Funga Juma: Masufuria ya Nyama: Siyo Wote Walioondoka Misri Walitoka Misri...

Vipi wakati wa hiyo safari ya Misri Musa mwenyewe aliua waisrael wangapi safarini ??

Na je, wakati wa safari Musa aliwanyima chakula wenzake huku wakiwa safarini ilimradi punda afike Kanaan ( huku yeye Musa na kundi lake kina Yoshua wakineemeka ) ?

Kuhusu kujitegemea hakuna mtu asiyependa nchi yetu IJITEGEMEE ila kusema Magu alikuwa anapeleka nchi yetu kujitegemea ni uongo asilimia 200.

Magufuli hakuwahi kukataa misaada, na tena alikuwa anatumia mbinu zote alizoweza kuhakikisha anapewa. Mfano:
  • Uwepo wa kina Halima Mdee bungeni hata kama ni kinyume na katiba, lengo ni kuwinda misaada tena kwa gharama kubwa ya katiba na fedha
  • Pesa za COVID-19 kutoka EU alizoa na haijulikani alipekeka wapi wakati alikuwa haamini kama Tanzania kuna COVID. Tena hizo pesa alichukua kimya kimya, bila kamati ya EU yenyewe kusema tusingejua
  • Pesa za WB za elimu kwa watoto wa kike. Yaani watoto wa kike waliopata ujauzito kurudi shule hakutaka ila pesa alitaka mpaka kina Zitto kutaka kuuawa.

Magufuli alikuwa anapinga misaada ambayo aliona dalili tu kuwa haaawezi kumpa kutokana ukiukwaji mkubwa wa Demokrasia, utawala bora na haki za binadamu.

Unajifanya hukitaki kitu ambacho, mwenye nacho ameshasema hakupi. In short Magu alikuwa anaona watu kama watoto fulani wajinga.

Hata pesa za kugharamia uchaguzi mkuu, siyo kwamba nia yake ilikuwa kunitegemea.

Nia ya Magu ilikuwa ni kukwepa waangalizi wa kimataifa kwenye uchaguzi hasa ukichukua pesa za UNDP kwasababu ni moja ya masharti yao.

Na hakuna asiyejua namna Magu alivyotumia majeshi, mauaji na uporaji kuipata Dola mwaka 2020.

Namfanisha na yule Mkulima wa kwenye biblia aliyevuna sana akatia ghalani, halafu akasema sasa nafsi yake ni kunywa, kula na kufurahi. Magu alikuwa ameshamaliza, kina Lissu wameshakimbia, kila mtanzania ameshakata tamaa. Bunge, mahakama, serikali vyote vyake. Mungu akasema NO hata Urais wa awamu ya pili hajakaa sawa.

Magu alikuwa ni shetani wa damu. Alikuwa katili hasa tena wa damu.

Tena alikuwa mtu anbaye hata kama huna tatizo naye, yete analala anawaza akamuumize nani.
 
Hayati Magufuli ni mmoja wa watanzania ambao wanajitambua na yeye alikuwa ni mtu aliejitambua.

Hii ni sifa moja kubwa sana ya binadamu, kujitambua.

Hayati Magufuli alijitambua na hata wengine kama mimi Richard najitambua na naamini Paschal na Mwanakijiji pia mwajitambua.

Watanzania waafrika wengi na hata baadhi ya wazungu waliweza kuona hilo kuwa hayati Magufuli alijitambua na aliweka alama ya bara la Afrika kwenye koti lake.

Ni kweli akiwa binadamu na yeye alikuwa na kasoro zake na hilo halina ubishi ila twasimamia masuala ya msingi aloyatenda na kuyatekeleza.

Moja ya mambo mazito yanothibitisha kuwa watanzania wachache hawajitambui ni kuonyesha kushangilia kifo chake wakati waafrika wengi walisikitishwa na tukio hilo na hata kutuuliza watanzania nini kimetokea?

Sasa baadhi ya wazungu na waafrika wengine hawapendi kuona waafrika wenzao wanajitambua maana wanahisi hapatashikika.

Kama hayati Magufuli aliweza kutikisa kila mahali na pakatikisika na akaja nchini bwana mkubwa wa uchimbaji madini kutoka Canada, basi alikuwa ni yeye na hatatokea Magufuli mwingine tena ndo imetoka hiyo.

