SoC01 Funzo kutoka kwangu binafsi: Dini, utii, heshima, kusaidia/kujitoa na bidii ni nguzo muhimu maishani

Stories of Change - 2021 Competition

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,307
Reaction score
25,932
Kila mtu ana lake la kusimulia maishani mwake. Laweza kuwa jema au baya; la kufurahisha au la kusikitisha na kuhuzunisha. Langu ni la kufurahisha na kufundisha. Lahusu maisha yangu binafsi. Nimeona vyema kuliweka hapa kama sehemu ya kujifunza katika kutekeleza azma ya Mtandao huu wa JamiiForums ya kuelimishana na kufundishana kwa ajili ya kusonga mbele kwa pamoja kama jamii ya kitanzania.

Nitajitahidi kuandika kwa kifupi. Mada yangu ni juu ya umuhimu wa dini, utii, heshima, kusaidia/kujitoa na bidii maishani. Mimi ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto 12 wa ndani ya ndoa ya wazazi wawili ambao wote kwasasa ni marehemu. Baba aliitwa Eusebius Petro Mselewa na Mama aliitwa Costantina Michael Mhagama. Wote walikuwa wenyeji wa mkoa wa Ruvuma(Wangoni) lakini walihamia Kibaha, Pwani tangu miaka ya 70. Na wote walifariki wakiwa hapo Kibaha.

Siandiki kama jambo la kujivunia ila naandika kwakuwa ni jambo la kweli. Kati ya watoto hao wa wazazi wetu (ambao kwasasa tumebaki 6), mimi tu ndiye niliyebahatika kuendelea na elimu ya sekondari na hata chuo kikuu. Si kwamba wenzangu hawakuwa na uwezo wa kielimu kama mimi,bali mazingira ya kimaisha ya familia na hata ustawi wa nchi kwa ujumla wake katika miaka ya 70, 80 na 90 mwanzoni yalichagiza kutoendelea kwao kimasomo.

Nilimaliza darasa la saba mwaka 1997 katika Shule ya Msingi Visiga iliyopo wilayani Kibaha, mkoani Pwani. Kwenye darasa letu la wahitimu 64, awamu ya kwanza tulifaulu wanne. Awamu ya pili waliongezeka watatu kutengeneza jumla ya wanafunzi saba tuliofaulu kwenda sekondari kutoka shuleni kwetu. Nilichaguliwa Shule ya Sekondari ya Ruvu. Wakati huohuo, nilipokuwa darasa la saba, nilifanya mtihani wa Seminari na kufaulu. Baba alinitaka nisubiri nafasi za kiserikali.

Nilianza kidato cha kwanza nikiwa mwanafunzi wa kutwa katika Shule ya Sekondari ya Ruvu. Ada ya wakati huo ilikuwa ni elfu 30 kwa mwaka na elfu 15 kwa muhula kwa mwanafunzi wa kutwa kama mimi. Ilipofika mwaka 1999 nikiwa kidato cha pili, mwezi wa sita wakati wa likizo mlipaada na baba yangu mzazi akafariki dunia. Nikabaki njiapanda. Shule zilipofunguliwa, nilibaki nyumbani kwa miezi miwili nisijue la kufanya. Tena, mwaka huo ulikuwa ni mwaka wa mtihani wa taifa na wastani wa ufaulu uliotakiwa ulikuwa ni 21.

Mkono wa Mungu ukanigusa. Nikiwa naendelea na utumishi kanisani kama mkatoliki kindakindaki, alijitokeza Marehemu Padre Mathias Mambo aliyekuwa Gombera wa St. Mary's Visiga Seminary kwa ajili ya kunishika mkono. Alifahamu uwezo wangu kitaaluma, kitabia na kidini na hivyo akakata shauri kunisaidia. Nilishakuwa nyumbani kwa miezi miwili bila lolote kuendelea. Akaniita Seminarini kwa mazungumzo. Tukazungumza na akanipa nafasi ya kuendelea na masomo kwa maana ya kunilipia ada.

Nilimuahidi kuwa mtii na mwenye bidii kwenye masomo na kuwa SITAMUANGUSHA. Nikarejea shuleni nikiwa na ari na nguvu kubwa. Ingawa nilikuwa nyuma kwa miezi miwili, nilifanya mtihani wa taifa wa kidato cha pili na kufaulu kwa wastani wa 59. Nikaendelea na elimu yangu nikisomeshwa na Marehemu Padre Mambo. Alinisomesha hadi kidato cha sita. Aliwahusisha mapadre, masista na watumishi wote wa Seminari aliyokuwa akiiongoza na kunitambulisha kama mtoto wake. Alivutiwa na uwezo wangu na utii na heshima yangu kwa watu.

