Fundi Mzuri wa BMW

Fundi Mzuri wa BMW

Shakir

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2012
Posts
1,627
Reaction score
1,926
Wadau,

Za mchana?
Nina BMW yangu 318i nilimnunulia shemegi yenu sasa sijui kaikorofisha nini maana haitaki kuwaka. Ni either fuse/relay, pump kimeo haivuti mafuta, umeme, nozzle etc sijajua lakini nikipata fundi mzuri ataniambia.

Wapi naweza kupata fundi mzuri wa haya magari kwa hapa Dar akanichekia?? Awe mwaminifu na asiwe na bei za kutisha!!
 
Attachments

  • IMG-20160531-WA0049.jpeg
    IMG-20160531-WA0049.jpeg
    156 KB · Views: 150
Samahan mkuu,naweza kujua consuption ya hii gari? Napenda sana bmw
 
Mkuu, kwanza msalimie sana huyo shemeji yetu. Mpaka umemnunulia usafiri mkali namna hii si haba atakuwa Mashallah!
Tukirudi kwenye suala la gari, ukienda pale Mwenge nyuma ya Tamal hotel huwa kuna mafundi wa kutengeneza gari za Mzugu hasa BMW, Range, Benzi and the likes. Kawacheki. But usiruhusu wachokonoe chokonoe gari. Siku hizi kuna computer (diagnostic kit) ambayo ikichomekwa kwenye system ya gari inaweza kujua ugonjwa then ndio wanatengeneza. Kupima gari kwenye computer roughly ni Tsh elfu hamsini.
 
Ushauri: fanya kwanza computer diagnosis. Kuna jamaa najua wanafanya. Ukiitaji nitakupa namba.
 
Peleka Noble Motors Nyerere Road ndiyo dealer wa BMW na kuna mzungu wa kijerumani kwa ajili ya BMW. Ila uwe na cash maana dealer si Fundi Nyange.
 
Hebu google hilo tatizo kama ni jepesi ulifanye,lakini kama ni zito fuata ushauri huo wa wadau.
 
Samahan mkuu,naweza kujua consuption ya hii gari? Napenda sana bmw
Hii gari ingawa ni ndogo but ni CC 2,000,
Na ulaji wake wa mafuta ni zaidi ya CC 2000 za Toyota ya Mjapan.
Yaweza kua Kilometa labda 7 au 8 kwa town trip
 
Mkuu, kwanza msalimie sana huyo shemeji yetu. Mpaka umemnunulia usafiri mkali namna hii si haba atakuwa Mashallah!
Tukirudi kwenye suala la gari, ukienda pale Mwenge nyuma ya Tamal hotel huwa kuna mafundi wa kutengeneza gari za Mzugu hasa BMW, Range, Benzi and the likes. Kawacheki. But usiruhusu wachokonoe chokonoe gari. Siku hizi kuna computer (diagnostic kit) ambayo ikichomekwa kwenye system ya gari inaweza kujua ugonjwa then ndio wanatengeneza. Kupima gari kwenye computer roughly ni Tsh elfu hamsini.
Nimeshapajua pale Mkuu, ilipokua stand kwa kule nyuma yake.
Sasa kuichokonoa chokonoa hapo ndio sijaelewa Mkuu, maana si itabidi niwaachie gari kama tatizo ni kubwa,
Na wamfahamu mtu mwenye hiyo Diagnosis Kit nimpatie hiyo fifty anifanyie??
Nakuja Inbox Mkuu
 
Ushauri: fanya kwanza computer diagnosis. Kuna jamaa najua wanafanya. Ukiitaji nitakupa namba.
Yeah,
Nisaidie namba mkuu, kuna jamaa pale juu kaniambia wanafanya kwa 50
 
Peleka Noble Motors Nyerere Road ndiyo dealer wa BMW na kuna mzungu wa kijerumani kwa ajili ya BMW. Ila uwe na cash maana dealer si Fundi Nyange.
Dah,
Mkuu kule gharama za matengenezo si zitafikia bei ya kununua Vitz used hapa mjini??
 
Diagnosis zipo sehemu nyingi tuu siku hizi fundi yeyote wa garage ya kawaida anaweza kuku direct kwa mwenye diagnosis
Wale wazee wa mwenge usithubutu kugeuza jicho watalamba spare orijino zote pameshachafuka pale* gari za umeme mchawi diagnosis kit tuu.
 
Au nimchukue mtu wa Mwenge nimlete home aitengenezee Home nikiwepo?? Na ukiacha wale wa mwenge pengine wapi tena ambako ni Watalaamu wa hizi mambo??
 
Obvsly hapo lazma fundi aje na mashine yake, ss gari haiwaki utaipelekaje? Swala ni kugundua ugonjwa kutengeneza ni jambo lingine mkuu
 
Kweli aisee,
Ila si umesema kwenye kutengeneza ndio hua wanapiga vifaa??
Sasa mimi hata akigundua tatizo nambana aitengenezee hapohapo
 
Tatizo la Dar kila fundi mwizi. Kuna siku mi nimenunua gari nikaomba aje fundi anichekie, yaani fundi tapeli akamtuma fundi ambaye hata hajui ufundi, nikamuuliza swali moja tu akaenda chaka, yaani watu wa Dar unahitaji kuwa makini sana, wanaweza kujifunzia kwenye gari lako. Na pia wezi sana. Bora ungeweza nenda kwa service provider wa BMW
 
Kweli aisee,
Ila si umesema kwenye kutengeneza ndio hua wanapiga vifaa??
Sasa mimi hata akigundua tatizo nambana aitengenezee hapohapo
Ujue ni mara chache sana watu wenye diagnostic machine wawe wanatengeneza na magari pia, mara nyingi wao hugundua tatizo lets say labda ni "control box" atakwambia badilisha or kifaa chochote kile kama ni plug and play ataweza kukufanyia hata yy, vitu mf. Plugs or hyo control box......lakin ikiwa tatizo kubwa atakwambia mwambie fundi wako abomoe kitu flani au yeye atakuelekeza mafundi anaowajua baada ya kugundua hyo shida
 
Nimekupata Mkuu wangu, ahsante sana na ubarikiwe
 
Back
Top Bottom