Lakini bara la Afrika bado lina waafrika na watanzania wengi ambao bado hawajajitambua na ikifika siku wanajitambua itakuwa ni siku ya kiama na tutakuwa tumechelewa maana yeye alikwishasema tumecheleweshwa mno.

Ushuhuda ni madudu ambayo yameanza kurudi baada ya kuondoka kwake duniani, mara TRA kuna mitambo imeharibika, mara TANESCO mfumo wa LUKU umeingiliwa, mara majambazi yamerudi na mara bandarini kuna figisu zimerudi hii yote ni kuonyesha kuwa watanzania bado hawajaweza kujitambua.

Hapo awali , tulisikia mara Kitalu C kilianza kuingiliwa mpaka pale mama Samia alipoamuru ulinzi uimarishwe.

Pia tumesikia wizara ya fedha watu wamesimamishwa kazi kwa ubadhilifu wa fedha na hiyo ni wizara ya FEDHA yaani hazina ya nchi!

Watanzania wenzetu hawa bila woga wameingia hazina na kukwapua fedha za walipa kodi!!

Hivyo, kwanza watanzania waweze kujitambua kuwa wao ni nani na wapo Tanzania kwa kusudio la Mungu ambae amewapa rasilimali na uwezo mkubwa wa kumiliki rasilimali hizo hivyo wahitaji usimamizi.

Kinachohitajika ni kujitambua, kisha kuhakikisha twazisimamia rasilimali hizo na kuzigeuza kuwa utajiri kiasi cha kumsaidia kila mtanzania aliezaliwa Tanzania na yule alie na vinasaba vya utanzania kwa elimu bora, makazi bora na maisha bora.
 
Wakati hao Wamisri wanalalamika njaa..., Musa alikuwa anakula peke yake na watu wake (minority) wakati wengine wana njaa (majority) au wote walikuwa wamefunga mikanda ?

Au all animals are equal but some are more equal ?
 
Uwe makini pia, awamu fulani ilikuwa haitaki wala kupenda kusikia habari mbaya zinazoihusu....hata kungekuwa na wizi kiasi gani hakuna mwandishi ambaye angeweza kuandika habari yayote wala kiongozi kuzungumzia huo ubadhirifu.....kupitia awamu hiyo kitu kinachoitwa transparency kilifutwa na hakikuwepo...

Moja ya changamoto zinazoikabili awamu hii ya Mama ni namna akili za watu zilivyojiseti baada ya kumezeshwa vitu vingi vya viongo na propaganda nyingi ambazo watu walizamishwa kuamini maana hakuna chombo cha habari ambacho kingeandika tofauti na alivyotaka bosi mkubwa mmiliki wa dola na maguvu yote..

Transparency ilimfanya JK akaonekana dhaifu na CDM kupata nguvu, lakini hata JK angeamua kuwa na tabia za jamaa kunyamazisha na kuficha mambo tusingejua kitu wala kuhoji kitu na JK tungemuita Malaika wa duniani....Mama ameamua kuuishi transparency, tunajua meeengi na kumpopoa sana Mama lakini ukweli kama Watanzania tunapaswa kukemea tabia mbovu na kuipa pressure serikali pressure itende inavyopaswa hii ni kww serikali yeyote na italeta faida kww nchi...

Siasa za kuchagua upande hazina maana kwa Watanzania na nchi...wananchi tunapaswa kupima mambo na kuyapigia kelele kwa maslahi ya umma....siasa za kuchagua upande either kwa misingi ya Dini, kabila, dhehebu nk ni mbaya sana na hazina faida kwa umma...
 
Zilikuwepo taarifa za wizi na ubadhilifu wakati huo au hukuwa unafuatilia?

Wizi khasa katika halmashauri ulikuwa ni mwingi tu na watu walikuwa wakikamatwa.

Na hata viongozi wengi walifukuzwa kazi kwa uzembe au kusababisha hasara.

Suala jingine ambalo bado ni tatizo kwa vyombo vyetu vya habari ni uandishi makini na kujitambua.

Vyombo vya habari za nje kwenye masuala yanohusu taifa au maslahi ya taifa vyombo hivyo huwa pamoja kabisa.

Kwa mfano ugonjwa COVID -19 vyombo vya habari vyapaswa kuelimisha jamii zaidi kuliko kuonekana vinasaidia propaganda kutoka nje kwani hilo ni suala linalohusu maslahi ya taifa na mstakabali wake.

