Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sio kuogopa katoa mfano wa kenye ilitakiwa umpinge kwa hoja sio kumuangushia Zigo la wogaTutengeneze katiba nzuri na tume huru ya uchaguzi halafu hayo mengine tutajua mbele ya safari, kwani mnaogopa nini
Always I told those stupid!Nitoe pole kwa familia ya mkuu wa ICT wa Tume ya Uchaguzi ya Kenya kwa msiba wa kusikitisha na ulioacha majonzi.
Kabla ya kuwa na katiba mpya wapinzani na pengine wengi wa wananchi wa Kenya waliaminishwa kuwa majanga mengi yanayohusu uchaguzi,amani na hali ya ujumla ya uendeshaji wa Taifa hilo hayakwenda vyema kwa kuwa hakuna katiba nzuri inayoweza kusimamia hali ya mambo.
Pia kulikuwa na kilio kikubwa juu ya uhuru wa Tume ya uchaguzi ,kwa wanaokumbuka kuna mtu maarufu hapo Kenya ukiongelea Tume Huru ya Uchaguzi akiitwa Kivuitu..huyu alitangaza matokeo Ikulu na Rais Kibaki akaapishwa hapo hapo na baada ya hapo alikwea pipa kuelekea South Africa.Kipindi hiki Tume iliitwa sio huru na ikapelekea mfumo wa Tume unadilishwe kwa sababu hii na pia kwa sababu ya katiba mpya ya Kenya.
Kwa ufupi kilio hiki au imani potofu "myth" hii sio jambo la kipekee kwa nchi ya Kenya bali ni jambo au imani ya wanasiasa wengi barani Africa.
Kila uchao ni lazima usikie kilio cha Tume kutokuwa huru au katiba kuwa mbovu...
Haijawahi kuwekwa kiwango cha uhuru wa Tume duniani kote...yaani kwa wanasiasa kila wakishindwa lazima utalisikia hili neno.
Tukirejea hapa nchini kumekuwa na kilio cha namna hii kwa miongo kadhaa sasa kiasi cha kumfanya JK angalau kujaribu kuwaletea hilo jinamizi linaloitwa katiba mpya ingawa palitokea mkwamo kwa kuwa suala hilo lilipigiwa kelele na wanasiasa,kuratibiwa na wanasiasa na hatimaye kuharibiwa na wanasiasa.
Kipo kilio cha mara kwa mara cha kudai Tume huru ingawa hakuna ushahidi usio na Shaka juu ya Tume kukosa uhuru.
Nadhani kwa yanayoendelea Kenya ni wazi kuwa hakutawahi kutokee usalama katika uchaguzi hata kama Tume ya uchaguzi itakuwa chini ya malaika na Katiba ikawa kama kitabu cha msahafu au bibilia.
Kwa maoni yangu sioni haja ya kuendelea na mchakato wa katiba mpya uliokwama kwani ni upotevu wa fedha unaolenga kutafuta au kufikia matarajio yasio na mashiko.
Yaani Katiba mpya au Tume huru sio suluhisho la figisufigisu za uchaguzi...hizi zitakuwepo tu.
RIP MJUMBE WA TUME YA UCHAGUZI KENYA.