Padre Mathias Mambo alifariki hata kabla sijamaliza kidato cha sita katika Shule ya Wavulana Songea. Alifariki mwaka 2003 na nilimaliza kidato cha sita mwaka 2004 mwezi Mei. Katika hali ya kustaajabisha, akiwa amelazwa hospitalini na nikienda kumtembelea na kumuaga nikielekea shuleni kuanza kidato cha sita, alinipa fedha zote na mahitaji yote ya mwaka mzima. Nilifika shuleni na kulipa kila kitu. Nilishangaza lakini nilijiweka salama kwa kulipa kabisa. Padre Mambo hakuona ufaulu wangu wa kidato cha sita na kuendelea.

Ingawa hakunishuhudia nikiwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wala Taasisi ya Mafunzo ya Sheria kwa Vitendo nikisomea shahada na stashahada za sheria, amebakia moyoni mwangu kama msaada wangu mkuu kwenye elimu na mafanikio yangu. Ameniachia mafunzo makubwa maishani mwangu. Daima alinifundisha kuamini katika uwezo wa mtu; kuheshimu wengine na kusaidia wengine kwa kujitoa hasa wenye shida. Alinisaidia kwenye shida yangu ya kupata elimu. Nami husaidia kadiri ya uwezo wangu wenye shida za kisheria na nyinginezo. Naamini katika kusaidia baada ya kusaidiwa; kutoa baada ya kupokea.

Pamoja na magumu yote niliyoyapitia, sasa ninayo nafasi adhimu ya kusaidia wengine. Kuna wakati nilikata tamaa lakini mkono wa Mungu ukanigusa. Sikuacha kusali na kuamini kuwa ningefanikiwa. Ndiyo maana, hata madaftari yangu sikuyagawa wala kuyachana baada ya nuru yangu ya kulipiwa ada kupotea. Imani yangu ikanipa matumaini. Matumaini yangu yamenifikisha nilipo.
 
Upvote 17

Huwa napata faraja sana unapoona na kuwasikia watu wema wenye unyofu wa moyo bado wapo.. Ingawa ni nguvu kuwatambua. Nafurahi sana. Kila leo kwenye majukwaa habari zinazoletwa ni ovu ovu tuu na kushabikiwa kiasi cha kuwakatisha tamaa baadhi ya watu wenye mwelekeo Mwema kwa kudhani labda matendo yao hayana Maana tena.

Asante sana watu wa Aina hii. Nchi inabarikiwa na kuepushwa na majanga mengi kupitia wema wachache waliopo.
 
Asante sana Mkuu kwa baraka zako
 
Basically, jiimarishe kiuchumi ili uweze na akiba ya kutosha. Baada ya hapo anza kusaidia wahitaji na wewe hauto athirika kwa kuwa unahifadi amaná ya kutosha.

Ukisaidia wahitaji muda huu kabla haujawa na uwezo mkubwa, utafanya mgawane umasikini. Ni hii ni taabu ya wasio na asili na mali ni wagumu kutengeneza na kujilimbikizia mali. Uchoyo ni mbinu ya kutunza pesa.
Unaweza usisaidie mtu mmoja mmoja muda huu, lakini ukatengeneza utajiri mkubwa.
Kwa kuwaajiri wafanyakazi kwa wingi, na kwa hilo utakuwa umetoa msaada mkubwa kwa jamii na nchi. Utawasomeshea watoto wao bila wewe kujua utawatibu wazazi na ndugu zao bila wewe kujua, utajenga nyumba nyingi bila wewe kujua. Unachangia kuproduce graduates kwa kugharamia elimu ya juu bila wewe kujua.
kuna mwalimu wangu wa imani aliwahi kunifundisha kuwa hakuna mtu anafilisika kwa kutoa msaada na pia huwezi kuacha kusaidia kwamba mpaka uwe na uwezo mkubwa,usipoweza kusaidia ukiwa na kidogo hata kikubwa hutaweza kusaidia!
 
Ndugu mimi ni mkatoliki mwenzako mwaminifu na mchapakazi na mhitimu wa chuo kikuu.Naomba nami unishike mkono nipate ajira ndugu!
 
Back
Top Bottom