Pili, vyombo vya habari vyapaswa kuchambua ni kwanini Dangote aliondoka nchini na ni kwanini anarudi mida hii?

Wanapaswa kuhoji kwanini Tanzania inaruhusu viwanda vya kigeni kuzalisha mbolea nchini?

Maana mbolea inahusika na uzalishaji vyakula na mazao mbalimbali ambavyo vyote vyaingizwa katika usalama wa vyakula yaani "Food Security" na je taratibu zote zimefuatwa?

Hivyo haya ni masuala ambayo ukitaka kuyadadavua inabidi kwanza uwe umejitambua kabla ya kuruhusu kila mtu alete malighafi za mbolea ambazo hufahamu kama zitaleta madhara kwa mazao na ardhi yetu.
 
Waandishi wengi wa taifa hili ni makasuku mkuu
 
Hapa huyo myunani hawezi kukujibu maana Musa hakuwa mroho/mbinafsi wala mungu mtu
 
Tatizo la binadamu ni kiburi chake cha asili. Huwa anapanga mipango yake halafu Mungu anatekeleza makusudio yake ambayo humuacha Binadamu akiwa mdomo wazi haamini anachokiona.

Usiku ule wa tarehe 17 March mtu mmoja alituma message kwenye group la whatsapp kwamba Mama Samia anatangaza kifo cha JPM, nikamwambia asiweke kitu kwenye group pasipo kuwa na uhakika, ndani ya dakika chache ikathibitika kuwa kweli msiba umelikumba taifa.

Kumwangalia Mama Samia anaongea mbele ya kamera akielezea kuhusu msiba, ndio kichwani ikaja picha ya ukuu wa Mungu, kwamba yule Mama ambaye alionekana ni msaidizi tu wa Rais JPM kuanzia dakika ile alikuwa ndio Rais wa nchi mpaka 2025.

Ukuu wa Mungu hauwezi kuhojiwa na kuelezewa kwa akili za kawaida za binadamu. Siku zote unazidi uwezo wetu, mipango yetu, tamaa zetu. Ni ukuu ulio juu kuzidi namna tunavyoweza kuuelezea.

Sasa jamaa wengi tu bado ni kama hawakubaliani na uhalisia wa kinachoendelea. Rais Samia hakutegemea kuja kuwa rais lakini cha muhimu sio kuangalia upungufu wake halafu mtu akadhani anaikomoa Tanzania. Hii nchi tunaiacha na hatujui ni lini.
 
Na Kundi kubwa ktk waliotamani kurudi Misri ni watendaji wa serikali ambao kwa Tamaaa ya nyama ya kwenye sufuria walisahau maumivu ya mijeledi mwilini mwao na mateso yasiyo na mwisho.
Hawa ndo walilalamika maji,umeme usio wa uhakika,foleni zisizoisha,uwizi na ujambazi,mauaji holela ya ma albino,posho kubwa za mabosi wao,ada kubwa za shule za private n.k,Hawa ndo wamesahau kurudi kwao Misri utumwani Basi ni mateso yasiyo na mwisho kwa vizazi vyao.

Ila tumewajua,wamejazana mtandaoni wakimdemsha mama wakati huku mtaani hali ni tofauti,watu wakimkumbuka Mussa aliyeanza kuwapeleka nchi ya ahadi.
 

Tuko pamoja kabisa ndugu yangu.
Umetaja watu hatari ambao licha ya kwamba wako jangwani, mioyo na akili zao bado zinaota Misri. Wanakumbuka matikiti maji, makoma manga, mapande ya nyama n.k. Lkn pia kuna wengine ambao wako jangwani, lkn wao kazi yao ni kufuata umati. Wenyewe wakisikia "kazi iendelee" kuelekea Kanaan kweli wanaongoza kuelekea nchi ya ahadi. Lkn pia wakisikia sauti za wale wanaokumbuka matikiti maji na mapande ya nyama wakinung'unika, nao bila kuwaza wamaanza kulia kwa sauti kubwa kuikumbuka Misri. Hawaeleweki wanataka nini, ama kwenda mji mpya au kurudi Misri. Lkn pia hawajui ya kuwa wale ambao wana mahaba na Misri walikuwa wakifaidika au kuwa na masilahi fulani huko. Lkn hawa fuata upepo wamekuwa wakiwaiga bila kujua sababu za kwa nini wanakumbuka mambo ya kale!! Ndivyo ilivyo kwa Tanzania, kuna wengine kipindi cha JPM walikuwa wakiiga mkumbo wa kulalamika bila kujua wale walioanzisha kulalamika kwa nini walifanya hivyo, pia walipoteza kitu gani kutokana na ule mfumo wa kale mpaka wanalalamikia mfumo mpya. Hawakujisumbua kujiuliza maswali hayo, wakabakia kulalamika tu, bila ya kujua kuwa wanatumika kama kikuza na kipaza sauti cha wanufaika wa mfumo wa kale.
Tuna tatizo la watu wengi tu kutokuwa na subira na kuzipa nafasi nafsi zao kabla ya kulaumu au kushutumu. Hilo sitalifafanua maana kila mmoja anajua. Wengi wetu tumeingia kwenye mtego huo wa kutamka tu jambo bila kujipa muda wa kutosha kuona mambo. Kwani wahenga walisema muda/wakati ni hakimu mzuri.

