Funzo kutoka Kenya: Katiba mpya au Tume huru sio suluhu ya uchaguzi wa Amani!

Hata Marekani walimtangaza huyo walienae na kukiwa na malalamiko kwa upande wa pili. Katiba ni uamuzi wa mtu na si mwarobaini wa matatizo tuliyonayo. Sasa kwa mfano TZ mbona nchi inakwenda vyema kwa kutumia hiyo hiyo katiba watu wanasema mbovu? Hakuna haja ya katiba mpya nakuunga mkono. Tuwe tunachagua watu serious tu kama Pombe inatisha sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukuku tu hamna hoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tangu siku ile prof kabudi alivyofafanua kuna nchi hazina sio tu katiba mpya bali hazina katiba kabisa na maisha yao yanakwenda mfano uingereza,israel,new zealand na Canada nilijufunza katiba sio mwarobaini wa matatizo ya mtanzania wakati wote.
Lkn halitakiwa kusema badala ya katiba zinajiendeshaje kama nchi! Kwa sababu kutakuwa na mfumo uliopo unaochukua nafasi ya katiba na ndio maana wanaendesha mambo yao vema zaidi ya nchi kama zetu zenye katiba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tangu siku ile prof kabudi alivyofafanua kuna nchi hazina sio tu katiba mpya bali hazina katiba kabisa na maisha yao yanakwenda mfano uingereza,israel,new zealand na Canada nilijufunza katiba sio mwarobaini wa matatizo ya mtanzania wakati wote.
Nakuunga mkono kamanda. Katiba ni makaratasi tuu. Ingekuwa na umuhimu basi nchi tajiri ndio zingekuwa za kwanza kutekeleza.
 
Umeona maana ya kuwa na Tume mpya we mburula.
Hichi ki thread nimekitafuta sana
 
Umeona maana ya kuwa na Tume mpya we mburula.
Hichi ki thread nimekitafuta sana
Unadhani Uchaguzi utakaorudiwa hautakuwa na figisu?

Unaujua msimamo wa NASA kuhusu IEBC iliyovurunda kwenye uchaguzi?

Tusubiri tuone!
 
Sasa nimejua agenda ya CCM kutaka kuwaziba mikono mawakili na wanasheria chini ya Waziri wa sheria ni namna tu ya kujilinda na utekelezaji wa haki kwa wananchi. Pia kitendo cha kuhodhi Jaji mkuu kuteuliwa siku zote na Rais ni janja hiyohiyo, kuzinyima mahakama fedha ndo yaleyale. Kweli Africa viongozi wanalewa madaraka. Mungu atawaadhibu sana nyie
 
Unamaana hata hii iliyopo( ya 1977) ifutwe tuishi bila katiba? Unadhani kama Kenya isingekuwa na katiba nzuri hali ingekuwaje? Kimsingi baada ya katiba nzuri kazi muhimu inayofuata ni kujenga taasisi muhimu za kitaifa kama mihimili mingine ya dola- Mahakama, Bunge na taasisi nyingine zinazotakiwa kusaidia uhuru wa kuwapata viongozi. Kazi haiishii kuwa na katiba nzuri. Katiba nzuri ni mwanzo mzuri na sahihi.
 
Kuna haja ya kufikiri kwa mapana zaidi.Katiba mpya sio tatizo! inaweza ikawa mpya lakini mbaya kuliko ya zamani, inaweza ikawa mpya lakini dhaifu inaweza ikawa mpya isiyojitosheleza.Inahitajika katiba mpya na bora hicho ndio tunachopasa kujifunza toka huko ulikokutaja!
 
Kinachoendelea Kenya ni Raila kuchukua silaha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…