Ukweli ni kuwa tunahitaji watu wengi sana walio kama Diamond Platnumz na Harmonize. Industry ya Muziki wa Bongo Flavour inawahitaji kwa wingi, ili iweze kustawi na kukua.
Hivyo, Harmonize hana budi kuondoka na kujitegemea, Kama sio leo basi kesho. Lakini, ni ubinadamu wa kawaida kabisa kuondoka kwa ustaarabu kwa watu waliokusaidia, umekuwa nao kwa muda mrefu na mmefanya nao mambo mengi.
Unapoaga na kuondoka kistaarabu na kila mtu akiwa na amani na wewe, inakusaidia; kwanza, kukaribishwa tena hata ikitokea ukakwama huko uendako na pili, utaweza kushirikiana nao vizuri hata baada ya kuwa umeshaondoka.
Umoja ni nguvu. Harmonize aendelee tu kushirikiana na WCB hata baada ya kuondoka, kama atafanya hivyo. Itamsaidia sana kukua kwa haraka.
Hakuna haja ya kuondoka kwa vurugu na vita, otherwise iwe ni kutafuta kiki.