NB: Tabia ya ulalamishi na kunung'unika ni mbaya sana. Kama unakumbuka kunung'unika na lawama za waisraeli, ndizo zilizosababisha Musa kutoingia nchi ya ahadi. Naye alikufa jangwani. Hivyo kulaumu kuna athiri utendaji wa viongozi wetu.

CC: gwandumi Mwakatobe nakualika uje usikilize hadithi ya hadithi ya Musa na Waisraeli jangwani.
 
Na sio lazima tuone sisi, bali hata wajukuu wetu wataona tunayoyatamani.
Hiyo ndo "mindset" ya mtu tumuitae "mzungu".

Wazungu walijenga Ulaya kwa gharama na taabu nyingi na leo hii wametulia na wajukuu hawana shida ya maji, umeme wa uhakika, miundombinu imara na kila tukionacho Ulaya na Marekani kilitokana na mababu zao kutolea jasho na kutaabika.

Kwanza Ulaya au Marekani mtu hujiuliza mara mbili atachezea vipi mfumo wa umeme kama Luku, au mifumo ya kutoa mizigo bandarini au kule TRA (kama kweli kulitokea zengwe).

Si kama hayafanywi, lakini hutendwa katika maneo ya watumiaji. Kwa mfano wahalifu huweza kurekebisha kifaa cha umeme na kutolipa bili ya umeme ili kustawisha zao la bangi nyuma ya maeneo ya viwanda.

Lakini kutokana na mfumo imara huweza kugunduliwa na kukamatwa mara moja maana mfumo imara wa tehama huweza kugundua bili kubwa ya umeme kutoka katika nyumba au jengo fulani.

Sasa hiyo ni mifumo imara na iliyo thabiti.

Au mzungu atajiuliza aanzie wapi kwenda hazina kama ya Federal Reserve ya Marekani au Treasury ya Uingereza aingie na aandike hundi za kughushi na watu walipane malipo yasoeleweka?

Wajukuu na vitukuu vyetu vitakuwa na shida sana maana bado matatizo ya kufikiri nje ya boksi kwa sisi babu zao bado ni kitendawili.
 
Kongole sana mkuu kwa andiko lako hili lililojaa mantiki na kufikirisha pia. Wajuzi wengi katika masuala ya "organisation behaviour" wanakubaliana kuwa "vision statement" ya kale kabisa katika kumbukumbu za kihistoria ni hii ya wana wa Israeli walipokuwa utumwani Misri, yaani kwa kuinukuu;

"Tuondoke Misri (utumwani) na tuelekee nchi mpya ya ahadi (Kaanani) iliyojaa maziwa na asali"

"Vision statement" ndiyo dira yenye kusimamia njozi ama ndoto ya matamanio ya jumuiya yoyote ile ambayo ipo kwenye mkwamo ama hitaji la wakati la kuhama kutoka hatua moja kwenye nyingine ya maendeleo. Ni vyema wahusika kwa pamoja wakashikamana na dhamira hiyo kupitia ktk umoja wao.

Ni kosa kubwa kwa wanajumuiya mmojamoja ama baadhi yao kwenda kinyume na dhamira hiyo. Ni usaliti kurudi nyuma ama kukwamisha wengine pale mnapoamua kuianza safari hiyo ya matamanio ili mkapate kufikia ndoto iliyokusidiwa yaani matokeo chanya (maziwa na asali).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…