiwa kama hujamuamini Mtume/Nabii wa Mungu wa wakati wako.