Fundi Magari ashinda kitita cha Tsh. bilioni 1.2 sport pesa jackpot

Msiache kubeti 👇

----
Valerian Massawe (36) kutoka Kiluvya, Pwani ameandika historia ya kuibuka mshindi wa zawadi ya kitita cha fedha Sh1.2 bilioni kutoka Kampuni ya michezo na burudani ya SportPesa baada ya kutabiri kwa usahihi mechi 13 za Jackpot ya wiki iliyopita ya Kampuni hiyo.

Massawe ambaye anajishughulisha na kazi ya fundi makenika, alitangazwa leo Jumatatu Mei 16, 2022 kuwa mshindi wa Jackpoti hiyo na Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi SportPesa, Tarimba Abbas.

“Ni furaha yangu kubwa sana kwa niaba ya kampuni kumtangaza kwenu Florian Valerian Massawe kuwa ni mshindi rasmi wa Jackpot yetu akiwa amejishindia Sh1.2 bilioni.”

“Ikiwa ni takribani miezi 14 tangu kumtangaza mshindi wa mwisho wa Jackpot ambapo alipelekea Jackpot yetu kukua kwa kasi mpaka kufikia Bilioni 1 ikiwa ni mara ya kwanza kwenye historia ya Tanzania. lakini leo kwa furaha kubwa lile jambo letu limetimia,” alisema Tarimba.

Tarimba aliongeza kuwa tayari kampuni hiyo imeshakamilisha malipo ya kiasi hicho cha fedha kwa mshindi.

“Hili ni jambo la kihistoria kwa kampuni ya kubashiri kumtangaza mshindi wa kiasi kikubwa (Bilioni 1.2) kwenye sekta ya michezo ya kubashiri na kwenda kukabidhiwa pesa yake.”

“Fedha hizi alizoshinda tayari zipo kwenye akaunti yake ya SportPesa na tunafuata utaratibu ili kuhakikisha tunamkabidhi maana malipo yetu sisi ni papo hapo mara baada ya kuibuka mshindi,“ amesema Tarimba

Ni miaka mitano sasa tangu kuanzishwa kwa kampuni ya Sportpesa ikiwa imetangaza jumla ya washindi nane wa Jackpot.

Chanzo: Mwananchi
Ngoja nisuke formation awam ijayo niupige mwingi😋
 
Ujanja tu abasi tarimba anachukua pesa bila kodi hapo... Wajanja tunaelewa.
 
“Ikiwa ni takribani miezi 14 tangu kumtangaza mshindi wa mwisho wa Jackpot ambapo alipelekea Jackpot yetu kukua kwa kasi mpaka kufikia Bilioni 1 ikiwa ni mara ya kwanza kwenye historia ya Tanzania. lakini leo kwa furaha kubwa lile jambo letu limetimia,” alisema Tarimba.

Tarimba aliongeza
===
Valerian Massawe (36) kutoka Kiluvya, Pwani ameandika historia ya kuibuka mshindi wa zawadi ya kitita cha fedha Sh1.2 bilioni kutoka Kampuni ya michezo na burudani ya SportPesa baada ya kutabiri kwa usahihi mechi 13 za Jackpot ya wiki iliyopita ya Kampuni hiyo.

Massawe ambaye anajishughulisha na kazi ya fundi makenika, alitangazwa leo Jumatatu Mei 16, 2022 kuwa mshindi wa Jackpoti hiyo na Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi SportPesa, Tarimba Abbas.

“Ni furaha yangu kubwa sana kwa niaba ya kampuni kumtangaza kwenu Florian Valerian Massawe kuwa ni mshindi rasmi wa Jackpot yetu akiwa amejishindia Sh1.2 bilioni.”

“Ikiwa ni takribani miezi 14 tangu kumtangaza mshindi wa mwisho wa Jackpot ambapo alipelekea Jackpot yetu kukua kwa kasi mpaka kufikia Bilioni 1 ikiwa ni mara ya kwanza kwenye historia ya Tanzania. lakini leo kwa furaha kubwa lile jambo letu limetimia,” alisema Tarimba.

Tarimba aliongeza kuwa tayari kampuni hiyo imeshakamilisha malipo ya kiasi hicho cha fedha kwa mshindi.

“Hili ni jambo la kihistoria kwa kampuni ya kubashiri kumtangaza mshindi wa kiasi kikubwa (Bilioni 1.2) kwenye sekta ya michezo ya kubashiri na kwenda kukabidhiwa pesa yake.”

“Fedha hizi alizoshinda tayari zipo kwenye akaunti yake ya SportPesa na tunafuata utaratibu ili kuhakikisha tunamkabidhi maana malipo yetu sisi ni papo hapo mara baada ya kuibuka mshindi,“ amesema Tarimba

Ni miaka mitano sasa tangu kuanzishwa kwa kampuni ya Sportpesa ikiwa imetangaza jumla ya washindi nane wa Jackpot.

Mwananchi
Dah!...jamaa katusua vibaya mno...
 
Unadhani huyo anagawa gawa tu pesa kiasi kwamba hana Ndugu, Rafiki wala Jamaa wa kuwasaidia hadi akuite wewe ukatajirike kupitia yeye [emoji848]

Ukiitwa mahali kuna fursa basi tambua kuwa wewe ndiwe fursa.

Stuka, chukua hatua [emoji28]
Akili sana
Mmmmh! Ngonjera hizi kwenye Jackpots winners labda zile Bonus winner ndio huwa ni ukweli
Big yes haiwezekani upewe pesa nyingi kizembe kuna njia wanaweza kuzitumia ili usipate mzigo mkubwa mfano kuweka mshindi zaidi ya mmoja ikiwa kweli umetusua.

Lakini sportpesa hata Kenya mshindi alikuwa mmoja sijui huwa wanafanya nini
 
Back
Top Bottom