Fungieni huu wimbo unahamasisha Umalaya kwenye Jamii

Fungieni huu wimbo unahamasisha Umalaya kwenye Jamii

Wimbo mbaya kuna mstari wanaimba;

'Na ukipata limama, eh likomoe
Likupe pesa huu mwaka utoboe'

Ni upuuzi wa mwisho yaani na vijana wana ukariri kama kasuku
Taasisi nyingi za sirikali zimepwaya kiutendaji ikiwemo BASATA.

Kama vile kuna nguvu ya kibiashara imewalalia mpaka wamekosa pumzi.
Nchi imekamatwa na wenye maokoto!
 
DANGA(nomino) uvugua

DANGA: (nomino) kiazi kikuu cheupe chenye ungaunga ambacho husongwa na kuwa kama ugali.

DANGA: (kitenzi) kitendo cha kutafutafuta kitu kilicho adimu.
Fasili hii ni kwa mujibu wa kamusi ya baraza la kiswahili zanzibar.
 
Kaa kwenye nafasi yako, tuheshimiane.!!
Usitake kujifanya mjuaji, unaweza ukatuwekea maana halisi ya “kudanga” au umesikia kwenye nyimbo tyr umejibeba kuja kujaza server za Mello na minyuzi yako ya kufatilia maisha ya watu.?
Nani kakufuatilia Mkuu.?
 
Kuna wimbo unaitwa "Huu Mwaka".

Kiukweli huu wimbo leo ndio mara yangu ya kwanza kuusikia. Nimeshangaa sana kusikia muimbaji akisema "Kudanga Danga sana ila usisahau kujenga kibanda"

Wimbo kama huu unawezaje kuachiwa uchezwe kwenye vyombo vya habari na wakati unahamasisha Umalaya/Kudanga kwenye jamii yetu.

RC Chalamila amekuwa anapambana kutokomeza biashara ya ngono, ameshindwaje kuuzuia huu wimbo usichezwe kwenye vyombo vya habari kwenye jamii yetu.?

Huu wimbo mtoto mdogo akiusikia unamjenga au unambomoa kimaadili?

NB: Mimi sisikilizaji Bongo Fleva ndio maana nimechelewa kujua kilichoimbwa kwenye huo wimbo.

Written by Mjanja M1
Zinazofungiwa ni nyimbo zinazowaanika wabadhirifu wa Tz! Nyingine zote ruksa!

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Kuna wimbo unaitwa "Huu Mwaka".

Kiukweli huu wimbo leo ndio mara yangu ya kwanza kuusikia. Nimeshangaa sana kusikia muimbaji akisema "Kudanga Danga sana ila usisahau kujenga kibanda"

Wimbo kama huu unawezaje kuachiwa uchezwe kwenye vyombo vya habari na wakati unahamasisha Umalaya/Kudanga kwenye jamii yetu.

RC Chalamila amekuwa anapambana kutokomeza biashara ya ngono, ameshindwaje kuuzuia huu wimbo usichezwe kwenye vyombo vya habari kwenye jamii yetu.?

Huu wimbo mtoto mdogo akiusikia unamjenga au unambomoa kimaadili?

NB: Mimi sisikilizaji Bongo Fleva ndio maana nimechelewa kujua kilichoimbwa kwenye huo wimbo.

Written by Mjanja M1
Ungeutuma ingependeza maana huo wimbo wengine hata hatuujui
 
Kwa tafsiri ya jamii yetu neno kudanga linamaanisha nini?

Umeusikiliza huo wimbo mwanzo mpka mwisho?
Jamii inapotosha na wewe unaendelea kupotosha baada ya kutoa elimu watu wasifikiri hivyo.
Mzee kasome mwenyewe kamusi uone maana ya neno kudanga.
Toa elimu kuhusu neno hilo na si kuleta ngonjera kubali kujifunza kuliko kusema jamii inasema nn
 
Back
Top Bottom