Teslarati
JF-Expert Member
- Nov 21, 2019
- 2,621
- 10,466
Habari wana jamvi
Nimeona niweke huu uzi asubuhi sababu mida hii ndo wenye nyumba huwategeshea vijana wapangaji wao wanaoonekana kujiweza kdg kiuchumi na kuwaelezea shida zao ili wawasaidie.
Kuna dogo mmoja kumpa mwenye nyumba wake 30 au 20 ilikuaga kawaida. Siku mzee yule akamfuata dogo akamwambia kuwa mwanae kakosa ada, hivo amkopeshe laki 5 watakata kwenye kodi, dogo akasema laki tano hana muda ule ila akampa yule mzee laki tatu. Hadi kuombana ada ni sababu wameshawekeana mazoea ya kuombana hela.
Sasa miezi mitatu ilopita dogo aliumwa sana hadi akapewa likizo kazini kwake, kakaa pale na demu wake anauguzwa kwa miezi miwili hivi, hospitali wamezunguka sana so dogo kiuchumi akawa hayuko vizuri. Kinachofanya niandike huu uzi ni kwamba huyo mwenye nyumba kashindwa kumvumilia dogo miezi miwili tu amtafutie kodi yake.
Dem wa huyo dogo ni ndugu yangu wa mbali ndo alinitafuta nimsaidie na akanisimulia story nzima. Nimefika pale kwao juzi nikamuangalia yule mzee na alivyo hana aibu anasema eti "Wadogo zako wanakaa na mm vizuri, ni watu wazuri" lakini kumvumilia mgonjwa tu kodi, tena anaekusaidiaga imekua gumzo.
Vijana mnaoanza maisha epukeni kutoa misaada ya hovyo hasa kwa watu kama wenye nyumba wenu mlipopanga vyumba au fremu, hio sio roho mbaya bali ni kujielewa. Weka akiba kisha saidia unapoweza. Ukiwa 'nice guy' utatumika sana